Je, supu ya ngozi ya ng'ombe inayouzwa maeneo ya Mbagala ina usalama kiafya?

Je, supu ya ngozi ya ng'ombe inayouzwa maeneo ya Mbagala ina usalama kiafya?

Sirikali Haina budi kutupia macho hili swala, Hawa ndio wanasababisha bidhaa za ngozi kuwa hadimu na ghali.

Huko Serengeti na Mikumi Simba akiua ngozi hagusi anawaachia wazembe Fisi maji.
 
Inawekana sababu ikawa umaskini, lakini tujiulize, Wachina ni maskini, maana wao
Mbwa aliwa sawasawa, nyoka aina ya kifutu hapishwi, kwa Wenyeji wa Zanzibar, ni mashahidi, kipindi fulani Walikua wanunua paka kwa ajiri ya kufanya kitoeo.

Kule Singida walianzisha kiwanda kilichokua kinasindika soseji za punda.
Tanzania hatuli paka, mbwa, na nyoka, ispokua miguu na ngozi ya ng'ombe mnyama anaeliwa Duniani kote, na ukija kwetu, tunang'ombe wengi, ila tunakula damu yake, na mavi tunatengenezea kitu kinaitwa kichuri.
Wachina vyakula wanavyo kula siyo vipya ni jadi yao .. hapa tz tunakula vyakula vipya kuliwa mfano makwasu kwasu na supu ya ngozi....kuna tofauti hapo
 
Je supu ya ngozi ya ng'ombe inayouzwa maeneo ya mbagala inausalama kiafya

Wadau hamjamboni nyote?

Kichwa cha habari chahusika

Supu ya ngozi imayochanganywa na mapupu & bandama ambayo hupelekea rangi yake kuwa nyeusi ni maarufu maeneo tajwa

Wadau je kiafya kuna Usalama?

Karibuni tujadili
Ishi kulingana na mazingira na uhalisia wa vitu vinavyokuzunguka! ... As long as haidhuru afya yako!
Ishi kulingana na kipato chako!

Supu hiyo hiyo ya ngozi unayoweza kuidharau...tambua inauzwa kwenye migahawa mikubwa! Ya kichina,kihindu na kikurya!

Ni vile tu tunadharau vitu...huko wanajifanya eti kuongeza thamani...

Hakuna kinachoongezwa thamani! Bali ni namna tu ya kuchukua fedha yako kwa kubadilisha na kunakshi madhari ya upatikanaji wa bidhaa hiyo hiyo!

Embe la kibada Lina virutubisho mara100 ya maembe yanayopatikana sehemu hizo zenye hadhi! I.e supermarket
 
Inawekana sababu ikawa umaskini, lakini tujiulize, Wachina ni maskini, maana wao
Mbwa aliwa sawasawa, nyoka aina ya kifutu hapishwi, kwa Wenyeji wa Zanzibar, ni mashahidi, kipindi fulani Walikua wanunua paka kwa ajiri ya kufanya kitoeo.

Kule Singida walianzisha kiwanda kilichokua kinasindika soseji za punda.
Tanzania hatuli paka, mbwa, na nyoka, ispokua miguu na ngozi ya ng'ombe mnyama anaeliwa Duniani kote, na ukija kwetu, tunang'ombe wengi, ila tunakula damu yake, na mavi tunatengenezea kitu kinaitwa kichuri.
Kuna mfilipino alinicheka sana nilipomwambia kuwa kwetu hatuli ngozi,wala mapafu ya ngombe,aisee,akaniambia kuwa kwao wanatafuna kila kitu cha mnyama,yaani wakati ngombe anachinjwa kuna watu zaidi ya kumi wanaisubiria ngozi tu,na kuna namna ya kuipika,siyo kuchemsha tu na maji na chumvi, anasema ukibahatika kula ngozi iliyopikwa kifilipino hutatamani steki wala maini tena,ngozi inawekwa viungo hadi unaisahau,ila kuna hii inachemshwa na kimario hapa jirani,sinywi, hata kwa bunduki.
 
Kama unakula kongoro ...unaogopa Nini supu ya ngozi ya ng'ombe!?? ..... Kongoro ni ileile ngozi ya ng'ombe ila Ina mifupa Kwa maana ya kwato, bomba na pua zote ni ngozi.... Zinaandaliwa kama inavyoandaliwa supu ya ngozi.....
 
Je supu ya ngozi ya ng'ombe inayouzwa maeneo ya mbagala inausalama kiafya

Wadau hamjamboni nyote?

Kichwa cha habari chahusika

Supu ya ngozi imayochanganywa na mapupu & bandama ambayo hupelekea rangi yake kuwa nyeusi ni maarufu maeneo tajwa

Wadau je kiafya kuna Usalama?

Karibuni tujadili
Wamechelewa sana kuanza kutumia hiyo bidhaa. Nigeria wanakula ngozi kitambo sana.

Subiri idadi ya Watanzania ifike 200mil kama Nigeria nakwambia hadi mijusi mtakula
 
Kuna siku mida ya jioni nikajisemea leo nibadili ratiba ya pweza, nikala hiyo supu ya ngozi, sijawahi kuumwa tumbo na kukesha chooni kwa kiasi kile. Nilikoma
 
Hahahahahaha inaitwa supu ya magozi gozi, utotoni enzi hizoo Temeke sokoni kulee, tumekula saaana
Kipande ilikua shilingi 20
Ikifika jioni tuu, tunakusanyana watoto wa mtaani hapo Ruvuma, mkamba, Madenge tunaanza safari
 
Back
Top Bottom