Je, Protase Rugambwa ndiye Kardinali ajaye Tanzania?

Rev. Ruwai'chi siyo Kardinali bali ni Askofu Mkuu Mwandamizi wadhifa fanani na Rev. Protase Rugambwa.

Kardinali pekee wa Kanisa Katoliki-Tanzania ni Rev. Kardinali Polycarp Pengo.
Ruwaichi ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam
Sio Askofu Mkuu Mwandamizi kama ulivyoeleza hapo juu.
 
Pamoja na uzoefu wake lakini nadhani hatoweza kuwa Kardinali kwa sababu ofisi ya Vatikan inaweza kuogopa kuonyesha hali ya upendeleo kwenye ukoo wa Rugambwa, kumbuka Kardinali wa kwanza Tanzania alikuwa ni kwenye ukoo huo, Laurean Rugambwa.
Hawana Undugu wowote na Laurean Kardinali Rugambwa.
Protase Rugambwa alizaliwa Mwaka ambao Kardinali Rugambwa alipewa hadhi ya kuwa Kardinali wa kwanza Mwafrika. Hivyo wazazi wake wakampa jina Rugambwa kwa heshima hiyo.
 
Pamoja na uzoefu wake lakini nadhani hatoweza kuwa Kardinali kwa sababu ofisi ya Vatikan inaweza kuogopa kuonyesha hali ya upendeleo kwenye ukoo wa Rugambwa, kumbuka Kardinali wa kwanza Tanzania alikuwa ni kwenye ukoo huo, Laurean Rugambwha
Hapa ni kufanana tu kwa majina na wala Rugambwa si ukoo. Kardinali Laurean Rugambwa alikuwa ni kutoka ktk ukoo wa Basiita tamka Abasiita. Hapa ukimtafuta Askofu Novatus Rugambwa, Protase Rugambwa wote utaona wanatoka kwenye koo tofauti isipokuwa wamefananisha jina ambalo linatumiwa na kila mtu na wa ukoo tofauti. Hii ni tofauti na maeneo mengine ambayo ukisikia mfano Mwakalinga, Tarimo, n.k

Hata hivyo sidhani kama kanisa linasimama ktk misingi ya ukoo ktk utoaji wa vyeo na madaraja ya kikanisa.
 
No papa hawezi hamisha maaskofu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]ujue askofu ni cheo tuu cha kawaida.. Kardinali ndio papa anateua

Sent using Jamii Forums mobile app
Papa anawateua na anao uwezo wa kuwahamisha Maaskofu kwa kadri yeye na jopo lake watakavyoona inafaa. Kwa mfano
Askofu Mkuu Ruwaichi kahudumu Majimbo ya Mbulu, Dodoma, Mwanza na sasa Dar.
Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga kahudumu Majimbo ya Dodoma, Mpanda na sasa Mbeya.
Askofu Mkuu Paul Ruzoka alihudumu Kigoma na sasa anahudumu Tabora.
Askofu Mkuu Damian Dallu Kahudumu Majimbo ya Geita na sasa Songea na wengine wengi.
 
Hivi kumbe Askofu Rugambwa yupo! Mimi nimekua nikisikia jina tu nikidhani alishafariki zamani, kumbe mwamba alikuwa zake mambele.

Halafu Askofu Paul Ruzoka kahamia wapi?
Yupo mmoja akiitwa Rugambwa alikuwa Cardinal huyu alifariki miaka ya 90s.
 
Umeshaenda "kuibudu siku ya leo ya jumamosi?"

Nadhani ingekuwa amri yako leo huko ungeenda kudanganya wenzio kuhusu hili maana bila kushambulia Ukatoliki ktk mahubiri yenu huwa mnajiona kama hamjafanya ibada.
 
No papa hawezi hamisha maaskofu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]ujue askofu ni cheo tuu cha kawaida.. Kardinali ndio papa anateua

Sent using Jamii Forums mobile app
Papa ndiye mwenye mamlaka ya kuhamisha na kuteuwa Maaskofu while Maaskofu ndiyo wana uwezo wa kuhamisha Mapadre kutoka Parokia A kwenda parokia B zilizopo ktk majimbo wanayoyaongoza.
 
Kardinali Rugambwa alitoka jimbo katoliki la bukoba....miaka ya 1960 akiwa kardinali wa kwanza mweusi...

Unasemaje hapo?
 
Huyu jamaa,kavuma sana.Nimelisikia jina la Rugambwa miaka mingi,kumbe ndiyo huyu,mbona anaonekana ni badobado sana?
Anyway,hawa ndiyo majasusi wabobezi,wanaijua dunia nje ndani.
Usije changanya...kuna Rugambwa wengi...


Kuna Novatus, protace na Laurean...
Na wala sio ukoo mmoja...

Ni majina tu ya kihaya...

Novatus na Laurean ambaye alikuwa kardinali na amezikwa Bukoba wote ni wa jimbo la Bukoba...protace ni wa jimbo la kayanga kule karagwe...
 
Pamoja na uzoefu wake lakini nadhani hatoweza kuwa Kardinali kwa sababu ofisi ya Vatikan inaweza kuogopa kuonyesha hali ya upendeleo kwenye ukoo wa Rugambwa, kumbuka Kardinali wa kwanza Tanzania alikuwa ni kwenye ukoo huo, Laurean Rugambwa.
Hakuna ukoo wa Rugambwa acha hizo...

Mila za kihaya ni tofauti na makabila mengi nchi hii..jina la Mwisho sio jina la ukoo...

Laurean ni mtu wa Kamachumu huko Bukoba akiwa ni mhaya aina ya wahamba..
NOVATUS ni mtu wa ichwandimi ni muhaya wa kihanja...

Protace ni mtu wa karagwe ni muhaya wa karagwe aka Mnyambo...


So hawana undugu hata kidogo...
 
Hivi kila nchi inakuwaga na Kadinali wake? Au ni kwa ukanda yaani regions say EAC region, Kadinali moja?
 
Hilo niliona mapema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…