Je, Rais Samia anayo haki na misingi ya kuongoza Tanzania Bara (Tanganyika) kwa mambo yasiyo ya Muungano?

Je, Rais Samia anayo haki na misingi ya kuongoza Tanzania Bara (Tanganyika) kwa mambo yasiyo ya Muungano?

Hii shida yote hii wakumlaumu ni nyerere, muungano wenyewe umekata kimtego mtego tuu, nguvu zinatunika kuulinda,sisi watanganyika ndiyo tunaulazimisha sijui tunaumwa nini?

Yes wa kumlaumu ni Nyerere, lakini hatuwezi kuendelea kumlaumu milele, inafika wakati tuchole mstari na tuseme sasa basi.
We need reforms zakutosha kwenye katiba juu ya muungano wetu
 
Hayupo anayepinga uwepo wa Samia, yeye yupo kwa mujibu wa Katiba iliyopo, Ila madhaifu ya hii Katiba na aina ya muungano tulionao unaonekana zaidi kipindi hiki. Muungano mzuri wa serikali moja tuu na sio vinginevyo

Welldone aisee, umeongea mawazo yangu
 
Mtoa mada ana hoja za msingi sana, ingawa kuzitoa muda huu inaonekana kama hapendi kuwe na rais kutoka visiwani, ila hii hoja hata kama ingetolewa kipindi cha hayati bado ina mantiki.

Sina ugomvi wowote wa Mama kuwa Rais wa Taifa letu, lakini kwa kipindi chake mapungufu mengi sana juu ya Muungano yanaonekana wazi wazi,

Sio sawa kukimbia hoja hii kwa sababu tu tuna Rais Mzanzibari kwa sasa, ni busara kujadili na ikiwezekana kushawishi mabadiriko yatakayo ondoa mkanganyiko huu.
 
Aisee hili la kupata Raisi anayetokea Zenji, halikuja bule, limekuja ili lituonyeshe jinsi katiba Yetu ilivyombovu na mapengo mengi yanayohusu muungano wetu

Ni Wakati muafaka sasa Katiba irekebishwe ama mambo yanayozungumzwa yakihusisha kero za muungano, na hili liongezwe kwenye kero la muungano

Nadhani wakati wa kurekebisha katiba yetu ni sasa, tusisubiri mpaka tugombane na kufukuzana,
Ni dhahiri kwamba, Mzanzibari kuongoza Bara kwa mambo yasiyo ya muungano inaleta utata, kwani hatukuungana kwa kila kitu.

Na katiba ya sasa inaeleza wazi juu ya mambo 22 ya muungano, nilitegemea Rais wa muungano kama anatoka Zanzibar ahusike na mambo ya muungano exclusive, na katiba iseme mambo yasiyo ya muungano yawe chini ya???? Makamu wa Rais, PM, etc
 
Si mambo ya kuhitaji kuumiza kichwa chako haya, miaka yote tumeimba, tumetisha, tumesingizia watu kuwa WANAHATARISHA MUUNGANO,
kwamba MUUNGANO ULINDWE KWA GHARAMA ZOZOTE.
Acha mambo yaende hivyo hivyo; ndiyo gharama yenyewe

Usinipangie cha kufanya, hii nchi ni yetu sote.
Kwani ni nani aliitisha referendum kuhusu muungano wetu kupata popular puplic opinion? Yupo?

Tanzania ya 1961 sio ya sasa, wengine hatukuwepo, tuna haja ya kuhoji
 
Rais Mh Mama Samia hajaanza kuongoza Tanzania leo. Amekuwa kiongozi mkubwa namba mbili Tanzania takriban miaka sita sasa.
Hapakuwa na swali wala figusi kipindi chote hicho.
Amepanda kuwa namba moja sasa maneno yamekuwa mengi mnoo..
Kipindi chote cha nyuma mlikuwa wapi? Au kwa vile haja toka kanda iliyo haribu tasnia na utu wa Watanzania?
Kwa taarifa tuu, Mama Samia ni Rais HALALI wa Tanzania. Kama mlitegemea genge la Wasukuma poleni sana.
Miaka mitano ilikuwa kama tuko jehanam.
Sasa mama kaja kutupa tabasamu mmeanza na uchokonozi.
Tulieni Mama Samia atupeleke Kaanan nchi ya maziwa na asali.
Mungu wanMbinguni amkinge Mh. Samia na macho ya husda.
 
Kwa kuwa Rais aliyeko madarakani ni asili ya Zanzibar, hivyo ni mZanzibari, na anaongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na yeye ni zao la muungano wetu. Na, kwa kuwa Katiba yetu imebainisha dhahiri mambo ya muungano, Je? Ni sahihi kwa Rais wa sasa kuongoza Tanzania Bara (Tanganyika) hata kwa mambo yasiyo ya muungano?
Swala la urais ni la Muungano, kwa hiyo lina-override eceptions zingine zote ndani ya JMT
 
Kama mngrjikita kujibu hoja basi tungefika mbali sana. Je, nimeandika uongo? Au kuna sehemu nimekosea?
Magufuli kaingiaje hapa?

Hoja ni hii, ni sahihi kwa Mzanzibar kuongoza Bara kwa mambo yasiyo ya Muungano??
Tubaki hapa jamani
Hawa vijana akili zao ni ndogo Sana wanachojaribu kufanya ni kuahirisha kujadili tatizo na sio kuliondoa tatizo kwa kuleta Mambo nje ya mada
 
Kwa kuwa Rais aliyeko madarakani ni asili ya Zanzibar, hivyo ni mZanzibari, na anaongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na yeye ni zao la muungano wetu. Na, kwa kuwa Katiba yetu imebainisha dhahiri mambo ya muungano, Je? Ni sahihi kwa Rais wa sasa kuongoza Tanzania Bara (Tanganyika) hata kwa mambo yasiyo ya muungano?

1.Kama ni sahihi, anaongozaje mambo yasiyo ya muungano ilhali yeye ni mZanzibari na ni zao la muungano na ana uishi muungano pamoja na mambo ya muungano, tukumbuke kwamba , tumeungana lakini hatujaungana katika mambo yoye, tumechagua mambo ya kuungana.
2.Kama sio sahihi nini kifanyike?
Je, anakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu yeye ni Mzanzibari au kwa sababu yeye ni Mtanzania?

Anyway, tusichoshane kwa maswali... hapa sio bungeni!

Kwanza, tuweke pembeni suala la kuwa rais kwa sababu alikuwa makamu wa rais! Umakamu wake wa rais ulitokana na Uzanzibari wake!

Lakini hapa tunaujadili urais, ambao mtu haupati kwa Uzanzibari wake bali kwa Utanzania wake! Na tunaposema Utanzania, tunazungumzia jamhuri ya muungano!

Sasa kwavile umeshasema mambo yasiyo ya muungano kwa Tanzania Bara yanashughulikiwa na serikali ya muungano; serikali hiyo ya muungano rais wake ndo huyo Samia, ambae, kimsingi urais wake hautokani na Uzanzibari wake bali na Utanzania wake!!!

Na kwavile urais wake unatokana na Utanzania wake, hakuna shaka kwamba, ana haki na mamlaka ya kusimamia yale yote yanayopaswa kusimamiwa au kushughulikiwa na serikali ya muungano!!
 
1. Rais ni Mtanzania.
2. Rais ni Kiongozi wa Serikali ya Muungano wa Tanzania.
3. Ana haki ya msingi ya kuongoza Tanzania yote, bara na visiwani.

Kinacho matter hapa si asili yake ni wapi, kama ulivyosema, Tanzania ni nchi moja, hivyo ukweli kwamba asili yake ni Zanzibar si muhimu.

Kinacho matter hapa, ni, je ana cheo gani na yupo katika serikali gani?

Mtu kama Waziri Kiongozi wa Zanzibar hastahili kuongoza mambo ya bara, si kwa sababu yeye ni Mzanzibari, bali kwa sababu ni mtumishi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, si serikali ya Muungano.Tumeona Dr. Omar Ali Juma alikuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar, halafu akaja kuongoza Tanzania nzima kama makamu wa rais.

Rais wa Tanzania ana haki ya kuongoza Tanzania bara na visiwani, kwani ni kiongozi wa Tanzania nzima.

Ila, Rais wa Jamhuri ya Muungano, hatakiwi kujiingiza kwenye mambo ya Zanzibar ambayo hayapo katika Muungano.

Zaidi, ukileta habari za Uzanzibari na Utanganyika katika nchi ambayo ni Muungano, hapo unaleta ukabila.

Una m define vipi nani Mtanganyika na nani Mzanzibari katika nchi ambayo kuna watu wengi wametoka bara kwenda kuishi visiwani na wametoka visiwani kuja kuishi bara?

Utam define kwa kuzaliwa? Kwa miaka ya kukaa sehemu? Au kwa vipi?

Wazanzibari wenyewe karibu wote ni mchanganyiko wa Wazaramo, Wamakonde, Wanyamwezi na kadhalika, sasa ukisema uwabague utarudi mpaka lini?

Huyo Ali Hassan Mwinyi kawa rais wa Zanzibar na Tanzania, na kazaliwa Kisarawe. Huyu ni mtu wa wapi?

Naona unatetea uZanzibari na Utanganyika tu, sioni mantiki katika hoja yako. Hujajibu hoja iliyoko mezani!!!!!

Ni kwamba, Mama ni Rais wa muungani hatujabisha, lakini katika muungano kuna mambo baadhi ya muungano(22) na nilitegemea ange base kwenye hayo 22 kwa upande wa Zanzibar, lakini anatoa wapi authority ya kudeal na mambo yasiyo ya muungano, ilhali yeye ni zao la muungano, na anaamini katika mambo ya muungano, hapo sijui
 
Naona unatetea uZanzibari na Utanganyika tu, sioni mantiki katika hoja yako. Hujajibu hoja iliyoko mezani!!!!!

Ni kwamba, Mama ni Rais wa muungani hatujabisha, lakini katika muungano kuna mambo baadhi ya muungano(22) na nilitegemea ange base kwenye hayo 22 kwa upande wa Zanzibar, lakini anatoa wapi authority ya kudeal na mambo yasiyo ya muungano, ilhali yeye ni zao la muungano, na anaamini katika mambo ya muungano, hapo sijui
Yeye kuwa zao la muungano haimpotezei uhuru wake wa asili wa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano.

Alipokuwa makamu wa rais hakuwa na huo uhuru wa kushughulika na masuala yote kwa ujumla wake?.
 
Bwashee Zanzibar ni nchi kamili

Hakuna nchi inaitwa Tanzania bara duniani kote

Nchi inayojulikana ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mzanzibar anaweza kufanya kazi popote katika JMT

Wewe siyo mzanzibari hivyo huwezi kufanya kazi kule wala kupewa ardhi, ni sawa tu na umeenda Kenya au Uganda!

Hakuna nchi inayojulikana Zanzibar duniani kote, nenda UN, AU, EAC, SADC etc hakuna bendera ya Zanzibar inayopepea huko.

Kwa hiyo kusema Tanzania Bara (Tanganyika) sio nchi na haijulikani popote ila Zanzibar ni nchi nadhani ni uwendawazimu tu, kwa sababu hivi vitu havina tofauti
 
Mfumo huu wa muungano ni wa hovyo sana kuwahi tokea
Aidha tungekuwa Na serikali tatu lakini hii ingemfanya rais wa muungano kuwa powerless kabisa

Au tungefanya complete unification ( of which binafsi naona tukae mezani sasa kufanikisha hili tuvunje Zanzibar Na Tanganyika iwe only Tanzania tuwe Na united states of Tanzania ) yaani tungeua utaifa wa Zanzibar Na Tanganyika ikazaliwa nchi moja tu kusiwe Na mtanganyika ama mzanzibar yaani Zanzibar ingekuwa kama Dodoma ama Mwanza tu.

Ila haiingilii akilini rais mzanzibar aiongoze Tanzania bara kwa mambo ambayo hatukukubaliana ni ya muungano haimake sense kabisa. Sijui mzee wetu alikuwa anafikiria nini with this system yani its illogical in every way possible.
 
Watu wanongea ongea tu Mara tumpe support,haya mambo CCM inayachukulia kilaini lakini tu kila Mtawala anaogopa ku ya solve lakini haya isipokuwa kizazi chetu hiki kuna siku CCM itakuja kuanguka na kutatokea vyama tofauti katika hizo Nchi ndipo kimbembe kitanzia hapo.

Exactly, na kama tuko makini yunaweza kuepusha kufika huko
 
Kwani Mzanzibari si Mtanzania? Mbona Mwinyi na Jumbe waliongoza Zanzíbar ilhali si Wazanzibari?
Je katiba inasemaje kuhusu Zanzíbar kutoa raisi au inasema MTANZANIA tu ?

Acha uongo, rudi kwenye hoja mezani
 
G55 ya nini kwa sasa. Lets give time kwa mama atulie kwenye kiti kisha haya Muungano tutayazungumza baadaye na yeye kuyafanyia kazi kwa mujibu wa Katiba na atakavyoona inafaa. Kwa sasa yupo kwenye nafasi hiyo kwa mujibu wa katiba iliyopo. Fullstop.

When is baadaye? Afanyie kazi asifanyie kazi, the bottom line ni kujadili haya mapungufu ya katiba na kuyatatua sasa
 
N



Pia kwenye bunge letu kuna wabunge wanaochaguliwa toka Zanzibar kama wabunge wa Bunge la muungano, lakini wanakaa katika bunge hilo hata kwa mambo yasiyo ya muungano. Kuna mbunge mmoja aliwahi kusema wazi hilo bungeni. Nani anawalipa posho zao ni serikali ya Tanganyika (Tanzania). Huko Zanzibar wana tayari wawakilishi wao, sijui kuna maeneo wana wabunge wawili sijui. Na pia wanapata pesa za ubunge za jimbo, inalipa Tanganyika. Jamani huu muundo si sawa kabisa. Hakuna anayekataa muungano, tunachoakataa ni muundo ufanyiwe marekebisho. Ili muungano uwe muungano ni muhimu kutofautisha kati ya Tanganyika na Tanzania, ili rais atawale Tanzania na katiba ya Tanzania na awepo kiongozi wa Tangayika na katiba ya Tanganyika. Kama ilivyo Zanzibar wana katiba yao, bendera yao na Rais wao.
Nafikiri pendekezo la katiba ya Warioba ingefaa liwekwe tena, kwa sababu jambo hili haitakwisha kulalamikiwa.
Makamu wa Rais amesema hatavumilia ye yote anayevuruga muungano. Ukweli ni kwamba hakuna anayekataa muungano kinachopingwa ni mfumo au muundo wa Muungano. Mbona nchi nyingi zina muungano wa kila nchi zilizouungana inajulikana kwa kuwa na uongozi wake.
Kitu kimoja nilichowahi kukusikia wanasiasa wanajisifu kuwa Muungano wetu ni wa kipekee duniani. Kwahiyo lazima tuudumishe. Sielewe tuudumishe kwa maslahi ya nani. Tumekaa miaka yote hii, ila naona kuna mabavu yanatumika kulinda muungano huu. Watu wanafukuzwa kila mmoja anapouliza juu ya jambo hili. Na sisi Watanganyika ni waoga mno hatuna ujasiri wa kudai nafasi ya Tangayika katika muungano huu.
Kama Zanzibar ni nchi iliyoungana na Tanganyika kwanini isitoe cho chote kwenye Muungano kwa uwiano wa ukubwa wake. Ukweli tumekamatwa na tunaendelea kuchezewa huu mchezo na siasa za nchi hii.
Mungu asaidie uongozi wa Chama tawala hivi wana masilahi gani katika mfumo huu ambao umeweza kupingwa miaka na miaka. Lakini wenye mabavu wachache wameshikilia usukani.

Asante sana mkuu, nimeheshimu sana mawazo yako.
Thank you
 
Back
Top Bottom