Je, ni sahihi Mwamposa kuimba wimbo wa taifa kanisani kwake?

Hata shule ya msingi huimba wimbo wa Taifa,

Hushangai bendera ya Taifa imechorwa bungeni, wabunge wanapitia juu yake na viatu na hawana habari!!
 
Wimbo wa taifa siyo msahafu wala biblia unaimbwa shuleni,uwanja wa mpila n.k. ilimradi hautumiki vibaya.
 
Sioni kosa lake yupo sahihi hata shule za chekechea wanaimba
 
Kanisani kuna utulivu mkuu? Cha ajabu wakati wimbo unaimbwa kuna misukule ilikuwa inapiga mayowe. Sasa hapo utulivu upo wapi?
Kwa hiyo wewe huwa unamuangalia ukiwa kama nani!?
 
Kwa hiyo wewe huwa unamuangalia ukiwa kama nani!?
Sijamuangalia bali nimemsikiliza kwenye redio mkuu. Halafu hoja iliyopo mezani hapa inahusu matumizi yasiyo sahihi ya wimbo wa taifa. Tafadhali turejee kwenye hoja. Wewe unadhani Mwamposa anayo haki ya kidhalilisha wimbo wa taifa?
 
Sijamuangalia bali nimemsikiliza kwenye redio mkuu. Halafu hoja iliyopo mezani hapa inahusu matumizi yasiyo sahihi ya wimbo wa taifa. Tafadhali turejee kwenye hoja. Wewe unadhani Mwamposa anayo haki ya kidhalilisha wimbo wa taifa?
Wewe ulikuwa unamsikiliza ukiwa kama nan!?
Hoja ya misukule iliingiaje!?
 
Mimi mbona Nina proudy wa kuuimba hata nikiwa bafuni tatizo ni nini?
Tatizo wimbo wa taifa ni nembo ya taifa. Haupaswi kuimbwa kama singeli au bongofleva na una unaimbwa kwenye matukio mbalimbali sio kila mahali na kila wakati. Umeelewa mkuu?
 
Wa hiyo wimbo huu unaweza kuimbwa mahali popote pale mkuu?
Mambo mengi ninakuunga mkono, ila hili naona umechemsha. Kuikmba wimbo wa Taifa ni part of Patriotism, itakuwaje ni kufuru? Labda zile sheria za Nyerere? Wakati ule hata ukishika bendera ya Taifa unawekwa ndani
 
kanisani pangu kila Mwaka mpya na mara chache may Mosi lazima tuugonge wimbo wa Taifa 🐒

ni sehemu ya uzalendrooo lakini pia kuliweka Taifa mikononi mwa Mungu 🐒
 
Duh! Mkuu, mbona makasiriko kihivyo? Inaonekana una lako jambo. Au ulitoa sadaka ya kujimaliza halafu haikurudi kama ulivyotarajia? Pole.
1. Kwani ungelitumia lugha ya kistaarabu unadhani tusingelikuelewa? Umetukana, umedhalilisha na umedharau kupitiliza. Unawaitaje watu waliokuwa wanasali/wanamwabudu Mungu Huyo huyo anayetajwa Neno la kwanza katika wimbo wa Taifa kuwa eti ni Wahuni, ni Misukule, ni Mbwa..... Kweli broo; Hebu watake radhi hao watu ulio watusi hivyo usije kulaaniwa bure/mno.
Mkuu , yafaa uuone wimbo wa Taifa kama mojawapo ya sala nzuri esp. kwa Wakristo lakini pia na kwa Watanzania wote. au wewe hutaki Mungu aibariki nchi yetu? Unataka kinyume cha kubariki yaani laana?
Wimbo huo huimbwa mahali pengi na waliopo hapo hutulia kwa adabu na heshima kubwa huku wakiimba na kama mtu hawezi kuuimba huo wimbo wa Taifa, basi hutulia tuli. Vipi hapo kwa Mwamposa waliimba huku wakicheza sana- kuserebuka? Kama walikuwa wanacheza,wanapiga vigelegele n.k hilo sio sawa. Lakini kuimba HAWAJAKOSEA KABISA.
2. Sasa labda nikuulize kidogo; Hapo kwa Mwamposa ww ulienda kufanya nini leo Pasaka yote hii? Kuimba wimbo wa taifa ni kusali na ndo mana wimbo unaanza kwa kutamka: Mungu ibariki ........
3. Mkuu, Nakuomba siku nyingine ukijisikia, basi uende kule kwingine usiende kwa Mwamposa au Kanisani kwani kote huko wanauimba wimbo huo kama mojawapo ya sala.Tena kwa Wakatoliki ndo usijaribu kabisa kwani wao wanazo hata nota za wimbo huo na huimbwa kiufundi.
Ni hayo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…