Je, Protase Rugambwa ndiye Kardinali ajaye Tanzania?

Niliwaza Ruwaichi.
Mfanyabiashara yule na ndiyo maana baada ya uchunguzi wa kina alioufanya baba Mtakatifu wa nani angestahili na kukosa mtu mwenye sifa stahiki, ndipo aliamua amrejeshe Protase ili aje awe.

Hujiulizi, kwa nini mambo yameenda kwa kasi ya kombora?!

Kumbuka pia, kwa nini uteuzi na kutangazwa Makadrinali ulichelewesha kutoka mwezi wa 4 uliopita?

Kuna tetesi pia, kwamba, baba Mtakatifu hakupendezwa na ubishi wa wazi wazi wa Ruwa alioufanya kwa Mamlaka iliyofariki.

Unamfahamu AG aliyepita wa Magufuli? Unafahamu mahusiano/ urafiki wake na huyo Protace?

Anyway, acha niishie hapa.
 
All in all jamaa aliona mbali but nimegundua hata Huku kwenye dini hizi teuzi zinahitaji connection even if watu walioshika dini watabisha
Hakuna connection kwa kanisa Katoliki, kila nafasi ina vigezo vyake. Mfano ni hii nafasi ya mshauri wa Baba Mtakatifu, anaangalia watu wenye exposure na uzoefu wa kitu anachohitaji.

Papa anafahamu kabisa akihitaji ushauri kuhusu kanisa la Tanzania basi ataupata bila shaka kwasababu Mwadhama Polycap Pengo yupo, lakini akihitaji ushauri wa kiutendaji katika masuala ya uendeshaji wa baadhi ya huduma za kipapa hasa kwenye nchi za maziwa makuu kutokea pale Vatican basi atahitaji mtu ambae amekua kwenye ofisi hiyo kwa miaka 10, ndipo linakuja wazo la kumpatia nafasi hiyo Mhashamu Protas Rugambwa.

Huenda alishapanga kumpa nafasi hiyo tangu siku alipomaliza muda wake kule Vatican, kwakua hakuweza kumbakisha basi akamleta Tabora ambapo atakua na majukumu kidogo kwasababu bado Askofu Mkuu Ruzoka yupo kwenye kiti, na huenda akaamua kumpatia Askofu msaidizi pale ambapo Mhashamu Ruzoka atakapostaafu.
 
Ina maana maaskofu wote nchi hii hakuna aliyefaa duh aisee
 
Dah!...upo vizuri sana kwenye utabiri
 
......
 
Unaumia ukiwa wapi? Wahaya Leo hatulali
 
Hongera Kadinali Protase Rugambwa, heri ya mafaniko ndani ya Kanisa Katoliki. Kanisa Katoliki liwe kiwanda cha kuzalisha imani, kujenga na kuimarisha maadili, tamaduni, mila na desturi za kanisa.
 
Na wewe mwanawane, kwani hujui kuwa Kadinali Pengo alitokea Sumbawanga ?

Je hujui Kadinali Rugambwa ambaye alikuwa Kadinali kabla ya Pengo alitokea Bukoba ?

Je, hujui hata Bwana Yesu alikuwa mtoto wa Seremala?

Mambo makubwa yanatokea sehemu dhaifu
 
Bwana Pendaelli, unajisikiaje leo na hii komenti yako?
 
What do you say now???
 
Huyu jamaa,kavuma sana.Nimelisikia jina la Rugambwa miaka mingi,kumbe ndiyo huyu,mbona anaonekana ni badobado sana?
Anyway,hawa ndiyo majasusi wabobezi,wanaijua dunia nje ndani.
Hiv hii kitu ya hawa watu kuwa majasus huwa kwel au ni uzushi zush tuu??.
Ofcz huwa ni wasomi sana na possibly wanaijua dunia .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…