Je, Taasisi za Serikali hazina watumishi wenye Sifa hadi Wakurugenzi Wakuu Wateuliwe toka Nje ya Mfumo?

Umezunguka sana kuwaponda watumishi wa umma lakini huelewi kuwa serikalini kazi nyingi zinafanywa kwa compliance ya either sheria ya bunge na kanuni zake au miongozo na nyaraka mbalimbali kutoka kwa wakubwa juu...
Hakuna mawazo binafsi serikalini
Hayo ni kwa Bakhresa na Mo huko ambao wakiamua asubuhi wanatoa maelekezo jinsi ya kufanya uhasibu...
 
Twende kilichosababisha taasisi za biashara za umma na mabenki na viwanda kufa zilikuwa nini ? Hawakuwa na wakurugenzi? Wakati mashirika yalikuwa na monopoly hayana mshindani
Wanasema sababu ni Nyerere na Mkapa
 
Ndio jibu hilo,watu wasio na ufanisi na wezi huwa hawategemewi.

Nikiangalia kesi ya NHC ilivyokufa na TIC ilivyokuwa imesinsia au hata TBC ni dhahiri Serikalini kuna watu wasiojitambua wengi Sana.

Kama customer care tuu inawashinda wataweza management zinazohitaji biashara kweli?

Hata sgr ikikamilika walete mtendaji kutoka kwenye sekta binafsi..

Pia serikali itazame atcl.
 
MIMI NASHAURI BADALA YA KUTEUA NAFASI HIZO ZITANGAZWE WATU WENYE SIFA WATAOMBA MCHUJO UTAFANYIKA ATAKAE KUWA NA VIGEZO NDIO ATEULIWE
 
Bro kati ya watumishi laki 5 wanakosa wanaenda private?
Inawezekana kabisa akakosekana

Nitakupa mfano Serikalini mtu hufaninyi kazi zote Unapewa kakipande kadogo tu.Mfano idara ya Bohari wako 200 nchi nzima kazi zao Bohari tu kufanya kazi Miaka 20 Bohari tu

Idara ingine uhasibu wako 100 kazi yao uhasibu tu Miaka 20

Idara nyingine manunuzi wako 100 kazi yao kununua tu uzoefu miaka 20

Private sector unakaa sehemu unapita kazi zote mwenyewe Inakupa uzoefu mkubwa tena mno kwenye level ya management.Serikalini.mgawanyo wa kazi uko shallow sana hampi.mtu uwezo na uzoefu overall wa ki Management kwa high lev


Kiongozi wa juu anatakiwa mwenye combination nyingi kwa mpigo key arrears zinazosumbua eneo husika

Pili. Mtu aweza toka nje kusaidia kutafuta changamoto sugu ambayo watu wa ndani hata wawe maelfu wameshindwa kuitatua pamoja na kupigwa kelele mno

Mfano Tanesco ilikuwa ina matatizo makubwa kifedha na huduma kwa wateja hazina kila siku ilikuwa kupeleka tu pesa Tanesco ruzuku Serikali ikamchukua mchumi toka private sekta Dr Idris Rashid akaenda atajisaidia shirika sana eneo la utendaji na ukusanyaji mapato .Tanesco walivyokuwa wenyewe na hao maelfu ya wafanyakazi wao wenye uzoefu Miaka kibao' umeme ulikuwa ukiomba unaupata baada ya miaka mitatu kupita na kwenda kulipia iwe billi ya umeme ilikuwa unatenga siku nzima kwenda kupanga foleni kulipia na mbili yenyewe ya kutambambikiwa na inakuja imechelewa kufungiwa umeme ukiomba ukibahatika unafungiwa baada ya Miaka mitatu.na hauingii.utapigwa porojo kuwa mita chache hadi uhonge nk

DR Idris ndiye alibadili utendaji kazi na kuleta Luku

Hao wa ndani uwezo wa kufikiri ulishafikia ukomo.wakawa tu wafanyaji kazi wa business as usual hamna jipya!!
 
Sawa lakini ubunifu ni zero huko Serikalini..

Nakupa mfano mdogo wa sekta ya barabara,hivi inakuaje Serikali ikitaka kujenga mradi mzuri wa barabara hadi wakakope WB au msaada wa wahisani?

Kwa mfano saizi Tarura amepewa zaidi ya bil.800,kusema tuu kwamba tutumie pesa walau bil.200 kwa kujenga barabara zetu za lami kwenye miji yetu japo kwa awamu hatuwezi hadi twende kwa mzungu?

Matokeo yake pesa zote hizo zinaishia kwenye mabaraba ya vumbi ambayo yanasombwa na maji kila siku..At the same time wanaenda Kukopa pesa kama hizo kujengea lami.Hizi ni akili au matope?
 
Hako Tarura ni Majanga, wanajua taratibu zote za ujenzi WA barabara Bora ila wamekuwa ndio wajenzi WA barabara bila Weledi!! Ni kama hizo Hela zipo kwenye pakacha linalovuja!!
 
Tatizo ni teuzi kwà utashi wa anayeteua na hata pasina kuulizwa na yeyote.Huo mwanya unatumika kuchomekana kwingi na kufanyiana hiana kwingi pia.Hapa Tanzania hautakiwi kushangaa shangaa yanayotokea.Mifumo mingi imevurugwa kiasi kwamba wananchi hawana mamlaka yoyote juu ya yanayotokea au kuamuliwa na wanasiasa uchwara.Utaalam wa watumishi hauthaminiwi na hayo ndiyo matokeo yake.
Tunatakiwa kusisitiza na kuhimizana juu ya hitaji la Katiba Mpya itakayonyoosha na kujenga taasisi imara za kiuongozi kwa nchi yetu kwa kurudisha mamlaka ya wananchi.
Msingi wa yote lazima uwe wananchi.
 
Haki sawa kwa wote ngoja aje nae akutane na urasimu, maagizo, sheria, kanuni, taratibu na miongozo, ubabe na usaliti, unateuliwa lakini hupewi autonomous control na freedom ya kupractice uweledi. Tunamtakia heri kwenye upigaji
 
Pia ndugu ujue kwenye vumbi huko hakuna value for money!! Mtu anakwambia tumeweka layer ya 150mm morram ila kipindi Cha audit unakuta Mvua ilishanyesha na kifusi hakipo Tena!! Full upigaji
 
Muarobaoni wa yote ni Katiba Mpya
 
Na vitambulisho vya NIDA pia
 
Pia ndugu ujue kwenye vumbi huko hakuna value for money!! Mtu anakwambia tumeweka layer ya 150mm morram ila kipindi Cha audit unakuta Mvua ilishanyesha na kifusi hakipo Tena!! Full upigaji
Ndio maana napinga kutumia pesa nyingi kujenga mavumbi,hii hapana kwa sababu Kwa miaka 5 tutajikuta tumetumia matilioni ya pesa ila hakuna cha kuonyesha..

Serikali Ike upya iseme pesa ya tozo iwe kwa lami tuu hasa mijini
 
Tena sekta zote wakichukua watu wa nje itafaa Sana .
Watu wa serikalin ni watu wazembe wajivuni ,kibri ,rushwa Sana .

Unaenda ofisini boss wa sehem husika anakuona km kikalagosi tu ,umakini ziro kabisa mazoea yamezidi mno.
 
Tena sekta zote wakichukua watu wa nje itafaa Sana .
Watu wa serikalin ni watu wazembe wajivuni ,kibri ,rushwa Sana .

Unaenda ofisini boss wa sehem husika anakuona km kikalagosi tu ,umakini ziro kabisa mazoea yamezidi mno.
Naunga mkono hoja
 
Ndio maana napinga kutumia pesa nyingi kujenga mavumbi,hii hapana kwa sababu Kwa miaka 5 tutajikuta tumetumia matilioni ya pesa ila hakuna cha kuonyesha..

Serikali Ike upya iseme pesa ya tozo iwe kwa lami tuu hasa mijini
Hapo umenena!! Sitaki kuwasifia watu au kuwasema vibaya, mheshimiwa Lowassa alishaliona Hilo la loop Holes na alishawahi kupiga marufuku ujenzi WA hizi barabara za Vumbi!! Alishauri watu wajenge Lami nzuri kulingana na budget!! Kama una budget ya km 2 Bora ujenge hapo kuliko km 10 ambazo ni Vumbi na hazidumu hata miezi SITA!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…