Je, Panya Road wamewashinda? Wamerudi kwa kasi ya kutisha sana

Je, Panya Road wamewashinda? Wamerudi kwa kasi ya kutisha sana

Mtaa unapaswa uwe na Ulinzi shirikishi,
Kama hauna,
Wanaume wa mtaa huo hasa wababa wa familia waitishe kikao cha dharura kuwakabili hao wahuni.

Itafaa akipatikana mmoja Kati ya kumi WA mfano ambaye mtamuadhibu Kwa kiwango cha juu kabisa ambacho itakuwa funzo Kwa wengine.
Robert Heriel:

Polisi jamii ni hao hao panya road na wezi, na wanatuhuma nyingi za uporaji usiku. Nina uhakika wewe hulindi mkuu. Kwanza hakuna tukio linaweza kutokea mahali popote wasiju, na panya road wanaofanya hivyo vitendo wapo na wanajulikana.
 
Kunawakati mwizi anaiba, alafu anakimbizwa,watu wanamuungia tu mtaa hadi mtaa mbaka anakamatwa.

Muhusika alieibiwa hajulikani,mwizi anapigwa sana.
Police wanakuja watu wanatawanyika wote hakuna anaeenda kutoa ushahidi.
Mwizi anafikishwa police' then hakuna mlalamikaji mwisho wasiku mwizi anaachiwa sababu hakuna mlalaikaji na police huenda wanashindwa kumpeleka mahakamani sababu alieibiwa hajulikani.
Mwisho wasiku kamakunapolice mwenye tamaa anachukua kiwiyake anamwachia mwizi mtuhumiwa aendelee namaisha yake.
Raiya tukimuona mtaani tunaanza kuwalaumu police kwamba wameshindwa kumfunga,tunasahau sisi ndio tunaotakiwa kuonyesha ushirikiano police ili kutoaushahidi mahakamani ilimwizi afungwe.

Tusipo badilika majizi tutayaona yana jitamba tu mitaani kilasiku labda tuyanyang'anye silahazao harakaharaka.
tatizo la wananchi kukimbia unaijua. rushwa ubambikaji wa makosa mpaka utoke! si bora ukimbie
 
Unadhani polisi wapo wengi sana kiasi cha kutosha kulinda kila mtu?

....jukumu la usalama lianzie kwenu
Sawa kabisa kaka, kumbuka, panya rodi wako na siraha, na raia haruhusiwi kuwa na siraha, siraha ziko police,

Linapotokea hilo, nguvu ya police itumike
 
Nyie endeleeni kulialia mtandaoni hadi mlawitiwe wote na wake zenu wakat hapo mtaani mnaweza kujipanga mkawadhibiti nyie mnawaza tu kufanya scrub na kuvaa suruali fupi na viatu bila soksi mtapakuliwa Hadi akili iwakae sawa, wanaume wa dar bana.

mtaani mko wanaume 100 mnavamiwa na vijana 20 mnashindwa kujipanga ili kukabiliana nao Hadi watokomee? Na mnajua kabisa ni kikundi kinacho fanya matukio Mara kwa Mara? Hivi mkipiga doria ya maana mkakamata hata watatu mkawachinja na kupiga Moto wenzao wakiona mnafikiri wataendelea kuwepo?
Couldn't help..nimecheka sana[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Jamaa yangu anaishi Makubuli anasema hawa watu wamerudi kwa kasi kubwa,ari na guvu kubwa sana. Wanaweza pora nyumba mpaka 20 kwa usiku mmoja. Ni vijana wa umri wa miaka 12-30 wanakuwa wengi wakiwa na mapanga ,visu ,magongo na bisibisi. Kiukweli wameuteka mji wa Dar es Salaam. Nadhani kwa hiki kipindi ambacho polisi wapo mapumziko tutapata shida sana. Mpaka wakimaliza likizo Polisi hali itakuwa tete. Tuuombe Mungu sana.

Serikali yetu sikivu yenye kutujali na kutupenda je bado hamjapewa hizi habari? yaani kuna watu washavamiw ana kudhuriwa zaidi ya mara tatu na wakiepeleka taarifa polisi wanawaambia "wewe siyo mtu wa kwanza kushambuliwa na hao vibaka andika maelezo tutafuatilia" inaishia hapo. imekuwa ni jambo la kawaida na polisi haw aamabo tunawalipa mshahara wanaonekana kutoshtushwa kabisa na jambo hili. tunaomba serikali kwa kweli iingilie kati suala hili kwa ajili ya usalama wa wapiga kura wake na wachangia kodi.

Jamani sisi wananchi wote tukiuliwa nchini wakabaki panya road penye yao ninyi viongozi nani atawachangia kodi ambayo ndiyo inawasaidia kuzunguka nchini kwenye helkopta kuhamasisha anuani za makazi? au kwenda kuzinduliwa huko Ulaya na Marekani? Tumsaidie Rais wetu jamani mbona kama kila kitu mmemuachia yeye tu. yeye uzinduzi , yeye kusafiri kujielezea, yeye kila kitu ninyi mnafanya nini?
Kila mtu ale kulingana na urefu wa kamba yake.
 
Mtaa unapaswa uwe na Ulinzi shirikishi,
Kama hauna,
Wanaume wa mtaa huo hasa wababa wa familia waitishe kikao cha dharura kuwakabili hao wahuni.

Itafaa akipatikana mmoja Kati ya kumi WA mfano ambaye mtamuadhibu Kwa kiwango cha juu kabisa ambacho itakuwa funzo Kwa wengine.
Kwanini yanatokea sasa.
 
Muliro jumanne muliro atawashughulikia hao wote na hali itakuwa shwari kabisa.
 
tatizo la wananchi kukimbia unaijua. rushwa ubambikaji wa makosa mpaka utoke! si bora ukimbie
Gharama ya kukipata kitu chako ni bora uchange ukanunue kipya.
Utaombwa vocha,hela ya mafuta,nauli,hela ya kula yaani uliyeibiwa unageuzwa dili hawa jamaa wanakula kotekote.Kibaka nae kama hakuna mlalamikaji,anaombwa rushwa anatoka.
 
Njia pekee ya kudili na watu primitives ni kuwafanyia uprimitives zaid.
Kule Dar kwa wakurya ukiingia 18 unakamatwa njemba kama sita au zaidi hizi unakamatwa kichwa unatikishwa kwa nguvu sana kisha unaambiwa nenda tumekusamehe
 
Undeni vikundi vyenu vya ulinzi shirikishi mjilinde wenyewe acheni uoga.

Halafu hao ni vijana wenu mnaishi nao huko kwenu huenda hayo ni matokeo ya malezi mliyowapa, jiulizeni mlikosea wapi.
Umetoka kazini umechoka,unawacha kulala unaenda kukesha kupigwa na baridi unalinda sungusungu?

Hawa maskarii kazi yao ni nini?
Wanalipwa kwa kodi zetu na bado tuwasaidie majukum yao?
 
Abiria chunga mzigo wako.
Police awafiki hata laki Moja tupo milioni 60 nani watalindwa nani waache, halafu kuondoa Mende mtaani siyo Kazi ya police hio ni ya jamii husika.
Jamii ikijichukulia sheria mkononi na njia hiyo ikaonekana ni kawaida na ndio suluhisho sijui mwisho wake itakuaje.
 
Back
Top Bottom