Je, Rais Samia anayo haki na misingi ya kuongoza Tanzania Bara (Tanganyika) kwa mambo yasiyo ya Muungano?

Kwa hiyo hayo mambo yasiyo na muungano yako upande mmoja tu?

Soma Katiba my friend, mambo yasiyo ya muungano ni kwa pande zote mbili.

Iweje Mzanzibari aongoze Bara kwa mambo yasiyo ya Muungano?
Wewe uko nchi gani bwashee?

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Zanzibar?

Tuanzie hapo.
 
Mfumo huu wa muungano ni wa hovyo sana kuwahi tokea
Aidha tungekuwa Na serikali tatu lakini hii ingemfanya rais wa muungano kuwa powerless kabisa

Au tungefanya complete unification ( of which binafsi naona tukae mezani sasa kufanikisha hili tuvunje Zanzibar Na Tanganyika iwe only Tanzania tuwe Na united states of Tanzania ) yaani tungeua utaifa wa Zanzibar Na Tanganyika ikazaliwa nchi moja tu kusiwe Na mtanganyika ama mzanzibar yaani Zanzibar ingekuwa kama Dodoma ama Mwanza tu.

Ila haiingilii akilini rais mzanzibar aiongoze Tanzania bara kwa mambo ambayo hatukukubaliana ni ya muungano haimake sense kabisa. Sijui mzee wetu alikuwa anafikiria nini with this system yani its illogical in every way possible.
 
Kama mngrjikita kujibu hoja basi tungefika mbali sana. Je, nimeandika uongo? Au kuna sehemu nimekosea?
Magufuli kaingiaje hapa?

Hoja ni hii, ni sahihi kwa Mzanzibar kuongoza Bara kwa mambo yasiyo ya Muungano??
Tubaki hapa jamani
Ndio ni sahihi.Hakuna Tanganyika wala Tanzania Bara.Tanzania na Zanzibar ambayo ni semi autonomous.Kama Rais wa JMT anao wajibu kwa upande wa Bara na Visiwani.Regardless of Ametokea wapi.
 
Chombo Kipo ni Waziri Mkuu,Mamlaka yake ni ya BARA peke yake.Unataka Waziri Mkuu awe na madaraka sawa na ya Rais wa Zanzibar?
Sio kweli waziri Mkuu ni appointee wa rais haiwezekani mzanzibar awachagulie kiongozi watanzania bara haimake sense hata kidogo
 

Safi sana, nimekuelewa boss
 
Ndio ni sahihi.Hakuna Tanganyika wala Tanzania Bara.Tanzania na Zanzibar ambayo ni semi autonomous.Kama Rais wa JMT anao wajibu kwa upande wa Bara na Visiwani.Regardless of Ametokea wapi.

Hiyo regardless ametokea wapi ni logically correct au kwa kuwa inatambulika kikatiba tu?
 
Huo upupu umeshachokwa na watanganyika

Zanzibar isepe kama itatawaliwa na waomani ni kivyao
 
Na huu ndio ukweli wenyewe. Karume aliuhitaji zaidi muungano kuliko Nyerere ndio maana hata kwenye negotiation hakukuwa na mambo mengi.

Mfano: Ukitaka leo kuungana na Kenya, kwanza suala la nani atakuwa Rais tu linaweza kukwamisha muungano wenyewe.

Karume aliogopa kubaki mwenyewe, alijua atapinduliwa maana hakuwa na uwezo wa kujilinda na ishtoshe hata mapinduzi yenyewe hakushiriki kikamilifu. Yaliongozwa na Mjaluo John Okello.

Hizi juhudi za kuuuona uonevu na kutaka kujitawala, zimeanza baada ya mambo kupoa.
 
Na katika miaka nane ya utawala wa Karume kulikua na majaribio 11 yakutaka mumpindua.
 
Sultan alikimbilia Uingereza lakini nchi yake ya asili yaani Oman ilikua tayari kumpa msaada wa kijeshi arudi Zanzibar. Wazalendo waliomba msaada Bara na huu muungano kuzaliwa.
Kakuhadithia nani hili jambo?

Unajua kuwa Zanzibar na Oman walivunja undugu baada ya kifo cha Seyyid Said? Wapi na wapi Oman walitaka kumsaidia Jemshid? Kakaa miaka na miaka Uingereza hakurudi Oman ila majuzi tu halafu useme alitaka kumsaidia?

Tuseme tu, Karume alikuwa na khofu matokeo yake kajiingiza mtegoni maskini, nchi ndo imeenda kudidimia kwenye Muungano.
 
Tanganyika ilishauza haki yake ya uzaliwa wa kwanza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…