Je! Rais Samia anapambana peke yake ndani ya CCM? Kitendo cha yeye kutoa hukumu kama M/kiti juu ya Gwajima, hakuashirii jambo hili?

Je! Rais Samia anapambana peke yake ndani ya CCM? Kitendo cha yeye kutoa hukumu kama M/kiti juu ya Gwajima, hakuashirii jambo hili?

mkulimamiwa

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2025
Posts
2,591
Reaction score
5,315
Kitendo cha Rais Samia kulibeba suala la Gwajima yeye kama yeye bila ya kuwa sehemu ya agenda kamili ya mkutano mkuu wa ccm wa juzi na na jana, kuna leta maswali mengi juu ya uungwaji mkono ndani ya chama chake

Kwa kiswahili kisicho sawa, hapa mwenyekiti alitumia kiti chake kumhukumu Gwajima pasina kuwa na uelewano wa pamoja kama Chama?

Rais wangu anao chawa wengi kiasi kwamba wengine ni viongozi na wenye ushawishi ndani ya CCM

Kitendo cha mpaka Chawa wa mama kutotiilia uzito jambo hilo na pengine kufikishwa meza kuu na kuwa miongoni mwa agenda mhimu katika kikao hicho, kunaleta maswali mengi sana

Uungwaji mkono ndani ya CCM, ni hafifu kiasi gani?

Watalaamu wa mambo ya siasa, jambo hili linaakisi kiasi gani cha ukweli?

Mungu bariki Tanzania

Mungu Bariki vyama vyote
 
"Tunataka kuona katika Taifa hili, vijana jeuri na wenye kujiamini, si vijana waoga, akina "ndiyo bwana mkubwa", vijana wanaohoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya kitanzania. Tunataka vijana waasi dhidi ya mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika Taifa"

Mwl J.K. Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania
 
Back
Top Bottom