Wanabodi,
Kwanza nitoe pole kwa kifo hiki cha malaika huyu
Jee mnajua Jeshi la Polisi Linaweza kushitakiwa kwa kifo hiki cha uzembe na wahusika kuhukumiwa kama kifo cha Mwangosi, lakini pia serikali ikashitakiwa kwa kesi ya madai na kuhukumiwa kulipa fidia kwa familia ya marehemu?.
Kuna mazingira ambayo polisi wanaweza kumuua raia wa kawaida katika polisi shootout na polisi wasiwe na criminal liability kama tukio hilo linahusisha matumizi halali ya risasi za moto kwa mujibu wa miongozo yao, lakini tukio lile ni kuthibiti riots, hivyo tangu lini jeshi la polisi linatumia risasi za moto kuthibiti riots za watu wasio na silaha zozote badala ya kutumia rubber bullets?!.
Tena kuna ushahidi wa kutosha na usiotia shaka, mara nyingi uvunjifu wa amani unasababishwa na polisi wanaodhibiti maandamano hayo!. Kama polisi wangesimamia na kuwapa ulinzi Chadema katika kufuata viapo vyao ili wakiona vurugu ndipo waungilie, what did they stand to loose?. Kilichotokea ni uzembe tuu wa polisi wetu na hakuna excuse yoyote itakayo weza kutolewa ku justify uzembe huu wa jeshi letu la polisi kupoteza maisha ya an innocent civilian just like that!.
Poleni sana, wazazi, wanafunzi wenzake, ndugu, jamaa, marafiki, wana Kinondoni wote na wote walioguswa na kifo hiki.
Serikali yetu lazima itoe taarifa rasmi kulaani mauaji haya, na ikibidi kugharimia mazishi, na kutoa pole nene ya ubani, kuwafariji wafiwa na kuwapooza, ili wasiende mahakamani!. Kifo cha Imran Kombe, mjane aliishitaki Serikali mahakamani na kulipwa kifuta machozi cha shilling milioni 300!.
Kama hizi ndizo gharama za
demokrasia ambayo Watanzania wanalazimishwa kuilipa ili tuu fulani ashinde!, bora tufute vyama vingi, turudi kwenye mfomo wa chama kimoja, CCM iachwe itawale peke yake!. Lakini yote haya Mungu yupo na haya anayaona!.
Rip, mwanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa kozi ya Procurement $ Logistics Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Aqulina Akwilini Baftaha, baada ya kufariki kwa dunia kwa kupigwa risasi iliyompata akiwa ndani ya basi la dala dala lililopita eneo la tukio.
Paskali