auferet dominus
JF-Expert Member
- Jul 18, 2017
- 1,804
- 1,292
Kwa namna yoyote mama SSH ni rais halali kabisa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa katiba ya JMT mwenye madaraka ya kutekeleza shughuli za wadhifa wake bila kulazimika kunukuu chochote kutoka kwa mtangulizi wake. Anaweza kunukuu ya mtangulizi wake pale tu atakapoona vyema hivyo. Hivyo sio sahihi hata kidogo kunasibisha chochote anachotakiwa kufanya na vya mtangulizi wake. Narudia tena halazimiki kurefer chochote toka kwa mtangulizi wake.