Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Rest in peace Aquilina
 
Ilikuwa kuwe na majeneza zaidi moja wapo liwe LA polis wanapenda kutumika kwa ccm kwa ujinga mkubwa

Nchi masikini.. askari hawana mafunzo ya kupambana na RAIA wanaoandamana..ANGALIA nchi zilizoendela ASKARI wote wana skills za kupambana na waandamanaji... Wanasoma na Kufundishwa nadharia na VITENDO.......
 
Kweli kabisa polisi walipiga risasi kwenye anga zao huko juu angani ukikatizi tu umelengwa.
Rest In Peace Binti Aquilina. Nimesikia wakisema aliuawa na kitu chenye ncha kali refer Kipindi cha Nipashe Radio One leo sa 12;30asubuhi!
 
Inasikitisha sana...

Inastajabisha sana...

Laiti vibali vingetolewa mapema kwa muji wa taratibu na sheria tusingefika hapa...

cc: mahondaw
 
Paskali umesema “Kilichotokea ni uzembe tuu wa polisi wetu na hakuna excuse yoyote itakayo weza kutolewa ku justify uzembe huu wa jeshi letu la polisi kupoteza maisha ya an innocent civilian just like that” Kwa maoni yangu ninachelea kuona kama ni uzembe tuu kwa vile wakubwa wanaotoa amri kwa polisi wameshasema watashinda kwa gharama yoyote ile. Hivyo hivi vifo vya left center and right ni mkakati wa kutawala kwa gharama yoyote ile. Mbona miaka ya nyuma haya mauaji holela hatukuyaona kwa kiwango cha kutisha hivi?
 
Kunatetesi kwamba waliokusudiwa ni mbowe na mnyika ile gari ndo nusura yao
Na hiyo ilikuwa ni ahadi ya Rais kuwa kama kutakuwa na maandamano anataka viongozi wa CDM wakae mbele, wataona atakachowafanya. Lakini kila afanyacho kinaenda tofauti.

Lisu haikuwezekana. Mbowe imeshindikana. Akiendelea, kuna siku atawalenga viongozi wa CDM watakaopoteza maisha ni wanawe. Mungu hadhihakiwi.
 
We p.u.m.b.a.v.u sana wewe! Unashangaa mbowe kutafutwa na polisi as if hujui nani aliitisha maandamano haramu, muda wa usiku, na aliyesema wako tayari kutangulia mbele za haki!!!
 
We p.u.m.b.a.v.u sana wewe! Unashangaa mbowe kutafutwa na polisi as if hujui nani aliitisha maandamano haramu, muda wa usiku, na aliyesema wako tayari kutangulia mbele za haki!!!
Kumbe na wewe mwehu kama baba yako?
 
Nani alaumiwe kifo Akwilina Akwilini?
Ni CHADEMA au jeshi la polisi au serikali ya CCM au Watanzania wote?

Wafuasi wa CCM wanasema viongozi wa CHADEMA na waandamanaji.
Nani alipiga risasi ni polisi au CHADEMA na wafuasi wake?
Hapa tunaangalia matumizi ya silaha au tunaangalia nani kaanzisha maandamano?
Sawa CHADEMA kaanzisha maandamano, je alikuwa anadai nini? Ni haki yake kikatiba?

Kwa nini tunalaumu jeshi la polisi?
1.Jeshi la polisi linathamini matumizi ya nguvu kuliko matumizi bila shuruti.
2. Jeshi la polisi na viongozi wake linatumika kisiasa, majibu yao kisiasa sana. Tujiulize polisi wakipewa bunduki huandikisha idadi ya risasi ndani ya bunduki pia zikitumika huandika ripoti maalumu ya matumizi yake.Risasi moja ilitumika wakague bunduki hizo na itafahamika nani ametumia? Au ni ngumu zilitumika nyingi?

Kwa nini tunailaumu serikali awamu ya tano?
1:Matukio ya utekaji,vifo au kupotea kwa watu yamekuwa ya kawaida katika serikali ni. Na hakuna anaejali serikali haiwajibiki.
Tundu Lissu kapigwa risasi hamna majibu hadi leo. Ben Saa nane hadi leo. ROMA na Moni walitekwa hamna majibu ya maana.Mwandishi wa habari wa Mwananchi Azory hadi leo haonekani.

2: Serikali inakubali kurudia chaguzi ndogo kila kukicha inatumia mabilioni ya pesa bila msingi. Tunaweza sema serikali inataka kuunda mfumo wa chama kimoja nchini inatumia pesa vilivyo na dola vilivyo juu ya kifo cha Akwilina Akwilini ni mmoja kwa mmoja polisi walitumwa kuzuia maandamano.

Kwa nini Mwigulu Nchemba ajiudhuru?
Kwa matukio haya yalioshamiri yanatokana na uzembe wa wizara yake, na yeye ni kama awajibiki. Hawezekani hamna masuluhisho ya vitendo hivi na si vigeni Tanzania kwamba havijui.Kujiudhuru kisiasa ni kawaida, kujiudhuru ni kukubali kuwajibika na kupinga vitendo hivi pia ni ishara ya uzalendo.

Kwa nini watanzania wote tulaumiwe?
Tumetanguliza siasa sana tumeshindwa kuungana tubadilishe mifumo hii duni. Vyama vya siasa vimetugawa ila tunasahau hamna tatizo la CHADEMA bali kuna tatizo la watanzania.Binti Aquelina huenda hakuwa sio mwanachama wa chama chochote nchini lakini kapigwa risasi kapoteza maisha yake. Tundu Lissu alipigwa risasi tulishindwa kuungana, Ben Saa Nane kapotea hatukuungana. Ila siku apigwe risasi au atekwe mamako au babako au ndugu yako yoyote nadhani utajua wa umuhimu wa kinga ni bora kuliko tiba.

USHAURI
Watanzania tuache siasa kwenye mambo ya msingi tusitupiane lawama wakati mizizi ya matatizo tunaifahamu. Kuna mtanzania hajui mifumo ya siasa nchini ni mibovu?
Au kuna mtanzania hajui utendaji kazi wa jeshi letu la polisi ni duni?
Au hatujui siasa za chama tawala ni duni?
Hiyo ndio mizizi ya matatizo hayo sio kutupiana lawama CHADEMA hawana hatia walikuwa wanatekeleza haki yao kikatiba ila chanzo ni mifumo duni ya siasa,siasa za chama tawala na utendaji duni wa jeshi la polisi.
Ifike pahala tufanye siasa zenye manufaa kwa nchi yetu, Serikali awamu ya tano ina mazuri na madhaifu yake. Tusilaumu tukaacha kutatua mizozo ya matatizo yetu. Kuna wengine CCM wanashangilia mnashangilia nini? wakati hili tatizo ni la kitaifa sio tatizo la WAPINZANI.

Ni bora usiwe mwanaCCM au mwanaCHADEMA ukawa mtanganyika au mzanzibari na upaze sauti mtanganyika au mzanzibari atapofanyia ndivyo sivyo.
 
Hivi ingetumika walau % 0.3 ya busara ya Kenyatta unadhanj yangetokea Hays.
 
Tatizo lilianzishwa na mkuu wa nchi pale aliposema upinzani wakiandamana watakiona, ilikuwa maandamano ya kupinga udikteta,polisi wakaingia barabarani kufanya mazoezi ya kuwapiga waandamanaji,viongozi wa dini wakaingilia kati,wakashauri maandamano yasitishwe kwanza ili wao vingozi wa dini wakamuone rais juu matatizo yaliyosababisha maandamano,leo hii ni mwaka wa pili unakaribia rais hajawa radhi kukutana nao,lakini yuko makanisani akiomba aombewe ila yeye akiombwa wakutane kwa matatizo ya nchi hataki,kwa hiyo ile amri/maelekezo aliyotoa kuwa wakiandamana washughulikiwe ndiyo inaendelea kutekelezwa,Mungu twakuomba utunusuru na hii sintofahamu nchini mwetu
 
Kwa nini unatafuta wa kumlaumu? Halafu iweje? Kwa nini tusijadili ni namna gani ya kuepusha vifo vya kizembe kama hivy tena??
 
Nafikiri mtoa hoja sasa umepata majibu namna shauri hili kilipofikia. Hii ndiyo Tanzania Mpyaa tuliyoitaka!!

Kudai haki yako kunapogeuka kosa - tena ukuzubaa unapigwa lile la lomesha la mauaji ama uhaini... ukome!!
 
Nimemkumbuka Akwiline, kumbe polisi wetu wanaweza kusambaratisha maandamano yasiyo na kibali kwa kutumia nguvu kidogo tuu bila kusababisha maafa.

Hii ni kufuatia jinsi maandamano ya jana ubalozi wa Africa Kusini yalivyosambaratishwa.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…