1. Rais ni Mtanzania.
2. Rais ni Kiongozi wa Serikali ya Muungano wa Tanzania.
3. Ana haki ya msingi ya kuongoza Tanzania yote, bara na visiwani.
Kinacho matter hapa si asili yake ni wapi, kama ulivyosema, Tanzania ni nchi moja, hivyo ukweli kwamba asili yake ni Zanzibar si muhimu.
Kinacho matter hapa, ni, je ana cheo gani na yupo katika serikali gani?
Mtu kama Waziri Kiongozi wa Zanzibar hastahili kuongoza mambo ya bara, si kwa sababu yeye ni Mzanzibari, bali kwa sababu ni mtumishi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, si serikali ya Muungano.Tumeona Dr. Omar Ali Juma alikuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar, halafu akaja kuongoza Tanzania nzima kama makamu wa rais.
Rais wa Tanzania ana haki ya kuongoza Tanzania bara na visiwani, kwani ni kiongozi wa Tanzania nzima.
Ila, Rais wa Jamhuri ya Muungano, hatakiwi kujiingiza kwenye mambo ya Zanzibar ambayo hayapo katika Muungano.
Zaidi, ukileta habari za Uzanzibari na Utanganyika katika nchi ambayo ni Muungano, hapo unaleta ukabila.
Una m define vipi nani Mtanganyika na nani Mzanzibari katika nchi ambayo kuna watu wengi wametoka bara kwenda kuishi visiwani na wametoka visiwani kuja kuishi bara?
Utam define kwa kuzaliwa? Kwa miaka ya kukaa sehemu? Au kwa vipi?
Wazanzibari wenyewe karibu wote ni mchanganyiko wa Wazaramo, Wamakonde, Wanyamwezi na kadhalika, sasa ukisema uwabague utarudi mpaka lini?
Huyo Ali Hassan Mwinyi kawa rais wa Zanzibar na Tanzania, na kazaliwa Kisarawe. Huyu ni mtu wa wapi?