Je, pesa uliyonayo itamudu gharama za maisha yako kwa miaka mingapi bila kufanya kazi?

Je, pesa uliyonayo itamudu gharama za maisha yako kwa miaka mingapi bila kufanya kazi?

Mwaka mzima million 2, so hauna familia wala majukumu ya ndugu?
Inamaanisha kwa siku anatumia Tshs 5,000/-
Ambayo chakula kwa Mama ntilie ni Tshs 1,500 @2 Jumla ni Tshs 3,000 na chai ni Tshs 800. Bado vocha na Nauli.
Tafuta pesa ndugu
 
Kwa TZ ni chini ya asilimia 0.3 wanaoweza kutoboa mwaka tu bila kufanya kazi na wakaishi ndani ya huo mwaka kama kawaida.
 
ndo ivo mkuu maisha hayatabiriki.

Kuna ndugu yang mbagara mwaka fulan aliugua, akaenda kujitibia india.
Alitumia kama 30milions, bila kuchangsha ndugu, na hakuyumba

Ase ilinifkilsha sana, kama huna unakufa ndugu wanakujaga kujitoa msiban.

Niliwaza kumbe ninasafari ndefu nijipambanie
Huyo jamaa yako hakutumia akili na yeye. Kwanini hiyo hela yote asingekata bima kubwa ya afya, nina hakika asingetumia hiyo hela yote kwa matibabu.
 
Hii ni wastani wa 179,166/= kwa mwezi. Mkuu unaishije kwa kiasi hiki? Yani chakula, bundle la kuingia JF, makazi, usafiri, na kadhalika? Au ni content tu??

Aidha, naunga mkono hoja kwamba inabidi mtu uwe na akiba ya kiasi fulani ambayo ikitokea chanzo chako cha active income hakiwezi tena kukupa pesa, akiba hiyo itakutosheleza kwa kiasi cha angalau miezi sita.​
Hapo kutoboa mwezi labda amejenga nyumba hivyo halipi kodi, chakula angalau uwe na shamba usinunue unga wala mboga za bustani, uwe na mifugo kama kuku, ng'ombe usinunue mayai na maziwa, usafiri unatumia baiskeli ili usilipe nauli, uwe na bima ndogo ya kukutibu wewe na wanaokutegemea, mwisho kabisa uwe umeoa ili usitumie hela ovyo kwa wale machangudoa.
 
Inamaanisha kwa siku anatumia Tshs 5,000/-
Ambayo chakula kwa Mama ntilie ni Tshs 1,500 @2 Jumla ni Tshs 3,000 na chai ni Tshs 800. Bado vocha na Nauli.
Tafuta pesa ndugu
hapo kwenye chakula ndipo naposave, huwa najipikia mwenyew mkuu
 
Hapo kutoboa mwezi labda amejenga nyumba hivyo halipi kodi, chakula angalau uwe na shamba usinunue unga wala mboga za bustani, uwe na mifugo kama kuku, usinunue mayai, usafiri unatumia baiskeli ili usilipe nauli, uwe na bima ndogo ya kukutibu wewe na wanaokutegemea, mwisho kabisa uwe umeoa ili usitumie hela ovyo kwa wale machangudoa.
sahihi kabxa mkuu, nalo neno.

Ila mim cjaoa nimepanga ila kulima nalima.
 
Hongera ila professionally hiyo sio faida.
Faida ni pale unapotoa costs (gharama za kwenye biashara) kutoka kwenye total revenue ( mapato ya kwenye biashara) ndio unapata faida. Hiyo tunaweza kuita savings pengine, sio faida.
 
sawa sawa! umeeleweka vyema mkuu.
 
Back
Top Bottom