Jana usiku muda kama ya saa saba niko kb pub tegeta opposite na Kibo complex, sasa ile natoka nje nile fegi naona mapira mawili wazee kibao hadi wananing'nia nikshtuka sema nikakausha nikaendelea kula fegi yangu, wale wazee wakapaki mbele ya pub mmoja akashuka akaingia ndani nahisi alienda kuzima mziki ndani ya dk sifuri wale wazee walikurupuka kwenye yale magari wanapiga watu hovyo kila mtu anakimbilia anakojua tukakimbia hadi tegeta kbaoni ndio kuulizana kwani kuna nini bodaboda wakatuambia panya road wamezingua huko chini, ikabidi nibadilishe Kiwanja hadi bm pub wazohill, nimechukua bia yangu kabla haijafika nusu naona mziki unazimwa na taa pia kuuliza wakasema polisi wanapita viwanja vyote kuzima mziki wakidai kudhibiti panya road, kusema kweli polisi wamefeli kudhibiti hivyo vitoto wao wenyewe wanaviogopa.