Je, ni Speed gani kubwa zaidi ushawahi kutembea na gari au pikipiki?

Je, ni Speed gani kubwa zaidi ushawahi kutembea na gari au pikipiki?

Hiyo bei nzuri sana, juzi nilikutana na mtu ana V8 kompressor E 63 AMG nikasema haya Sasa wapendwa ligi wazee wa crown na Subaru fateni hapo 😁😁😁😁
😂😂😂Huyo kumfuata labda uwe na 2GR iliokatwa kamba yani! Kama ile masterplan ikikaa vizuri itabidi tuweke kichwa kimoja maalum kwa ajili ya kukata kamba za mjapan.

Itakuwa entry strategy nzuri kwenye soko.
 
Sehemu ndefu mnazungumzia gari gani? Kwani hizo 2jz si mnasema zina nguvu kuliko 4gr? Mbona 4gr sekunde kadhaa tu imefutwa sahani?
Wanasema na gearbox ( aina ya gearbox ) inachangia kitu kuchomoka chap chap plus other technology ambazo zipo Kwa engine
 
😂😂😂Huyo kumfuata labda uwe na 2GR iliokatwa kamba yani! Kama ile masterplan ikikaa vizuri itabidi tuweke kichwa kimoja maalum kwa ajili ya kukata kamba za mjapan.

Itakuwa entry strategy nzuri kwenye soko.
Masikhara hayo mzee!
Kwa hizi specs, Crown hata ikikatwa kamba itaweza kweli? Labda kwa stage 2 tuning ya maana kidogo!
Screenshot_20220719-220416_Chrome.jpg
 
Duuh mie 130 tu na ka-corolla kangu ila niliona kanatetemeka nikarudi kwenye speed pendwa around 90 - 100 zaidi ya hapo nikiwa na-overtake au nipo kwenye zile barabara zinazoonyesha uende zaidi ya 80 maeneo ya Shelui - Igunga kuitafuta Nzega

Ila mngekuwa mnatuambia hizo speed mlikuwa mnakwenda nazo kwa umbali gani maana barabara zetu nazo changamoto, ukikanyaga baada ya kilometa chache unakutana na tuta au kona kali au repair ya barabara / kajishimo
 
Kwema wakuu, je ni speed gani kubwa zaidi ushawahi kutembea na gari au pikipiki na ilikuwa ni gari gani au pikipiki gani...
Mi nlidhani umewahi kuendesha gari kwa speed ya juu sana kumbe unazungumzia hizi za kawaida za 180 mpaka 190?

Ulikuwa unaendesha msafara wa harusi? Sasa sisi ambao tumeendesha speed mpaka 300 si tungeanzisha forum au website kabisa? Wewe wa speed 180 unaanzisha uzi? Aisee....umenichosha kbisa.
 
Ikishafika 150km/h nakosa amani. Na hiyo niliifikia zamani kwenye 2016 BMW 3i. Hizi gari zetu nyepesi Raum na Dualis sizidi 120km/h.

Nimeshasalimika ajali Mara mbili nikizidi hapo naanza kutetemeka hata bila kujua kwanini. Nnakosa utulivu kabisa.
 
Back
Top Bottom