Je, Serikali inazungumziaje suala la wanafunzi kukaa na njaa shuleni hadi usiku?

Kwahiyo serikali ina uwezo wa kulisha hao watu wote? Kama mtu hawezi kununuliwa mwanae madaftari wewe unategemea ataweza kumnunulia chakula kweli kila siku?

Wewe Kama msomi usitoe mitazamo ambayo haipo kwa kulinganisha , Mtu na ntu , unabidi kusoma between the lines ili uelewe what I mean, lengo ni kuandaa mfumo ili mzazi kupitia hand to mouth yake ya kila siku Basi aweze kuchangia elfu nne kwa mwezi na miambili kwa siku na Serikali iweke support Yake ,na mtoto Apate chakula


Watz Msiwe wabinafsi
 
Mkuu mahitaji ni mengi hata kuliko hicho chakula kuna wanafunzi wanatembea kilomita 5km kuenda na 5km wazazi amekosa nauli ya 400, wengine hawana madaftari ya sh 500, wengine sare zimechaka sasa mkuu serikali ianze na lipi hasa katika hayo?
 
Njaa haikubaliki. Nilisoma shule ya aina hio bahati nzuri shule ilikua karibu na nyumbani. Ilikua ikigonga kengere ya mapumziko saa 4, mbio hom kuwahi kiporo Cha wali maharage na chai. Suala la ukosefu wa chakula mashuleni linazaa utoro. Serikari Kwa kushirikisha wazazi waliangalie Kwa jicho pevu ili kuwasaidia watoto.
 
Mkuu mahitaji ni mengi hata kuliko hicho chakula kuna wanafunzi wanatembea kilomita 5km kuenda na 5km wazazi amekosa nauli ya 400, wengine hawana madaftari ya sh 500, wengine sare zimechaka sasa mkuu serikali ianze na lipi hasa katika hayo?
Mkuu Serikali haitaki ushauri hizo changamoto zinaweza kuisha maana Kama Serikali inanunua Magari ya mil 300 na kumpa Dc so kwanini ishindwe kuondoa changamoto za Elimu
 
Mkuu Serikali haitaki ushauri hizo changamoto zinaweza kuisha maana Kama Serikali inanunua Magari ya mil 300 na kumpa Dc so kwanini ishindwe kuondoa changamoto za Elimu
Mkuu wewe kama mtanzania unaona serikali ina "political will" ya kutatua hizo changamoto?.....au?
 
Nadhani hapa umepotoka kidogo kwakuwa maeneo yote hayo uliyotaja yana shule za kutosha sana
Je ulimaanisha hawa wanaokuja kusoma shule za katikati ya jiji?. Hawa huwa na ndugu ama wazazi mitaa hiyo na pia hawawezi kuwashindisha njaa kuanzia alfajiri mpaka usiku WATAKUFA
 
Africa huwezi kufanikisha maisha kupitia elimu bila mateso, lazima upitie chagamoto hizo hamna mafanikio kwenye silver-plate, hao wanao fanikisha bila kupitia ugumu wowote asilimia kubwa wana shindwa maisha au wana haribikiwa mapema, wengine wanakua mashoga mafisadi wezi wadangaji nk......pia hiyo ni sehemu ya maandalizi yetu kukabariana na maisha ya mbeleni. Ndo maana unaona watoto wawakubwa hawawezi ajira za ualimu kijijini kwenye mazingira hatarishi kuishi
 
Maisha ya wazazi wa mjini Mzazi anahama kila siku kutokana na Maisha leo yupo sinza Kesho kivule Sasa kwa style unadhani ni Rahisi Kupata kumuhamisha mtoto shule kila unapohama kimakazi .
Sasa hapo umlaumu serikali kwa kosa la mzazi?
 
Mkuu angalia shule za serikali hapa dsm , nakuambia hivi nikimaanisha sijaweka chumvi , ikifika jioni we pitia vituo vya daladala ujionee au muulize Mwalimu atakwambia then, wanafunzi wanasoma shule za Mbali sababu kuu wazazi wa dsm hawana makazi ya kudumu leo mtu yupo kinyerezi Kesho mbezi keshokutwa Mbagara.
 
Kwaiyo ulitaka iyo hela itoke wapi au tumkate mzazi kwenye mshahara kabla hajapokea tuipeleke shule?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwaiyo unataka serikali impe mzazi makazi ya kudumu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazazi wakiambiwa wachangie kidogo angalau watoto wapate tu uji shuleni ni vita!!!
 
Serikali ifanye mamgapi, wazazi fanyeni majukumu yenu mnataka mpaka watoto wenu walishwe na serikali?
Ndio serikali ni jukumu lake kuwapa wananchi wake maisha mazuri na elimu, kuwalisha watoto shule sio jambo geni, ikiamua inaweza.
 
Mkuu mahitaji ni mengi hata kuliko hicho chakula kuna wanafunzi wanatembea kilomita 5km kuenda na 5km wazazi amekosa nauli ya 400, wengine hawana madaftari ya sh 500, wengine sare zimechaka sasa mkuu serikali ianze na lipi hasa katika hayo?
Ifanye yote kwa wakati mmoja, ikiamua inaweza
 

Je, Wazazi nao wanazungumziaje suala la wanafunzi kukaa na njaa shuleni hadi usiku?​

Maana yake Serikali haiwezi kufanya kila kitu.
 
Hizo sababu zipo ila ukweli wake ni mdogo sana, uhalisia ni kwamba kuna wazazi wana ile kasumba kwamba shule za city center ni nzuri
Imagine mtoto anatoka Mbezi anaenda kusoma Magomeni kapita shule ngapi hapo katikati?
Na ishu ya kuhama nayo uongo tu, ina maama kila baada ya miezi mitatu mtu anahama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…