Je, Shekilango na Urafiki ndio Stendi mpya za Mabasi yaendayo mikoani?

Stand ya Magufuli Mbezi ulikuwa ubunifu usiokuwa na tija. Kwenda kurundika mabasi zaidi ya 300 yanayotakiwa kuondoka kwenda mikoani kwa wakati mmoja ni kituko. Dsm inahitaji stendi nyingi kulingana na eneo ambako magari yanaelekea.

Hapo Mbezi kwenyewe kutafuta gari linalohusika upande ni vurugu na mbinde.

Watu hawasemi lakini Stendi ya Mbezi haina tija kwa wananchi. Labda makusanyo ya serikali tu. Ndio maana mwanzishaji three hii kaona eneo moja tu la ukusanyaji mapato.
 
Asante mpiga debe umesikia, kaanga ksranga na choma mihogo uuze utapata hela nzuri kuliko kupiga debe.
 

Alichoandika mleta mada kina mantiki...

Kuna mabasi yanayoanza na kumalizia safari hapo Shekilango/Urafiki na hayafiki kabisa kwenye hiyo stendi mpya...

Abiria akihitajika kupanda basi, analazimika kwenda hapo Shekilango/Urafiki...

Ilianza kama utani hivi kwa New Force, Dar Lux na Kilimanjaro, lakini sasa hivi kuna makampuni si chini ya 15...
 

Idea nzuri sana mkuu, hapa ndipo linapokuja suala la exposure kwa viongozi wetu...

Miji mingi mikuu huko duniani huwa na stendi kuu zaidi ya moja, na stendi hizo hujengwa maeneo fulani kulingana na wapi magari yataelekwa kutokea hapo au pia kurahisisha wananchi kutotembea umbali mrefu kuifuata stendi...
 
Kwan lazima upande Dar lux...panda mengine yanayoenda unakoenda...acha ghiliba!
 

Ujumbe mzuri sana hata Ubungo mama yake ni mnazi mmoja serikali ikiwa na mautopolo mengi watavuna utopolo.
 
Acha uchochezi fazaaa
 
Kama alivyosema mdau mmoja hapo juu Viongozi wetu wengi hawajatembea au hawana maono ya mbali. Ni ushamba wa hali ya juu kuweka stendi moja kwa mji mkubwa kama Dar. Tulishindwa nini kujenge stendi kubwa kule Mbagala kwa ajili ya magari yanayoenda mikoa ya kusini??

Tulishindwa nini pale Mnazi mmoja pakachimbwa chini(undeground) kabisa pakawa na bus terminal kwa ajil ya watu wanaotoka katikat ya mji kuanza safar yao pale wakitaka kusafiri?? Tulishindwa kitu gani kuweka terminal kubwa huku upande wa Bagamoyo kisha tukajumlisha na hiyo ya Mbezi zikawa terminal 4. Yaani tuna wasomi wa mipango miji wa hovyo mno nchi hii na wana mawazo mgando
 
Sijui kwa hayo uliyotaja.. Ila Njombe express yetu inaingia Mbezi kisha inaenda urafiki
 
Sijui kwa hayo uliyotaja..ila Njombe express yetu inaingia mbezi kisha inaenda urafiki

Sawa, hao watakuwa wanafanya vyema...

Kuna mabasi yanayotokea pale Urafiki (sina haja ya kuyataja), breki ya kwanza huwa Kibanda cha Mkaa ambapo ndio itapakia abiria waliopaswa kupandia Mbezi Terminal, baada ya hapo ni safari kwenda mkoa...

Hiyo stendi bubu ya Urafiki/Shekilango iliasisiwa na makampuni machache wakati ule stendi kuu ikiwa Ubungo, na lengo lao lilikuwa ni kusaidia abiria wao kwa kuwapa huduma na mazingira mazuri wakiiga mifano ya wakongwe kama Scandinavia, Fresh ya Shamba...
 
Mleta uzi acha wivu, mabasi yote yanayoanzia safari Shekilango hasa yanayopita Morogoro road lazima yapite stendi ya Mbezi wakati wa kwenda na kurudi, na kuna baadhi yanayopita njia ya bagamoyo hulazimika tena kupitia mbezi. Kila basi linaloingia stendi linatoa ushuru, sasa sijui umefanya utafiti wako kwa muda gani au umekurupuka tu na kuandika.

Tukienda kwenye swala la kupeleka huduma karibu na mteja, sidhani kuna mfanyabiashara yeyote anayeweza kuamua kuweka huduma yake mahali ambapo hakuna uhitaji mkubwa, pale shekilango ni center nzuri kwa wasafiri na inafikika kwa urahisi na inapunguza adhabu kubwa ya kuamka saa 8 kuwahi mbezi na kuanza kupambana na wapiga debe tangu unashuka stendi ya daladala hadi kufika stendi ya Magufuli.
 
Una expose upumbavu wako na kwa jinsi gani ulivyo na wivu na roho mbaya
 
Mtu atoke Kigamboni akapandie gari Mbezi acha uzwazwa
 
Umeshaenda pale Magufuli stand siku za karibuni au umeambiwa tu?

Whether una tiketi au huna, hiyo 300 getting utalipa tu.

Unawajua Suma JKT?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…