Je, pesa uliyonayo itamudu gharama za maisha yako kwa miaka mingapi bila kufanya kazi?

Mwaka mzima million 2, so hauna familia wala majukumu ya ndugu?
Inamaanisha kwa siku anatumia Tshs 5,000/-
Ambayo chakula kwa Mama ntilie ni Tshs 1,500 @2 Jumla ni Tshs 3,000 na chai ni Tshs 800. Bado vocha na Nauli.
Tafuta pesa ndugu
 
Kwa TZ ni chini ya asilimia 0.3 wanaoweza kutoboa mwaka tu bila kufanya kazi na wakaishi ndani ya huo mwaka kama kawaida.
 
Huyo jamaa yako hakutumia akili na yeye. Kwanini hiyo hela yote asingekata bima kubwa ya afya, nina hakika asingetumia hiyo hela yote kwa matibabu.
 
Hapo kutoboa mwezi labda amejenga nyumba hivyo halipi kodi, chakula angalau uwe na shamba usinunue unga wala mboga za bustani, uwe na mifugo kama kuku, ng'ombe usinunue mayai na maziwa, usafiri unatumia baiskeli ili usilipe nauli, uwe na bima ndogo ya kukutibu wewe na wanaokutegemea, mwisho kabisa uwe umeoa ili usitumie hela ovyo kwa wale machangudoa.
 
Inamaanisha kwa siku anatumia Tshs 5,000/-
Ambayo chakula kwa Mama ntilie ni Tshs 1,500 @2 Jumla ni Tshs 3,000 na chai ni Tshs 800. Bado vocha na Nauli.
Tafuta pesa ndugu
hapo kwenye chakula ndipo naposave, huwa najipikia mwenyew mkuu
 
sahihi kabxa mkuu, nalo neno.

Ila mim cjaoa nimepanga ila kulima nalima.
 
Hongera ila professionally hiyo sio faida.
Faida ni pale unapotoa costs (gharama za kwenye biashara) kutoka kwenye total revenue ( mapato ya kwenye biashara) ndio unapata faida. Hiyo tunaweza kuita savings pengine, sio faida.
 
sawa sawa! umeeleweka vyema mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…