Kuna tatizo kubwa sana kuhusu uchaguzi huru wazi na wa haki nchi hii kiasi cha kwamba kila mwananchi amekata tamaa na suala hili.
Mimi na wananchi tunajiuliza tatizo ni kukosekana kwa utashi wa kisiasa na Rais na viongozi wengine kuwa na utashi wa kisiasa wa kutoa miongozo thabiti ya walio chini kuzingatia sheria, kanuni za uchaguzi zilizopo na matokeo ya ukiukwaji ni nini?
Hapa utashi wa kisiasa wa kweli unahitajika haijalishi ni katiba au sheria gani zilizopo. Hii ni pamoja na vyombo vyote vya dola, Tume na mahakama kutenda haki katika kusimamia uchaguzi.
Hili akilisimamia Rais kwa dhati bila kuwasikiliza wapambe na machawa tutapiga hatua. Baada ya hapo ndipo pengine tupitie sheria zetu kuondoa kasoro.
Mimi ninaamini maboresho ya katiba, Sheria na kanuni sambamba na Utashi wa kisiasa havitengani ni mapacha.
Hapa HAKI, HAKI, HAKI inapaswa itamalaki katika mifumo yetu, hii ni pamoja na kujenga ustaarabu na utamaduni wa kupenda ushindani bila kufikiria madaraka zaidi ya maslahi ya wananchi. Tumeona angalau mfano kidogo wa uchaguzi wa juzi wa Chadema.
Imewezekana. No reform no Election itakuwq na maana kama Rais akitaka na Serikali nzima ikamwelewa kuhusu mwelekeo mpya kwa vile wanufaika wa uchaguzi mbovu ni wengi mno.