Je, Taasisi za Serikali hazina watumishi wenye Sifa hadi Wakurugenzi Wakuu Wateuliwe toka Nje ya Mfumo?

tutafikatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Posts
3,327
Reaction score
4,624
Thread hii, inatokana na baadhi ya teuzi za wakurugenzi wa TANESCO na MSD kutoka nje ya mfumo. Nina declare interest kwamba sina shida na teuzi ya MSD. Ni mmoja wa colleagues tuliyekuwa tukifanya naye kazi nje ya mfumo. Ninaamini anastahili, na ataweza.

Tatizo linatokea hapa.

1. Hivi inakuwaje nchi yenye watumishi wa serikali zaidi ya 500,000 ikose mtu mmoja wa kuongoza taasisi kama MSD au TANESCO? Je, viongozi wa taasisi ndogo ambao wanaweza pata promotion ya kupewa nafasi kama hizo hawajiwezi? Kama hawajiwezi kuchukua nafasi kama hizo kwanini wasiwapishe watanzania wengine ili kuwaandaa watu wapya kwa nafasi kama hizo?

2. Katika hao watanzania 500,000 walioajiriwa na serikali, hakuna watu ambao mpaka sasa hawajapata nafasi za uongozi na bado wanaweza fanya vizuri? Kwani ili upewe nafasi ya uongozi lazima uoneshe uzoefu wa kuongoza? Watumishi hawa uzoefu waoneshee wapi? Kwani hakuna traits ambazo zinaweza tumika kuibua kiongozi mzuri?

3. Kama huu mfumo wa kuchukua watu toka nje ya mfumo unafaa na vyombo vyetu vya vetting vinaona ni mzuri kwanini huu huu mfumo tusiutumie na kwenye vyombo kama Majeshi ya Ulinzi na Usalama, TISS na PCCB? Kwani huko kuna kitu gani special wanachofanya hadi nafasi zao zilindwe ndani ya mfumo? Mtu akiwa vizuri apate nafasi na kumwingiza kwenye mfumo husika.

Sina shida na wateuliwa, wanastahili, ila ninahisi kuna shida mahala hasa katika kutafuta watumishi wa serikali wenye sifa na kuwafanyia vetting.

Kwanini hawa jamaa wa vetting wasiwe wanaadhibiwa kwa kutofanya vetting nzuri? Yaani katika watumishi laki tano ukose mtu wa kuongoza MSD au TANESCO?

HII NI AJABU.
 
Serikalini usipofahamika hakuna kupewa nafasi. Hata kitengo ukikisia wizarani basi fuatilia huyo aliyepewa hiyo position lazima atakuwa na uhusiano na kiongozi mkubwa.
Hilo nalikubali asilimia 100. Kuna shida mahali.
 
Kunahitajika mawazo Mapya na uzoefu mpya

Serikalini wengi kelele tu utasikia toka Miaka hiyo toka enzi za Nyerere tunafanya hivi hivi utaniambia nini

Mfano mzuri ni kitengo cha Passport toka kianzishwe enzo za Nyerere kuipata lazima ulete barua sijui ya mwaliko 'uthibitisho wa safari nk
Hawajui kuwa Passport inatakiwa hata kufanya mitihani ya nje online na kuombea scholarship nk online

Kuwaambia badilikeni hawasikii ohh kijana utatuambia mini mimi mwaka wa 30 huu anafanya hivi hivi Sehemu kama hizo kuweka mtu wa ndani hapo hapo ni majengo

Uelewa wa private sekta maeneo mengi mkubwa kuliko walioko serikalini

Ofisa biashara wa Serikali unakuta kafanya kazi Miaka 20 kazi yake kusaini leseni za biashara huwezi linganisha na mfanyabiashara aliyeko private sekta.Ukiteua Waziri au katibu mkuu wizara ya biashara kutoka private sekta unakuwa umefanya la maana kuliko kuteua huyo mtia sahihi kwenye leseni kushika hivyo vyeo hajui kitu hata ukimpa ubalozi sijui iwatafute wawekezaji anaanzia wapi kichwani kweupe.Yuko so narrow kichwani

Mabalozi tulionao wengi kichwani kweupe kutarajia sijui watasaidia diplomasia ya uchumi na biashara ni uongo

Teuzi Serikali iangalie na private sekta kuna watu wanajua mavitu hasa kuwazidi hao akina uzoefu Miaka kibao Serikali au taasisi za umma

Ku inject new things vizuri pia kuchukua private sector

Mfano humu tumepiga kelele PayPal iruhusiwe kwa watanzania kupokea pesa serikalini huko hakuna hata mtu anaelewa PayPal ni nini hata huko wizara ya fedha na biashara.Kwa hali hiyo bila kuchukua private sector hatufiki mbali
 
Acha huko kwny mashirika,huko Local government tu nako mambo yamehorojoka miaka hii.Kuna siku Magu alikua amamhoji mkurugenzi wa halmashauri moja akamuuliza wewe kabla ya kuja kufanya kazi hapa ulikua unafanya Kazi wapi,jamaa akajibu Marekani mkuu.Magu akawamwambia kwa hio huko Marekani ndipo ulipofundishwa huu upumbavu unaoufanya 😄😄

So point yangu ni kua yaani siku hadi local govt wanaletewa wakurugenzi kutoka Marekani huko,ajabu Sana hii.
 
Kunahirajika mawazo Mapya na uzoefu mpya

Serikalini wengi kelele tu utasikia toka Miaka hiyo toka enzi za Nyerere tunafanya hivi hivi utaniambia nini

Mfano mzuri ni kitengo cha Passport toka kianzisge enzo Nyerere kuipata lazima ulete barua sijui ya mwaliko 'uthibitisho wa safari nk
Hawajui kuwa Passport inatakiwa hata kufanya mitaani ya nje online na kuombea scholarship nk online

Unaonaje tukistaafisha watu wote laki tano tukaleta damu mpya? Au kama ngumu, huko MSD tukatoa waajiriwa wote na kupeleka wenye mawazo mapya. Ikiwa ngumu sana, basi tuanze kupeleka watu kwa stahili hizi hata kwenye Kurugenzi na Idara za TISS zinazopwaya.
 
Hii ni ajabu sana. Au tunaongozwa na remote ya wale wanaofanya vetting ambao wanajua nafasi zao ziko safe.
 
Hamna lolote kujuana tu
Wanaofanya kazi ni watu wa chini sio Kiongozi wa Taasisi
 
Unaonaje tukistaafisha watu wote laki tano tukaleta damu mpya? Au kama ngumu, huko MSD tukatoa waajiriwa wote na kupeleka wenye mawazo mapya. Ikiwa ngumu sana, basi tuanze kupeleka watu kwa stahili hizi hata kwenye Kurugenzi na Idara za TISS zinazopwaya.
Kinachotakiwa ni juu kubadili huko ndiko kuna shida

Mfano mdogo .wafanyakazi wa Serikali na sekta binafsi husoma Vyuo vilevile darasa moja chuo kimoja ndani na nje ya nchi

Lakini mashirika mengi ya umma na mabenki yalikufa wakati hayana mshindani!! Mfano National Milling Corporation ilikufa Kampuni za usafirishaji kama KAMATA nk zilikuwa,mabenki kama THB na NBC chini ya wazawa zikafa

National Housing ilikuwa inakufa Serikali ikachukua private Sector Mchechu kuwa mkurugenzi mtendaji ndio ikaamuka!!!
Tukubali tu kuwa kuna maeneo mtu wa ndani haitakiwi kupewa.Hawana competence na mawazo Mapya kazi wanazoweza ni zile za ki desk officer za business as usual za kutumwa fanya hiki na ufanye hivi.Unamwekeza wee na kumuuliza umeelewa eee nielewa anaanza kufanya hayo aliyoyaelewa .Lakini kuwa na new ideas na innovation hamna kitu kichwani harabupeleke seminar Ulaya anarudi tu na album Imejaa picha alizopiga tu kichwani hamna kitu kipya kaja nacho
 
Kunahirajika mawazo Mapya na uzoefu mpya

Serikalini wengi kelele tu utasikia toka Miaka hiyo toka enzi za Nyerere tunafanya hivi hivi utaniambia nini

Mfano mzuri ni kitengo cha Passport toka kianzisge enzo Nyerere kuipata lazima ulete barua sijui ya mwaliko 'uthibitisho wa safari nk
Hawajui kuwa Passport inatakiwa hata kufanya mitaani ya nje online na kuombea scholarship nk online

Kuwaambia badilikeni hawasikii ohh kijana utatuambia mini mimi mwaka wa 30 huu anafanya hivi hivi Sehemu kama hizo kuweka mtu wa ndani hapo hapo ni majengo

Uelewa wa private sekta maeneo mengi mkubwa kuliko walioko serikalini

Ofisa biashara wa Serikali unakuta kafanya kazi Miaka 20 kazi yake kusaini leseni za biashara huwezi linganisha na mfanyabiashara aliyeko private sekta.Ukiteua Waziri au katibu mkuu wizara ya biashara kutoka private sekta unakuwa umefanya la maana kuliko kuteua huyo mtia sahihi kwenye leseni kushika hivyo vyeo hajui kitu hata ukimpa ubalozi sijui iwatafute wawekezaji anaanzia wapi kichwani kweupe.Yuko so narrow kichwani

Mabalozi tulionao wengi kichwani kweupe kutarajia sijui watasaidia diplomasia ya uchumi na biashara ni uongo

Teuzi Serikali iangalie na private sekta kuna watu wanajua mavitu hasa kuwazidi hao akina uzoefu Miaka kibao Serikali au taasisi za umma

Ku inject new things vizuri pia kuchukua private sector

Mfano humu tumepiga kelele PayPal iruhusiwe kwa watanzania kupokea pesa serikalini huko hakuna hata mtu anaelewa PayPal ni nini hata huko wizara ya fedha na biashara.Kwa hali hiyo bila kuchukua private sector hatufiki mbali
Hivi sasa pasipoti ni kama anasa.
Sisi tulio huku mikoani na mbali na mkoa ni changamoto sana.
Nilipokuwa nashughulikia yangu niliambiwa hivyo hivyo kuwa wanahitaji barua ya mwaliko.
Hivi Dunia ya sasa bado watu wanaalikana kwa barua?
Hivi ndugu yangu aliyeko nje ya nchi akiugua ghafla nami nikahitajika kwenda kumuuguza, kumuongezea damu nk itakuwaje? Pasi itapatikana kwa dharula?
Hivi nikitaka kwenda kutalii nani atanipa barua ya mwaliko?

Ofisi ya PSSSF wanakwama wapi kufungua ofisi wilayani [kama NSSF] wakati ndiko waliko maelfu ya wateja wao?
Wakati umefika huduma na uhakiki ufanyike wilayani badala ya mkoani.
Kuna wastaafu walemavu au wagonjwa ambao kusafiri ni lazima wawe na gari MAALUM [binafsi] kwa kuwa hawezi kutembea.
Hawa wanatumia gharama kubwa ambapo hawana pesa.
Vile vile wanalazimika kugharamia watu wawili au zaidi wanaowasindikiza. Ongeza chakula na malazi.
 
Thread hii, inatokana na baadhi ya teuzi za wakurugenzi wa TANESCO na MSD kutoka nje ya mfumo. Nina declare interest kwamba sina shida na teuzi ya MSD. Ni mmoja wa colleagues tuliyekuwa tukifanya naye kazi nje ya mfumo. Ninaamini anastahili, na ataweza.

Tatizo linatokea hapa.

1. Hivi inakuwaje nchi yenye watumishi wa serikali zaidi ya 500,000 ikose mtu mmoja wa kuongoza taasisi kama MSD au TANESCO? Je, viongozi wa taasisi ndogo ambao wanaweza pata promotion ya kupewa nafasi kama hizo hawajiwezi? Kama hawajiwezi kuchukua nafasi kama hizo kwanini wasiwapishe watanzania wengine ili kuwaandaa watu wapya kwa nafasi kama hizo?

2. Katika hao watanzania 500,000 walioajiriwa na serikali, hakuna watu ambao mpaka sasa hawajapata nafasi za uongozi na bado wanaweza fanya vizuri? Kwani ili upewe nafasi ya uongozi lazima uoneshe uzoefu wa kuongoza? Watumishi hawa uzoefu waoneshee wapi? Kwani hakuna traits ambazo zinaweza tumika kuibua kiongozi mzuri?

3. Kama huu mfumo wa kuchukua watu toka nje ya mfumo unafaa na vyombo vyetu vya vetting vinaona ni mzuri kwanini huu huu mfumo tusiutumie na kwenye vyombo kama Majeshi ya Ulinzi na Usalama, TISS na PCCB? Kwani huko kuna kitu gani special wanachofanya hadi nafasi zao zilindwe ndani ya mfumo? Mtu akiwa vizuri apate nafasi na kumwingiza kwenye mfumo husika.

Sina shida na wateuliwa, wanastahili, ila ninahisi kuna shida mahala hasa katika kutafuta watumishi wa serikali wenye sifa na kuwafanyia vetting.

Kwanini hawa jamaa wa vetting wasiwe wanaadhibiwa kwa kutofanya vetting nzuri? Yaani katika watumishi laki tano ukose mtu wa kuongoza MSD au TANESCO?

HII NI AJABU.
Umeuliza swali zuri sana kifupi mifumo yetu ilishakufa mkuu na sio kweli kwamba hawapo wenye uzoefu wapo wengi mno wazuri sana tatizo siasa tatizp connection mfano mdogo miongozo ya tamisemi inataka DED awe walau mkuu wa idara kwa kipindi kisichopungua miaka 5 lakini sote tunajua nini kinafanyika makada ambao hata kwenye utumishi wa umma hawakuwepo ndo wameteuliwa
 
Kifupi kila taasisi ya umma na huko serikalini kila bosi ajitafakari utendaji wake.Na ni vizuri atizame udhaifu hasa unaolalamikiwa na wadau uko eneo lipi afanyie kazi vinginevyo aweza jikuta mtu anatokea private sector kuja kuchukua nafasi yake sio lazima iwe ya juu kabisa yaweza kuwa hata ya middle Management kwenye eneo lionekanalo kuwa critical. Sio vizuri kubweteka na uzoefu ohh nina Miaka 30 nafanya kazi hii hii !!!! Cha ziada nini?
 
Ni kweli mkuu.
 
Bro kati ya watumishi laki 5 wanakosa wanaenda private?
 
Wanaojua kazi ni Wakurugenzi chini ya DG
Twende kilichosababisha taasisi za biashara za umma na mabenki na viwanda kufa zilikuwa nini ? Hawakuwa na wakurugenzi? Wakati mashirika yalikuwa na monopoly hayana mshindani
 
Back
Top Bottom