Je, taarifa ya ndege ya Air Tanzania kuanguka ziwani Victoria ni ya kweli?

Je, taarifa ya ndege ya Air Tanzania kuanguka ziwani Victoria ni ya kweli?

Mkuu leta uthibitisho umeme kukatiaka sio habari
Mrejesho kuhusu katizo la Umeme.

Ndugu wateja poleni kwa katizo la umeme lililopo hadi sasa.

Awali katika tangazo letu, matarajio ilikuwa umeme kurudi katika hali ya kawaida kuanzia majira saa tano asubuhi.

Kwa Bahati mbaya baada ya uchunguzi wa kina katika kituo chetu za Ubungo ambako tatizo limetokea, Imegundulika tatizo ni kubwa tofauti na ilivyoonekana hapo mwanzo.

Tunaomba sana radhi kwa kadhia hii

Mafundi wetu wapo eneo la tukio ili kuhakikisha umeme unarudi mapema iwezekanavyo katika vituo vingine vya kupokea na kupooza umeme.
 
Mwanzo nilijua umeme ni huku mtaani tu, daah na kuhusu hiyo ndege naona kama kuna haja ya kuweka maboya (life jacket) incase ikianguka sehemu za majini itasaidia kunusuru uhai wa abiria

Ndege yoyote ile ina maboya( life jacket)
 
Mwanzo nilijua umeme ni huku mtaani tu, daah na kuhusu hiyo ndege naona kama kuna haja ya kuweka maboya (life jacket) incase ikianguka sehemu za majini itasaidia kunusuru uhai wa abiria
Mkuu unafikiri ndege ikiangukia ziwani ama baharini itaelelea kama meli.
 
Duh, hii sasa shubiri kwa walopanga safari za sikukuu
 
Hii taarifa haina uhakika. Ndo mana swala lililoongelewa sana huku ni umeme
 
Kwa huu uhuni wa kubambikia watu vyesi hakuna Mungu wa kusikiliza kilio chenu, halafu bado mnashupaza shingo kwa kuleta vitu mtumba bado treni la SGR litachinja mpaka akili ziwakae sawa.
Amina.... na iwe hvooo coz halichagui wa kuchinja, likianzia na mama yako itakuwa poa sana😂
 
Hakuna ajali, bali yalifanyika mazoezi ya utayari Uwanja wa ndege Bukoba.
Vyovyote vile , hawajali MaCCM na hawachelewi kufanya propaganda kwenye dhiki za watu.
Hukuna wakuwaamini.
 
Najiandaa kwenda airport Dar kumpokea mgeni wangu napigiwa simu sasa hivi ndege iliyokuwa iwalete Dar imeanguka ziwa Victoria, uokowaji unaendelea.

Mwenye taarifa zaidi tujurishane maana Jiji zima la Dar na Zanzibar halina umeme.

=====
UPDATE ;
======

Hakuna ajali, bali yalifanyika mazoezi ya utayari Uwanja wa ndege Bukoba.
IMG_i283bh.jpg
 
2019 nilsafiri na ndege ya ATCL ilipofika Lake Victoria nilihofu sana haswa wakati inatua Mwanza.

Hofu yangu ilijengeka Kwenye msingi wa historia ya ununuzi wa hizi ndege na uzoefu wa ndege zenyewe.

Mungu awaponye tu
sio sawa kabisa, kwanza huyo mtoa UZI haja clarify ni ndege aina gani ya ATCL , isitoshe ndege hizi za ATCL ni za kisasa kabisaa mfano izi A220
 
Kuna ndege ya Air Tanzania kutoka Bukoba inajiandaa kutua Mwanza muda huu.... Hizi habari zina chembe ya ukweli au ni uzushi tu?
 
UPDATE ;
======

Hakuna ajali, bali yalifanyika mazoezi ya utayari Uwanja wa ndege Bukoba.

Mtoa mada katoa update muda kidogo.
 
Tatizo mnafikiri ajali ya ndege ni kama Kirikuu chako kikibinuka!
 
Back
Top Bottom