Je, supu ya ngozi ya ng'ombe inayouzwa maeneo ya Mbagala ina usalama kiafya?

Sirikali Haina budi kutupia macho hili swala, Hawa ndio wanasababisha bidhaa za ngozi kuwa hadimu na ghali.

Huko Serengeti na Mikumi Simba akiua ngozi hagusi anawaachia wazembe Fisi maji.
 
Wachina vyakula wanavyo kula siyo vipya ni jadi yao .. hapa tz tunakula vyakula vipya kuliwa mfano makwasu kwasu na supu ya ngozi....kuna tofauti hapo
 
Ishi kulingana na mazingira na uhalisia wa vitu vinavyokuzunguka! ... As long as haidhuru afya yako!
Ishi kulingana na kipato chako!

Supu hiyo hiyo ya ngozi unayoweza kuidharau...tambua inauzwa kwenye migahawa mikubwa! Ya kichina,kihindu na kikurya!

Ni vile tu tunadharau vitu...huko wanajifanya eti kuongeza thamani...

Hakuna kinachoongezwa thamani! Bali ni namna tu ya kuchukua fedha yako kwa kubadilisha na kunakshi madhari ya upatikanaji wa bidhaa hiyo hiyo!

Embe la kibada Lina virutubisho mara100 ya maembe yanayopatikana sehemu hizo zenye hadhi! I.e supermarket
 
Kuna mfilipino alinicheka sana nilipomwambia kuwa kwetu hatuli ngozi,wala mapafu ya ngombe,aisee,akaniambia kuwa kwao wanatafuna kila kitu cha mnyama,yaani wakati ngombe anachinjwa kuna watu zaidi ya kumi wanaisubiria ngozi tu,na kuna namna ya kuipika,siyo kuchemsha tu na maji na chumvi, anasema ukibahatika kula ngozi iliyopikwa kifilipino hutatamani steki wala maini tena,ngozi inawekwa viungo hadi unaisahau,ila kuna hii inachemshwa na kimario hapa jirani,sinywi, hata kwa bunduki.
 
Kama unakula kongoro ...unaogopa Nini supu ya ngozi ya ng'ombe!?? ..... Kongoro ni ileile ngozi ya ng'ombe ila Ina mifupa Kwa maana ya kwato, bomba na pua zote ni ngozi.... Zinaandaliwa kama inavyoandaliwa supu ya ngozi.....
 
Wamechelewa sana kuanza kutumia hiyo bidhaa. Nigeria wanakula ngozi kitambo sana.

Subiri idadi ya Watanzania ifike 200mil kama Nigeria nakwambia hadi mijusi mtakula
 
Kuna siku mida ya jioni nikajisemea leo nibadili ratiba ya pweza, nikala hiyo supu ya ngozi, sijawahi kuumwa tumbo na kukesha chooni kwa kiasi kile. Nilikoma
 
Hahahahahaha inaitwa supu ya magozi gozi, utotoni enzi hizoo Temeke sokoni kulee, tumekula saaana
Kipande ilikua shilingi 20
Ikifika jioni tuu, tunakusanyana watoto wa mtaani hapo Ruvuma, mkamba, Madenge tunaanza safari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…