Je, Rais Samia anayo haki na misingi ya kuongoza Tanzania Bara (Tanganyika) kwa mambo yasiyo ya Muungano?

Ni sawa, ila mtoa hoja anachouliza ni kwa mantiki gani Mzanzibari aongoze mambo ya Tanganyika yasiyo ya Muungano wakati Mtanganyika (Hata alipokuwepo Magufuli) asiongoze mambo yasiyo ya Muungano Zanzibar? Mimi nona hapa dawa ni serikali 3 au moja, hizi mbili zina utata.
 
Hoja ni kwamba rais anapotoka Zanzibar kuwe na kiongozi mwingine mkuu anaesimamia Mambo ya bara yasio ya Muungano, Kama wanavyofanya wao Zanzibar
Labda ingefaa, lakini nayo inahitaji mabadiliko ya Katiba
 
Yaan mzanzibari aongoze bara kwa mambo hata yasiyo ya muungano ila Mbara asiingilie mambo yasiyo ya muungano Zanzibari! asee Nyerere alikosa hekima katika hili.
Kimsingi Nyerere aliweka mambo yote ya Tanganyika ndani ya serikali ya muungano ndiyo maana tanganyika mambo yote ni ya muungano na ndiyo maana hakuna serikali ya tanganyika hivyo tumsapoti mama aendelee kuongoza nchi.
 
Kimsingi Nyerere aliweka mambo yote ya Tanganyika ndani ya serikali ya muungano ndiyo maana tanganyika mambo yote ni ya muungano na ndiyo maana hakuna serikali ya tanganyika hivyo tumsapoti mama aendelee kuongoza nchi.
Unachoongea haki make sense hats kidogo.

Mambo ya muungano yapo 22, any thing out of hizo 22 haihusiani Na muungano!!

Rais wa muungano ( ambaye sio wa bara) ana pata wapi mandate ya kumanage mambo yasio katika muungano Tanzania bara.

Huu ni mtego hatari sana ( a ticking bomb) nalitakuja kulipuka siku ambayo rais wa jamhuri Na wa Zanzibar watatoka vyama tofauti


Na ndio maana ili kuepusha ili itabidi chama chenye nguvu kushinda muungano urais itabidi kitumie nguvu ya ubabe ama wizi kuiba kura Na Zanzibar kishinde hata kama hakipendwi ili kuepusha hili balaa.

Ndomana Mimi sipendi kuilamu CCM inachofanyaga Zanzibar najua it is a necessary evil maana wanajua mfano

Wangeruhusu siku maalim akachukua urais Zanzibar Na CUF ( au ACT ) nchi haiwezi tawalika aisee kutakuaa Na mkanganyiko mkubwa mno wa kimadaraka maana katiba Mpya ya Zanzibar nayo changamoto tupu
 
Nime quote vifungu vya katiba ku-support arguments zangu, nimeuliza kuna mahala nimeongea uongo?
Sijajibiwa zaidi ya matusi yako,

I quit arguing will stupid zero brain like you.
Acha usen&&ge! Hivyo vifungu ndiyo umevijua leo? Mtawala yoyote huwa anataka katiba inayomlinda akiwa madarakani. Dikteta Magufuri alijua wazi kwa katiba hii mbovu itampa mamlaka ya kufanya lolote na hakuna wa kumuuliza. Kumbuka Mwl. Nyerere aliwahi kusema kuwa kwa katiba hii akitokea mwendawazimu akawa Rais basi atakuwa Dikteta. Sasa alipoingia huyo mtu wako ikulu na kuambiwa arekebishe katiba unakumbuka alitoa jibu gani la kifedhuli?
 
You got it all wrong sina husda yeyote Na wazenji why should I?

Ninachosema huu mfumo unamapungufu mengi yanayofunikwa Na CCM kwakuwa inashika madaraka both sides.

Siku ikitokea JMT Na Zanzibar zina marais from different political parties tutaona mengi sana
 
Nakuuliza kwa nini huu mjadala unauleta leo wakati mama yupo madarakani? Wewe na wenzio wote wanafiki wakubwa akiwemo Humphrey polepole! Mna ndimi mbili kama nyoka. Acheni ujinga na kuleta chokochoko. Sisi wote ni waTz ujinga wenu pelekeni kwa wake zenu acheni mama atawale Nchi kwa raha na afanye lolote atakaloona linawapa faida Raia wake
 
Watanganyika ndio wanautaka wala sio wazanzibar
 
Watanganyika ndio wanautaka wala sio wazanzibar
Huu Muungano naona unawanufaisha tu CCM. Sidhani kama hiyo idadi ya Watanganyika ni kubwa kihivyo! Ni wale wachache tu wanao fanya kazi huko Zanzibar, wafanyabiashara na pia wale walio jenga undugu kwa kuoana/kuoleana!

Kinyume na hapo, hakuna.
 
Yaan mzanzibari aongoze bara kwa mambo hata yasiyo ya muungano ila Mbara asiingilie mambo yasiyo ya muungano Zanzibari! asee Nyerere alikosa hekima katika hili.
Hii shida yote hii wakumlaumu ni nyerere, muungano wenyewe umekata kimtego mtego tuu, nguvu zinatunika kuulinda,sisi watanganyika ndiyo tunaulazimisha sijui tunaumwa nini?
 
Niliweka andiko humu juu ya umuhimu wa TAMISEMI kuwa chini ya Waziri Mkuu ambaye ndio mtendaji wa bara.
 
Hayupo anayepinga uwepo wa Samia, yeye yupo kwa mujibu wa Katiba iliyopo, Ila madhaifu ya hii Katiba na aina ya muungano tulionao unaonekana zaidi kipindi hiki. Muungano mzuri wa serikali moja tuu na sio vinginevyo
 
Mkuu mambo ya Tanganyika yasiyo ya muungano yanasimamiwa na TAMISEMI ambapo hapo awali TAMISEMI ilikuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
 
Yaan mzanzibari aongoze bara kwa mambo hata yasiyo ya muungano ila Mbara asiingilie mambo yasiyo ya muungano Zanzibari! asee Nyerere alikosa hekima katika hili.
Mkuu, ktk vitu Vya kisheria, huwa vina tabu yake, Sheria unaweza itengeneza leo na ukaiona inakidhi matakwa ya hiyo, lkn kadri siku zibavyokwenda, sheria hiyo huwa inaenda inapitwa Wakati, na ndiyo maana kuna kipindi cha marekebisho ya sheria

Tafadhali, usimlaumu mtu, zungumzia hizo sheria, bado zinahitajika ama zimepitwa Wakati??
 
Tumeshachanganya sana damu ni vigumu kukwepa kuwa kitu kimoja.
 
Serikali moja ya majimbo mawili
Hayupo anayepinga uwepo wa Samia, yeye yupo kwa mujibu wa Katiba iliyopo, Ila madhaifu ya hii Katiba na aina ya muungano tulionao unaonekana zaidi kipindi hiki. Muungano mzuri wa serikali moja tuu na sio vinginevyo
 
Aisee hili la kupata Raisi anayetokea Zenji, halikuja bule, limekuja ili lituonyeshe jinsi katiba Yetu ilivyombovu na mapengo mengi yanayohusu muungano wetu

Ni Wakati muafaka sasa Katiba irekebishwe ama mambo yanayozungumzwa yakihusisha kero za muungano, na hili liongezwe kwenye kero la muungano
 
Ni vigezo gani vilitumika rais wa Tanganyika kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na rais wa Zanzibar kuwa Makamo. Kifo Cha Abed Aman Karume kiliacha maswali mengi ya Muungano yasiyokuwa na majibu.Kama angekuwepo mwaka 1977 katiba isingekuwa kama ilivyo sasa.Kwa maoni yangu yeye Karume hakutaka rais wa Muungano atoke Zenj.Lengo lake lilikuwa ni ulinzi wa serikari ya Mapinduzi Zanzibar.Ndio maana bado inaendelea kuwepo.Wewe utakuwa rais na mimi makamo.Mtazamo was hayati Karume na unapaswa kuwa endelevu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…