Je, shetani yupo? Anaishi wapi?

Je, shetani yupo? Anaishi wapi?

I meant mfano kwa nini wanaume walioumbwa kuwa wanaume watifautiane kiakili. Kwa nini capacity yao kushinda temptation za huyi so called satan zitofautiane?
OK OK hii Kumbe ni Kwa muktadha wa IQ nipe muda niiandalie mada kamili
 
shetani anaumbo na anaakili kama wewe na anakaa katika watu kama hauna Mungu basi ujue unashetani ndani yako! anakaaje mtafute Mungu atakuonyesha shetani anakaaje ndani ya binadamu! huyo shetani makao yao ya kukutania au makao makuu ni kuzimu lakini makao ya kufanyia kazi ni duniani!
Je wajuwa shetani ni mfalme wa ulimwengu?
 
Ndio shetani wapo wanaishi hapahapa duniani wanapatikana milimani, kwenye magofu, sehemu za majalala na kwengineko ndio ameachwa Mungu km nimtihan kwa binaadamu.

Kudhibitisha bila vitabu vya dini ni ngumu kwa sababu ndo kwenye evidence tosha.

Kinyume na hapo utadanganywa karibu simba wanga, Tanga , kilwa migodini na pemba utapata jibu kwa kuwahisi, kuwaona na maskan zao utaskia njia flan usipite ikifika jion.


Huyo kwa avatar yako ndio shetani mwenyewe,, usingejieleza, ungemwambia jamaa aone avatar yko tufunge mjadala
 
Kikubwa tunachokitaka sisi ni kuokoa muda wa vizazi vyetu. Hakuna kitu kinapoteza wakati na kufanya watu masikini kama kuamini kuna kitu kinaitwa mungu. Walio masikini wengi wanaamini maisha mazuri watakuja kuishi mbinguni. Na wanaaminishwa kuwa maisha ya duniani hayana thamani. Hiki ndo kitu ambacho mm sikupendi. Lazima tuwaambie ukweli watu wetu ili tuwe na vizazi vyenye kujielewa
Mkuu, we unaamini uwepo wa Majini, Uchawi, au Nguvu za kishirikina zinazotumiwa na baadhi ya waganga wa kienyeji?
 
Hapa duniani hamna cha shetani wala nini na ukuiona mtu kila kitu anamsingizia shetani ujue huyo ni bingwa wa kukwepa majukumu.
 
Mkuu we unashangaa leo? Mwenzio nilishashangaa nikazoea. Na wewe utazoea tu kama utakuwa unatembelea humu JF. Dunia hii acha tu!!!!

Hatari sanaaa!!!! Mdogo mdogo tutafika tu... Thank 4 ur quote
 
Shetan yupo kati yetu, kazi yake kubwa ya kwanza ni kutambua mawazo ya binadam anawaza au anataka kufanya nini, kama unawaza kutenda mema basi hapo atafanya linalowezakana kuvuruga mawazo yako mema, tukumbuke kuwa shetani ni malaika walioasi mbinguni, wakafukuzwa huko, kwa hiyo wana uwezo mkubwa kiakili na nguvu kuliko binadamu na bila msaada wa Mungu hatuwezi kushindana nao, matendo yote maovu yanatambulisha uwepo wa shetan. Shetan tunaishi naye majumbani mwetu, kazini, kwenye starehe, usiku na mchana yupo kati yetu akisababisha majanga mbalimbali kwa wanadam. Mashetani wamegawana kazi, wengine wapo kati yetu na wengine wapo huko msituni, miliman, baharini na kwengineko, kama mashetan wote wangeishi milimani, mtoni au baharini maovu yangekuwa machache sana katika jamii zetu. Tukumbuke kuwa tumejaliwa akili ya kutambua mema na mabaya pia shetan ni kama mmbwa aliyefungwa kamba kwenye mti hawezi kudhuru mpaka binadam ajipitishe karibu yake nikimaanisha kukubali kushawishiwa na kutenda dhambi.
 
Shetani yupo,na anaishi kwa mtu mwenyewe,,kwa upana zaidi,shetani ni ile hali ya mtu kufanya jambo kinyume na Mungu anavoagiza,au kinyume na jamii inavoona, ni kama kinyume cha mambo mema,kwangu Mimi shetan nafikiri sio kiumbe ila ni mawazo tofauti na mawazo mema ambayo humjia mtu
 
Hata nikirejea kwote huko, bado swali litajirudi kuhusu uwepo wa shetani. Maana shetani ndo alimlaghai hawa. Maana yake ni kwamba shetani alifuata order ya mungu kutokana na jibu lako kuwa uwepo wa shetani ni mpango wake. Kwahiyo uovu wote alionao shetani sio wakwake kwakua yeye ni mfuata order tu zinazotolewa na mungu
Hata uwepo wako ni mpango wa mungu! Na unafuata order bila hata kujua! Sema. Mabaya tunampa shetan wakati mengineyo ni maelekezo toka kwa mungu
 
Kinachotuumiza sana sisi ni kuamini kila tunachoambiwa bila kujua lengo la yule anayetuambia kuwa ni nini. Ukitumia muda mwingi kutafakari juu ya hili suala la uwepo wa mungu, hakika utapata majibu. Tatizo letu tulio wengi tunaogopa kwenda in deep
Et, uwepo wa mwanadamu ni Ku fail kwa mungu au?! Ukinijibu ntakutoa to go machon
 
Et, uwepo wa mwanadamu ni Ku fail kwa mungu au?! Ukinijibu ntakutoa to go machon
Hakuna kitu kinaitwa mungu. Ni mpango wa watu waliutengeneza ili wapate fursa ya kukutawala kiutamaduni. Ndio maana nasema kuamini uwepo wa mungu kwa watu wa sasa ni uvivu wa kufikiri. Tatizo lenu mnaamini msaada kuliko kujitegemea
 
Hakuna kitu kinaitwa mungu. Ni mpango wa watu waliutengeneza ili wapate fursa ya kukutawala kiutamaduni. Ndio maana nasema kuamini uwepo wa mungu kwa watu wa sasa ni uvivu wa kufikiri. Tatizo lenu mnaamini msaada kuliko kujitegemea
Wewe ulitokana na nini?!
 
Back
Top Bottom