Mzee hukukisoma vizuri hicho kipengele ulichokinukuu. Hakuna mahali kwenye kipengele hicho panapotaja neno awamu. Habari za awamu zilikuja tu toka kwa wanasiasa kwa sababu ya utashi wao tu. Hivyo awamu hii ingeweza kuwa awamu ya tano au ya sita kulingana na anavyoamua mwenye sauti kubwa.
Hili jambo umeliweka kama vile raisi anayeingia madarakani ni lazima awe na vipindi 2. Nafikiria ingeitwa awamu ya ngapi kama kwa bahati mbaya fulani hivi marehemu angeangushwa katika uchaguzi. Ungeendelea kuuita utawala mpya awamu ya tano sababu tu miaka 10 haijakamilika