Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Apo ndipo wasiwasi unapotokea Kwa vijana wasaka mirija ya asali, hawezekani majibu ya oral yawen Siri, alafu placement zinachukuwa mwaka mzima,Huenda wakawa wanafanya kazi nzuri,ila hakuna uwazi haswa upande wa Oral interview,hawatoi result za oral interview ili msailiwa aone kabisa kama ameshindwa au amefanikiwa hata kuwepo kwenye database.
Pia kuwepo uhusiano wa result za written na oral interview.
Pia wanatumia muda mrefu sana kurelease majina ya waliofanikiwa kupata ajira,mpaka msahiliwa unajiuliza hivi hakuna uhitaji wa nguvu kazi wa haraka kwenye taasisi zilizo toa tangazo la ajira?
-Pia ukifanikiwa kuongea nao,jibu lao kubwa ni kua wapo wachache sana.
Kijana Mjinga sana uyo yani kitendo cha Kuchemka Kupambana na Wenzie PSRS basi analalama Waondolewe judistrication ya Kuajili ili tu Mjomba wake Amshike MkonoMleta Maada ni vile members wengi hawakufahamu humu ndani.Ila wewe ni mmoja ya msomi Mpuuzi,wewe unadhani serikali hawana akili mpaka wakaanzisha chombo Cha kuajiri???
Tunayejua magumu ya Ajiri ni Sisi tuulize huko kwenyewe Polisi,Takukuru,JWTZ tunaona kila siku rafiki zetu Wana sifa zote za kuwa askari na Wanapenda lakini wanakosa.Na hao wenzetu wanaopata kazi wanajisifu jinsi gani walipata hizo kazi kuwa vyomboni humo....
Ajira ambazo Sasa mtu anapata kihalali zote ni kupitia PSRS,ambao hao wanaratibu tu hizo Ajira kuanzia mitihani mpaka mwisho Huku wakishirikiana Kwa Kila kitu na Taasisi Husika.Ndio maana kwenye Oral Interview watu wa Taasisi husika baada ya Mchujo ndio wao Huamua wamchukue nani na wamuache Nani.Tena Maofisa wa PSRS wakiwepo wakisimamia kuhakikisha Haki imetendeka na hakuna upendeleo....
Sasa nikirudi kwako.Wewe ni mtu tunayekufahamu na unajisifu una ndugu zako Wakubwa baadhi ya Mashirika Kwa hiyo unataka wazo lako la kukosa/kushindwa saili za PSRS basi Mashirika ya ajili kisa wewe upate kazi???? Mimi nasema Acha Upuuzi...
Leo hii unaona kuna Vijana wenzetu wanaopata kazi Mashirika yote ambayo zamani walisema kama huna ndugu yake pale huwezi pata.Angalia Leo hii TRA,Brela,NAOT ,EGA, na kwingineko kwingi tu Kuna Vijana wengi wamepata fursa kupitia hii PSRS,Huku connection zao akiwa Mungu...
Mtanzania ni mtu asiyeridhika na kitu chochote kile kizuri,wewe ni mmojawapo.
Mimi kiufupi kama mwana CCM nasema PSRS ndio kimbilio la wengi na Waendelee kuajiri wao.Hatuoni malalamiko kabisa Kwenye Ajira,uwazi na kufuata kanuni ndio msingi wao.Unaona Majina ya Kuitwa Usaili wa Mchujo Kwa uwazi,unaona matokeo ya Mtihani wa Mchujo muhusika kupitia namba Yako,Lakini pia mwisho kwa Uwazi unaona Majina ya Kuitwa Kazini Kwa Uwazi kabisa.Aisee PSRS Raha Sana.
Ushauri wangu kwako kijana,Jiandae kikamilifu,pambana na Muombe Mungu ipo siku utafanikiwa.
PSRS Iko Juu[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
Mbona wale wa TRA mwaka Jana walipita, na mitihan ilivuja balaa, msijifanye nyie ni watenda wema,Kijana Mjinga sana uyo yani kitendo cha Kuchemka Kupambana na Wenzie PSRS basi analalama Waondolewe judistrication ya Kuajili ili tu Mjomba wake Amshike Mkono
🙏🙏Jk alikuwa na kipaji Cha uongozi alihakikisha Wananchi wanakuwa na maisha mazuri yenye furaha na matumaini , hakuwa na kiburi kama viongozi tunao waona SaSa ivi wakipewa madaraka wanavyotujibu vibaya.
Alihakikisha vijana wanapata ajira pindi wamalizapo masomo Yao, Tena kwa wakati , NGOs zilikuwa za kumwaga , nchi ilifunguka haswa, pesa zilikuwa nyingi kitaa watu tulifurahia maisha , ila SS imebaki story TU.
Jk kipindi Chake watu walikuwa wanabadilisha asali watakavyo, unatoka kwenye asali ya nyuki wakubwa unaenda kwenye asali ya nyuki wadogo, SS ivi ata asali ya kijiko hakuna , ikibahatika unapewa kombe la maji baridi.
Walimu walikuwa wakiji upgrade Kimasomo SS ivi nikama wamepigwa stop Kiana Yan.
Jk mungu akupe umri mrefu zaidi, bado tuna vitu vingi sana vya kujifunza kutoka kwako
View attachment 2581135
Jk alikuwa na Tunu ya uongozi 🤝, alikuwa anaamini hakuna linaloshindikana kwa njia ya mazungumzo,Mpaka majeshini, Mara ya mwisho aliajiri wanajeshi madereva la Saba, form fail asali kwa wote , watu walikuwa madereva tax, hiace, Sasa hivi makopro ma mp, jk mwana Sana.
Jk alikuwa na Tunu ya uongozi 🤝, alikuwa anaamini hakuna linaloshindikana kwa njia ya mazungumzo,Mpaka majeshini, Mara ya mwisho aliajiri wanajeshi madereva la Saba, form fail asali kwa wote , watu walikuwa madereva tax, hiace, Sasa hivi makopro ma mp, jk mwana Sana.
Umeandika kwa uchungu sana mkuu, Mimi nakuunga mkono 100%Ila naona malengo mazuri kabisa ya mkuu wa nchi, vibali vinatolewa ila usimamizi wa mchakato wa ajira na namna ya kuingia kwenye system kuna watu wamefanya kama kilakitu chakwao, wanaweka watu wao, hawafuati kanuni zinazo waongoza, wanafanya kazi kimazoea hawajui kuwa kuna kesho wao umri umeenda ndg zao wataingiaje kwenye asali baada ya wao kutoka hawafikirii. Wenzetu mataifa mengine wapo serious na ajira ambae anasifa anapewa bila konakona. Sasa ajira ilitangazwa mwaka jana tena may na june hii ni April na itafika july watu hata kazini hawajaitwa huu ni uzembe na ni magumashi ambayo Psrs hawana majibu ya kutupa tuwaelewe.Mambo ni nyoronyoro kama jongoo, yaani mwaka mzima wa fedha unasubiria kazi daah inaunmiza sana.
Hawa jamaa ifike sehemu wawe reliable mambo sijui paper limevuja, cjui nani alikuwa na maswali kabla ya interview, mara mnasubiri placement mwanka mzima tatizo ni nini.Mnajua data zote ni taasisi gani, wilaya gani zinataka watumishi kibali kipo tayari sasa siasa yanini kwenye hayo mambo,mkielemewa mseme muongezewe wataalam, nina hofu PSRS hamana wataalam wakutosha, Miundo mbinu na procedure zenu bado sana.
Maana kama una wataalam, professionals na watu wenye uzoefu hamuwezi enda hivyo. Hapo nimezungumzia wataalam wakutosha
Watu wa ICT tena Cerified IT ambao wapo current, watu wa mitihani maana hata paper zenu hazieleweki kesho hivi kesho vile ni vile mnajisikia kufanya au mtu kaamka anasema hii paper iwe hivi hamna utaratibu, tuna taka ethics za kazi yenu zizingatiwe.
Punguzeni mlolongo, mambo ya vikako kila siku vikao mambo yapo wazi yanawapunguzia ufanisi wa kazi.
Data base Data base ifanye kazi ,vijana tumechoka kurudi kufanya mausaili kila muda bila sababu. Leo mmetangaza wataalam wa maendeleo ya jamii lakini mnao wengi kwenye data base si walifanya mwaka jana usaili mmewaita wale wote, wapeni kazi madogo mtu kama amefaulu chuo na anaweza kujieleza kamati ya usaili imempa atleast passmark ya 50 mpeni kazi huo ndo utaratibu na ndio sheria, na kanununi inataka, tena mapaka waishe wote kwenye kanzi data ndio mtangaze..kuita kwenye usaili watu wanatoka tunduma, rombao, tarakea mwingine mbjnga, mwingine sengerema, nduta, nyasa, ludewa mnawatesa watoto wa watu provided hawana kazi za msingi za kuwainguzia kipato cha hayo magharama.
Hayo lazima tuongee na tutaongea mpaka kieleweke maana hiyo ni haki ya kila mtanzania .
Linswena
Mimi nilikuwa na wazo ndugu zangu,
Hebu tuache kulalamika nyuma ya keyboard na tutafute njia mbadala za kuelezea hili tatizo la michakato kuwa ya muda mrefu maana tunacholalamikia sio uchache wa nafasi ila ni michakato kutokuwa na ukomo,bahati mbaya hata wabunge wetu nao wakati wa kujadiki bajeti walijikita kwa walinu na wataalam wa afya tu as if nchi ina wasomi na wahitaji ajira kwa kada hizo tu!!
Nadhani kuna haja ya kutafuta watu wenye ushawishi waite press na kuiadress hii inshu vizuri ili ieleweke, na press yenyewe waainishe na mifano ya michakato iliyochukua muda mrefu na mingine kuishia hewani bila kurudi na feedback za placement, na watu wa kuweza kuzungumzia hili jambo kwa upana huu ni either mwenyekiti wa vijana BAVICHA AU ACT na tena isiwe humu kwenye mitandao ya kijamii bali iitwe press na hili jambo lisemwe kwa upana wake,
Humu tumeshalalamika sana bahati mbaya kwa utafiti wangu ni kuwa kilio chetu kinaishia kwa wale wale wanaocheleweaha mchakato,basi ni heri waseme watu wote mlifeli au wasiite interview maana ni haki ya mtu kupata matokeo kwa kile alichofanya,sasa hivi kila siku ni mchakato mchakato,hivi kuna mchakato sensitive kama wa uchaguzi??mbona unaisha muda mfupi??lkn huu wa ajira ni kama wa chura napo hadi apigwe teke ndio asogee,watu kila siku wanalalamika wanafata barua na kukuta zina zaidi ya mwezi tangu ziandikwe lkn tukirudi huku kauli ni mchakato.
Hebu tuamke tuone namna iliyo bora ya kufikisha taarifa kwa wahusika wa maamuzi,mtu kama pambalu au nondo wanatakiwa waite press na kuichambua hii kitu kwa upana ieleweke kwa jamii.
Dbaba Martin Maranja Masese
Kilaza kwann?Mwambie mjomba wako pale TRA kuwa mambo yamekua magumu, saili zote lazima zipite utumishi.
Jifue ukagombanie ajira na wenzio utumishi, hatutaki watumishi vilaza kwenye mashirika yetu kisa tu wana connection