Je, ni Speed gani kubwa zaidi ushawahi kutembea na gari au pikipiki?

Daah safi sanaaaaa,
Raha ya mwendo kasi hata ikitokea imekushinda israil anakuja fastaa sio unapata ajali unavunjika vunjika unawapa tabu watu kukuuguza.
 
Nikikumbuka kuna Rafiki yangu alikua na volkswagen nilitembea umbali wa Kilomita 120 ilibaki Kilomita 60 nifike safari yangu, Bwana yule akaanza Kilomita kama 10 hivi akaja kunikata njiani Kilomita 60 sijamaliza kwa kweli kuna Watu wanatembea!!!!!......
 
LC 200 GXR

Niligonga 200KPH lakini kuna muda niligusa hadi 240KPH ambayo ndiyo mwisho wa kisahani

Ilikuwa Mafinga to Makambako tulikuwa tunatoka Dar kuenda Mbeya na tulikuwa tunapokezana kuendesha
Itakuwa kipande cha Saohil pale hakuna tuta sana afu kuna sehem barabara imenyoka kinoma na ile sehemu baada ya Nyololo kwa mbele ndio waweza tembea hivo
 
Siku moja tunatoka mbeya harusini kurudi dar sie tuna crown royal salon 4gr-fse kipande cha kumaliza kitonga hapa kuishusha down fortuner hiyoo apo! Mbele kuna alteza...

Kuna kale kamchezo njia nzima mkiwa road za mikoani mnakutana mko watatu mnaongozana na hamtaki kuachana tukamkata fortuner na alteza hiyo tukaila..
Heee![emoji16] fortuner hajakubali katuacha tukamtuliza alteza maana yeye Ana 3sGE tukamwambia kiishara tulia ligi huwezi..

Jamaa wa fortuner tulinyoosha nae hadi msamvu maana yeye alikua anaenda dom tukaachana hapo lakini najua jamaa alikubali mziki.[emoji16]


Nyingine tulikuwa tunatoka msibani saa 8 ivi mchana tunaludi zetu dar tukiwa ndani ya lc j200... watu kama 6 hivi.Tupo katikati ya swanga na tunduma discovery 5 na range
Rover evoque zikatupita shwaaaaah! Wanao ijua barabara ilivyo saii from tunduma mpaka swanga wananielewa road inashawishi ukanyage! Dah tuliwatamani sema nikwavile tumetoka mazikoni tukaona isiwe tabu acha wapite
Tusije kuludisha msiba kwa mara nyingine..

Saa 10 tunafika uyole pale tumemaliza kula tunasepa wale jamaa kumbe nao walipitia mahali tunawaona hao tukavutiwa kuwafata sema tulikuwa na wamama kama wawili waoga aah! Tukawaacha waende tena alafu zile gari zilikuwa za ubalozi zimekula tinted tiiii! Ligi ni tamu bana![emoji16]
 
Opa kuelekea bagamoyo sio mzoefu ila mpambe ndo alikua fundi nikiwa sina shaka huku tuna piga story jamaa ananambiaa punguza ndo nimuanglie badala yake nikaona miti inavo pepea nikaogopa naakuanza kukaza mikono mpaka ilivo rudi 70 kwa 80
 
120 kph kwa gari isiyo na mawenge ya kuyumba, ni mwendo wa kawaida sana. Kuanzia 140kph na kuendelea, gari inakuwa nyepesi sana. Na hata umakini kwa dereva huongezeka.
Eeeeh hiyo huwa naendesha nikiwa na jamaa zangu tu , mama hakawi kusema utembee 60, sema gari nilokuwa nayo ni carina ukitembea juu sana ya 120 inakuwa nyepesi , huwa natembea hivo mkeka wa Iyovi via Iringa to Igawa road pana sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…