Je, Shekilango na Urafiki ndio Stendi mpya za Mabasi yaendayo mikoani?


Una uhuru wa kuweka biashara mahala popote unapotaka cha maana eneo Ni lako Na halali!
 
Hizi ni ofisi kwa hiyo abiria anaetaka kupandia gari ofsini anaruhusiwa na zile ofic zilikuwapo hata kituo cha mbezi hakijajengwa, basi lolote lazima liingie ktk stendi kuu ya eneo husika hata kama halishushi abilia usipofanya hivyo unapigwa fain, na ukiingia kituoni unalipia.

Sasa basiyote ambayo ofic zao zipo nje ya au mbali na mbezi ikifika pale mbezi lazima liingie kituoni hata kama limejaaa,likiingia pale wanalipa ushuru wanaondoka, nakumbuka nilikuwa naenda dodoma kufika moro basi halikuingia kituoni likapita mbele tukakamatwa na trafiki akaandikiwa fain tikaendelea na safali ,huwenda umeandika kwa nia njema lkn umeandika kitu ambacho hukijui
 
Kwa Bagamoyo Road "Kibo Complex wasipafunge"Watafute eneo lenye Parking kubwa ,itasaidia mtu unakaa Mabwepande ukifikiria namna ya kwenda Stendi ya Mkoa unaingia gharama sawa na nauli ya basi
 
Acha wivu pale kuna ofisi za Mabasi ya mikoani na watu na hata Abiria uwa wanapandia pale kwani ni tatizo?
 
Sekta binafsi
 
Nashangaa sana Kila basi sasa limeanzisha kituo chake, yaani wengine Shekilango, wengine Tabata, wengine Buguruni n.k.

Mamlaka zipo kimyaaaaaaa.
LATRA wapo, Waizara ya usafirishaji wpo, n.k.
kinacho fanywa na baadhi ya makampuni ni uvunjifu wa sheria na taratibu, hivyo ni lazima sheria zisimamiwe.
 

Mfano new force inapotoka shekilango lazima ipite stendi ya mbezi, vile kwa dar lux...

Kuna basi za arusha, kaskazini yote zinazo zungukia chalinze , kuna basi ukanda wa arusha tanga moshi zinatoka stendi, kupita goba madale bagamoyo road.

Nenda rudi hivyo. Changamoto iko wapi
 

Yani unataka mtu atoke kongoe,ama kigamboni aende mbezi ilitu akalipe miambili getini kwaajili ya kumpokea nduguyake.

Kwanini unachukia watu wanapo rahisisha maisha.
 
Sio kweli, labda kama haujaelewa mada.
Hakuna basi ambalo halipakii wala kushusha abiria stendi ya Mbezi. Hii ni bila kujali kwamba basi hilo lina ofisi Shekilango ambako nako linapakia au kushusha.

Kwa kifupi, ni kosa kubwa kwa basi kutoingia stendi. Iwe ni stendi ya Mbezi, Kibaha, Stendi mpya Dodoma, Igumbilo, au yoyote ile.
 
kama inauma chomoa then ofisi ziwe wapi
 
Ni exposure tu tunakosa, Ila kwa jiji kubwa kama Das'lam kungekuwa na stand kubwa kama ya Mbezi sehemu tofauti ili kukidhi mahitaji na jiografia.

Kuweka stand Mbezi kungeenda sambamba na kuweka stand sehemu nyinginezo kama Bagamoyo road(Mwenge/Tegeta), Kilwa road(Mbagala) ili wanaoishi huko wawe na unafuu wa kuondoka na kuamua wapi pa kupandia gari.

Lakini pia, kufanya booking office kuwa stand sio sawa, Sheki ni ofisi za kununua tiketi, sio stand ya mabasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…