Je, Rais Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Awamu ya Tano au ya Sita kwa mujibu wa Katiba ya nchi?

Je, Rais Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Awamu ya Tano au ya Sita kwa mujibu wa Katiba ya nchi?

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
11,662
Reaction score
6,888
Leo asubuhi nememsikia mtangazaji mmoja wa East Africa Radio (kwenye kipindi cha 12:00- 04:00) akisema Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni Rais wa awamu ya sita. Yawezekana wengi wakawa na mtazamo huo, au wengi wakafuata mtazamo huo baada ya kumsikia mtangazaji huyo. Je, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, toleo la 20 Juni 2005, Rais wa sasa anamalizia awamu ya tano au anaanza awamu nyingine, yaani ya sita?

Je, awamu ya tano (phase 5) imekuwa na Marais wawili? Mmoja ameshika kipindi cha kwanza (1st term) na mwingine karibu kipindi cha pili (2nd term) kwa sababu yule wa kwanza amefariki dunia?

Ikumbukwe kuwa awamu moja ina vipindi viwili (one phase has two terms).

Je, mwanahabari huyo aliptitia katiba ya nchi kabla ya kuongelea facts?

Je, ibara ya 40 (4), inatoa jibu sahihi la swali juu ya kuanza kwa awamu ya sita au la, ni kuwa Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan amefungua awamu ya sita?

Rejea ibara ya 37, kifungu cha 5.
 
Mzee hukukisoma vizuri hicho kipengele ulichokinukuu. Hakuna mahali kwenye kipengele hicho panapotaja neno awamu. Habari za awamu zilikuja tu toka kwa wanasiasa kwa sababu ya utashi wao tu. Hivyo awamu hii ingeweza kuwa awamu ya tano au ya sita kulingana na anavyoamua mwenye sauti kubwa.

Hili jambo umeliweka kama vile raisi anayeingia madarakani ni lazima awe na vipindi 2. Nafikiria ingeitwa awamu ya ngapi kama kwa bahati mbaya fulani hivi marehemu angeangushwa katika uchaguzi. Ungeendelea kuuita utawala mpya awamu ya tano sababu tu miaka 10 haijakamilika
 
Nami kama nimewasikia, ila wamesema raisi wa sita. Nasi awamu ya sita.
 
Mzee hukukisoma vizuri hicho kipengele ulichokinukuu. Hakuna mahali kwenye kipengele hicho panapotaja neno awamu. Habari za awamu zilikuja tu toka kwa wanasiasa kwa sababu ya utashi wao tu. Hivyo awamu hii ingeweza kuwa awamu ya tano au ya sita kulingana na anavyoamua mwenye sauti kubwa.
Hili jambo umeliweka kama vile raisi anayeingia madarakani ni lazima awe na vipindi 2. Nafikiria ingeitwa awamu ya ngapi kama kwa bahati mbaya fulani hivi marehemu angeangushwa katika uchaguzi. Ungeendelea kuuita utawala mpya awamu ya tano sababu tu miaka 10 haijakamilika
Umenifilisi, yaani kama angeshinda Lisu..angeitwa Rais wa awamu ya ngapi?
 
Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Sita na moja kwa moja anakuwa Rais wa awamu ya 6. Awamu zinahesabiwa kutokana na mabadiliko ya Rais, sio vipindi vya U Rais. Mwalimu Nyerere alikuwa Rais wa awamu ya kwanza lkn yeye alikaa madarakani kwa zaidi ya miaka 20... Waliofuata walikaa madarakani kwa vipindi vya miaka 10, kasoro Hayati Dr. John Joseph Pombe Magufuli ambaye yeye awamu yake amehudumu kwa miaka mitano na miezi michache. Huyo Mtangazaji yupo sahihi.
 
Tunataja awamu kwa kulingana na Awamu za Rais. JPM alikuwa Rais wa Awamu ya Tano kwasababu ni Rais wa Tano
Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu ni Rais wa Awamu ya Sita kwasababu ni Rais wa Sita Tangia ncui yetu ipate uhuru .

Katiba haihusiki hapo bali ni utashi tu
 
Nyerere alikuwa Rais wa awamu ya ngapi na ngapi maana alitawala miaka 20+
 
Mzee hukukisoma vizuri hicho kipengele ulichokinukuu. Hakuna mahali kwenye kipengele hicho panapotaja neno awamu. Habari za awamu zilikuja tu toka kwa wanasiasa kwa sababu ya utashi wao tu. Hivyo awamu hii ingeweza kuwa awamu ya tano au ya sita kulingana na anavyoamua mwenye sauti kubwa.
Hili jambo umeliweka kama vile raisi anayeingia madarakani ni lazima awe na vipindi 2. Nafikiria ingeitwa awamu ya ngapi kama kwa bahati mbaya fulani hivi marehemu angeangushwa katika uchaguzi. Ungeendelea kuuita utawala mpya awamu ya tano sababu tu miaka 10 haijakamilika
Ila pia kwa common sense, serikali inaundwa na baraza la mawaziri pia. Baraza la mawaziri ni lile lile. Halijavunjwa na kuwekwa jipya...
 
Ni Rais wa awamu ya kwanza ya mpito/interim president. First interim president in Tanzania! Ni wazo tu, hilo mnalionaje?
 
Kwani huko Zanzibar Rais Mwinyi ni Rais wa awamu ya ngapi? Awamu zinaendana na Rais, hivyo awamu moja haiwezi kuwa na Marais wawili kwani kila Rais ana utaratibu wake wa kuongoza.
Alipokufa Dr Omar Juma, aliyekuwa makamu wa awamu ya tatu, je yule Dr. Shein aliyemfuata alikuwa ni makamu wa wamu ya nne?
 
Alipokufa Dr Omar Juma, aliyekuwa makamu wa awamu ya tatu, je yule Dr. Shein aliyemfuata alikuwa ni makamu wa wamu ya nne?
awamu inaisabiwa kwa ukaaji madarakan kwa Rais mfano mzee Mwinyi Zenj ametawala miaka.mingapi na anahesabika
 
Back
Top Bottom