Je, ni wakati gani muafaka kwa mzazi kuwabariki watoto wake?

Je, ni wakati gani muafaka kwa mzazi kuwabariki watoto wake?

Mila na desturi za zamani zilimnyima mwanamke haki, utamaduni wa kubariki ulikua kwa wanaume lakini haimaanishi mke wa isaka angembariki mtoto basi baraka isingefika.

Soma kumbukumbu 30:19 Matendo yetu ndiyo yanaamua tupate baraka au laana
Ni vizuri mkuu kwa kufanya marejeo ya mandiko.

Lakini tumeona jinsi Isaka alivyoishiwa baraka zote kwa mtoto mmoja tu, hakuweza kumbariki yule mwingine.

Na wakati huo tunaona mama hakuhusika na baraka zozote ukiachana na zile figisu alizofanya.
 
Baraka hutolewa kwa kumtamkia au kumnuia yale mema unayomtakia kwenye maisha yake, kwa mujibu wa historia za vitabu vitakatifu..... hii ilifanyika kama hafla maalumu na sio kujisemea tu moyoni au kila siku.
Kwahiyo kumtamkia mema mwanao mpaka upange siku maalum?

Baraka sio maneno Bali matendo unayomfanyia mwanao Kila siku iendayo
 
Upo uzi humu ulielezea hizo baraka vizuri tu,shida mkisoma hamuelewi na hata mkielewa hamuamini,baraka sio maneno wazee baraka ni kitu cha kushikika kabisa sio maneno tu kama mnavyojidanganya na ndo maana inaisha na hapewi kila mtu,ingekuwa ni maneno tu basi yasingeisha na kila mtu angepata,Mungu alimueka alama kaini ili asiuliwe na raia wengine huko aendako baada ya kumuua nduguye,Daudi alipakwa mafuta ili awe mfalme na kadhalika na kadhalika.Kifupi baraka au laana ni kama uchawi tu,mtu anapewa laivu na sio maneno kama muaminivyo.na hakuna laana ya kuvua nguo au kutamka kama hakuna means zingine za kijadi hazijatumika,kwa leo naishia hapa.
 
Kwahiyo kumtamkia mema mwanao mpaka upange siku maalum?

Baraka sio maneno Bali matendo unayomfanyia mwanao Kila siku iendayo
Sio rahisi hivyo, japo hivi ndivyo wengi wetu hudhani.... hizo blah blah za kuambiwa tu eti "Mungu akubariki" huwa ni porojo tu.
 
Wengi humu mnajadili mawazo yenu, kwa maoni yenu.... na pengine mazoea au mapokeo tu.

Lakini hamna msingi wala hadidu zozote.
 
Biblia haieleweki au wanaoifata hawaielewi ndo maana hiyohiyo biblia imekataza kula nguruwe lakini wafuasi wa biblia wanakula kwahiyo usitegemee kupata suluhu ya chochote ndani ya hicho kitabu.
 
Biblia haieleweki au wanaoifata hawaielewi ndo maana hiyohiyo biblia imekataza kula nguruwe lakini wafuasi wa biblia wanakula kwahiyo usitegemee kupata suluhu ya chochote ndani ya hicho kitabu.
Aisee!
 
Baraka hutolewa kwa kumtamkia au kumnuia yale mema unayomtakia kwenye maisha yake, kwa mujibu wa historia za vitabu vitakatifu..... hii ilifanyika kama hafla maalumu na sio kujisemea tu moyoni au kila siku.
Sio maneno/maneno/maneno..../maneno tu na blahblah nyingi! Muwekee msingi wa kufanikiwa ikiwa ni pamoja na kumkazania kufanyakazi kwa bidii juhudi na maarifa. Kusoma, heshima, kujua nafasi ya Mungu! Zaidi wekeza kwenye lasirimali! Sio kukaria mambo sijui ya kunuia kutamka sijui nini??? Uo ni ujinga na kurithishana UMASIKINI
 
Back
Top Bottom