Je, Rais Samia atakumbukwa maisha kwa ushindi wa 55% au atasahaulika kwa ushindi wa 80% mwaka 2025?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Hilo ndilo swali la msingi

1. Je Raisi anataka kukumbukwa maisha kwa kujenga mifumo na kutupa katiba bora Tanzania
2. Atasahaulika kwa kuiba kura na kugushi uchaguzi na kujipa 80% ya ushindi ambayo ni fake?

Haya ni maamuzi yake. Mafisadi wote wanataka achague namba 2 kwani wanajali matumbo tu

Sawa kwenye namba moja ni lazima wapinzani kwa hali halisi watapata 45% na wabunge wengi lakini hawatakuwa majority. Lakini kuna wabunge wengi watakosa viti kwenye uchaguzi huru na wa haki. Lakini ndiyo nchi ilipo. Hili sio taifa la chama kimoja!

Kwa namba 2 ni kama 2020

Mama ngoma iko kwako. Lakini nakushauri uende na namba 1 kwani wapinzani wameshikiliwa na Mbowe tu. Mbowe akikata tamaa hii nchi itakuwa hatarini huo ndiyo ukweli

Watanzania wengi wanafikiri mwenye sikio la Raisi Samia ni Kikwete hili sio la kweli. Mwana siasa wa kumwangalia sana Tanzania kwa sasa ni Kinana. Kinana na Mbowe ndiyo wanasiasa ambao wataamua mwelekeo wa nchi yetu kwa miaka mingi ijayo. Ndiyo maana niliuliza kuhusu Kinana na Uzalendo wake. Je kinana wa sasa ambaye ni mzee anataka kukumbukwa kwa lipi yule Mzalendo wa 1980’s au fisadi na majigambo ya 1990’s . Tuombe Kinana wa sasa arudi kuwa wa 1980’s. Kwa connection ya Arusha Raisi Samia kamchagua Kinana kwasababu ana waelewa Chadema kuliko yeye na hata kikwete. Hawa wa pwani anawajuwa sana wasiwasi ni hawa wafanyabiashara kama Mbowe ambao ni wagumu sana kuwasoma ndiyo maana Raisi kamleta kinana. Tuombee mikutano yao ya vyama iwe na tija kwa taifa
 

Mtu mjinga tu na mwenye maslahi na utawala wa CCM, ndio atasimama kwenye mstari wa kura kushiriki maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Kwa hii katiba ambayo rais anapanga matokeo, ni aibu mtu mwenye akili timamu kujipanga kwenye mstari wa kura. Machafuko au mapinduzi ndio yatarejesha heshima ya box la kura.
 
Umeanza
Unapata nini kwa upuuzi huu unaandika kila siku…?
Unajua ni kiasi gani unaumiza mioyo ya waliodhulumiwa haki zao baada ya mwendazake….
Hii nchi ni yetu sote hubirini upendo Kati yetu kila mmoja kwa Imani yake sio kuja humu na maandiko ya kejeli dharau tu kwa ajili ya matumbo yenu
Tuwe Wakweli
Haki ipi nakuuliza ubayoisifia wewe?
Mlishaelekezwa hii title ya Dr muitumie inavyostahili sio kujikweza tu
Punguza ukora bro…. Unakera kwa ufupi
Usomi wenu isiwe fimbo ya kuwachapa wananchi
 
Tanzania tuko watu milioni 60 hivyo eligible voters ni million 45. CCM wako milioni 5 na wakiiba kura ni milioni 5 nyingine jumla kura milioni 10!. Watu milioni 35 wakihamasishwa wakajiandikisha na kupiga kura, hata CCM, NEC, serikali yote, polisi wote, jeshi lote, hata waibe vipi hawewezi kuiba kura milioni 35!. Hivyo nyie msiopiga kura ndio majinga ya mwisho yanayoipa CCM ushindi wa mezani kwa kuweka mpira kwapani.

P
 
Nimeanza nini?
Unapata nini kwa upuuzi huu unaandika kila siku…?
Yaani kila ninachoandika ni upuuzi?.
Unajua ni kiasi gani unaumiza mioyo ya waliodhulumiwa haki zao baada ya mwendazake….
Kuna watu wowote wamedhulumiwa haki zao baada ya Blaza wangu kutangulia?. Ni kina nani?. Kila ukiumiza watu mioyo karma itakushughulikia, unaweza kunielimisha kiwango changu cha ni kiasi gani nimeumiza watu mioyo?.
Hii nchi ni yetu sote hubirini upendo Kati yetu kila mmoja kwa Imani yake
Karibu pande hizi 2017: Watanzania (CCM, Upinzani) tu Wamoja, Tupendane, Tuheshimiane, Tushirikiane kuijenga nchi yetu
Humu nimesema
Pia nimeshauri... https://www.jamiiforums.com/threads/angalizo-kwa-wana-jf-tuwaepuke-prophets-of-the-doom-
sio kuja humu na maandiko ya kejeli dharau tu kwa ajili ya matumbo yenu
Tuwe Wakweli
Haki ipi nakuuliza ubayoisifia wewe?
Pata muda kuona hizi haki
1. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
2. Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
3. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
4. Asante sana Rais Samia kwa kuliponya Taifa. Umeonesha kwa kauli na matendo; tunajenga nyumba moja, hakuna sababu ya kugombea fito!
5. Ushauri kwa DPP: Kutekeleza nia njema ya Rais Samia, kuona Haki ikitendeka; je, tumchagize DPP kutumia Nolle kufuta kesi zote zinazosuasua?
Mlishaelekezwa hii title ya Dr muitumie inavyostahili sio kujikweza tu
Punguza ukora bro…. Unakera kwa ufupi
Usomi wenu isiwe fimbo ya kuwachapa wananchi
Duh...!. Yamekuwa haya?!. Kwa vile JK alipewa causa na akaitwa Dr, Mzee Mengi pia vivyo hivyo, hamkusema, then why not Dr. Samia?. Hili nimeshauri Baada ya kutunukiwa PhD na kuwa Dkt. mnaonaje jina la "Mama" sasa tukaachana nalo ila Nyumbani wanaweza kuendelea kumuita Mama?
P
 

Narudia tena, kwa mwanaume anayesimamisha vizuri kwenda kusimama kwenye mstari wa kura ni upuuzi kama upuuzi mwingine. Kwa macho yangu niliona wanaojita usalama wa taifa wakilazimisha kusainiwa kwa matokeo fake ya uchaguzi. Sasa sijui unazungumza nini.

Hakuna uwezekano wa wapiga kura kufika hata milioni tano kwa ule upuuzi uliofanyika 2020. Hakuna watu wajinga wa hivyo. Machafuko au mapinduzi ndio njia pekee za kurejesha heshima ya box la kura.
 

Mchana ulileta bandiko kuhusu kuwa na vyuo vingi, ila ujinga bado uko. Nikachangia kwenye bandiko lako kuwa wasomi ndio wajinga zaidi kuliko wasiosoma. Hapa nakudhihirisha kuwa wasomi ndio wajinga zaidi, ww ukiwa mfano halisi.

Hakuna nchi yoyote hasa hizi za waafrika wananchi wanaozidi miaka 18, kuwazidi walio chini ya idadi hiyo. Sheria za nchi yetu zinasema wenye miaka 18+ ndio wenye haki ya kupiga kura. Sensa ya juzi ambayo ni idadi rasmi, tuko 61m. Inawezekana vipi watu 45m kuwa eligible kupiga kura kutoka watu 61m? Hata juzi Magufuli uchaguzi wa 2020 aliposema wapiga waliojiandikisha wako 29m+ tulisema ni uongo wa wazi, na lengo ni kupora uchaguzi kwa matokeo ya kupika. Na kweli uchaguzi ule ambao wapiga kura hawakufika hata kukaribia 10m, yeye alitangazwa kupata kura 12m+! Hiki ni kipimo halisi cha wasomi wajinga, ww ukiwa mmoja wapo.
 
Hatogombea
 
Tatizo kubwa ni watu kujifanya hawawajui maofisa wa ofisi za uma wanaofanya uhalifu halafu wanategemea lawama ziende kwa Rais. Kila mtumishi wa uma anatakiwa atimize wajibu wake kwa kuzingatia katiba na Sheria.
Mtumishi wa uma hatakiwi kuonesha upendeleleo wa wazi kwa chama fulani (ni kosa la jinai na kinyume Cha katiba). Hii inahusisha tume ya uchaguzi, majeshi yote ikiwemo polisi , mahakama na wengine wote wanaoajiriwa wakati wa uchaguzi.
Kwa sababu ya ujinga (ambayo ndiyo asilimia kubwa) na vishawishi vingine vikiwemo pesa na ahadi za vyeo, watumishi wengi wamefanya uhalifu ambao wanastahili kuadhibiwa kwa ajili hiyo.
Kuondoa hili tatizo, njia rahisi ni kuwatambua wahalifu hao, kuwataja na makosa yao (siyo rahisi kushtakiwa kwa sababu waandaa mashitaka na serikali ni sehemu yao), lakini kumbukumbu zitabaki na pia wataogopa na wale wajinga wataelewa.
Jambo muhimu kuliko yote ni kujenga taifa la watu wenye akili nzuri, wanaoheshimiana katika hali ya ustaarabu, na hili litafanikishwa zaidi na watumishi wa uma na siyo wanasiasa.
Ikumbukwe kwamba CCM bado ndicho chama kilichojijenga zaidi kwa sababu za kihistoria na hivyo kutafuta ushindi wa wizi wa mchana kweupe ni ujinga na aibu ambayo inatakiwa iepukwe.
CCM inatakiwa iongoze kwa mfano wa kuheshimika.
Hata ushindi wa 51% ni ushindi tu.
 
CCM iliwahi kushinda uchaguzi upi wa urais tangu vyama vingi? Zanzibar ni good example.

Sanduku la kura lini lilitenda HAKI bila msuguano!!!!
 
P, tutegemee namba 2.

Nilikuwa nafikiria juzi nitaanza kukuita Bro ! We have alot in common kuanzia Ilboru, Magu etc.

Ukiwa Ilboru ulikuwa mbele ya Lissu au nyuma yake? Au walati mmoja.
Kumbe nyie ndio mlikuwa watabe.
Sasa kuna hizi product za siku hizi za Tbr boys na wapi sijui khaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…