Aisee kwa mara ya kwanza ndo naanza kujitambua au barehe, kuna pisi moja kali niliieelewa sana ilikuwa jirani na kwetu,, sasa nikaanza namna ya kuiambia shida yangu,,
Ilikuwa mtiti kutamka neno nakupenda kijasho kilinitoka na maongezi yaliyo jaa hofu, nilijikakamua nikamwambia unajua neema huku nikijikanyaga kijasho cha kutosha
Unajua mimi nimeshindwa tu kukwambia siku za nyuma ,neema mimi naku huku nikisita naku, nakupenda nataka tuwe wapenzi,,
Mara naye akadakia hata mie pia nilikuwa nakupenda ila nikuwa nashindwa kukwambia .
Mambo siyakawa mambo,, hapohapo tukapeana na ahadi kwamba ntamtafuta baadae.
Neema nilikupenda kwa dhati japo ulinipiga mizinga ya kutosha na ulicho nifanyia sitokisahau na ulinifunndisha mpaka sasa nimekuwa mgumu wa kuhonga.
Popote ulipo ntakukumbuka kwa mizinga yako. Hakika ulinikomesha.