tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,327
- 4,624
Thread hii, inatokana na baadhi ya teuzi za wakurugenzi wa TANESCO na MSD kutoka nje ya mfumo. Nina declare interest kwamba sina shida na teuzi ya MSD. Ni mmoja wa colleagues tuliyekuwa tukifanya naye kazi nje ya mfumo. Ninaamini anastahili, na ataweza.
Tatizo linatokea hapa.
1. Hivi inakuwaje nchi yenye watumishi wa serikali zaidi ya 500,000 ikose mtu mmoja wa kuongoza taasisi kama MSD au TANESCO? Je, viongozi wa taasisi ndogo ambao wanaweza pata promotion ya kupewa nafasi kama hizo hawajiwezi? Kama hawajiwezi kuchukua nafasi kama hizo kwanini wasiwapishe watanzania wengine ili kuwaandaa watu wapya kwa nafasi kama hizo?
2. Katika hao watanzania 500,000 walioajiriwa na serikali, hakuna watu ambao mpaka sasa hawajapata nafasi za uongozi na bado wanaweza fanya vizuri? Kwani ili upewe nafasi ya uongozi lazima uoneshe uzoefu wa kuongoza? Watumishi hawa uzoefu waoneshee wapi? Kwani hakuna traits ambazo zinaweza tumika kuibua kiongozi mzuri?
3. Kama huu mfumo wa kuchukua watu toka nje ya mfumo unafaa na vyombo vyetu vya vetting vinaona ni mzuri kwanini huu huu mfumo tusiutumie na kwenye vyombo kama Majeshi ya Ulinzi na Usalama, TISS na PCCB? Kwani huko kuna kitu gani special wanachofanya hadi nafasi zao zilindwe ndani ya mfumo? Mtu akiwa vizuri apate nafasi na kumwingiza kwenye mfumo husika.
Sina shida na wateuliwa, wanastahili, ila ninahisi kuna shida mahala hasa katika kutafuta watumishi wa serikali wenye sifa na kuwafanyia vetting.
Kwanini hawa jamaa wa vetting wasiwe wanaadhibiwa kwa kutofanya vetting nzuri? Yaani katika watumishi laki tano ukose mtu wa kuongoza MSD au TANESCO?
HII NI AJABU.