Je, Taasisi za Serikali hazina watumishi wenye Sifa hadi Wakurugenzi Wakuu Wateuliwe toka Nje ya Mfumo?

MIMI NASHAURI BADALA YA KUTEUA NAFASI HIZO ZITANGAZWE WATU WENYE SIFA WATAOMBA MCHUJO UTAFANYIKA ATAKAE KUWA NA VIGEZO NDIO ATEULIWE
Hii point
Raisi apelekewe majina matatu ateue mojawapo

Ila kama hatatokea yeyote ndio ateue
 
MIMI NASHAURI BADALA YA KUTEUA NAFASI HIZO ZITANGAZWE WATU WENYE SIFA WATAOMBA MCHUJO UTAFANYIKA ATAKAE KUWA NA VIGEZO NDIO ATEULIWE
Nadhani pia kuna baadhi ya post tusiogope hata kuwatafuta kimataifa wazoefu

Mfano Tanroads Raia wa Ghana ndie alikuja kuisuka na kuiweka hivyo ilivyo akiwa mkurugenzi mtendaji

Kama skill hazipo tuagize nje lengo nchi isonge mbele
 
umeongea points tupu
 
Kuwa CEO sio mchezo jamani. Huku utumishi wa umma tunajuana. Viongozi wetu ni watupu mno na hawana exposure.
Hawajui hata kutumia techniques zaidi ya moja ili kuzifikia targets. Wanafanya mambo kwa mazoea, style zilezile za kizamani. Ukileta jambo jipya unatimuliwa kama nini sijui.
Bora haohao wa private sector wameshaongoza taasisi mbalimbali za kimataifa, zenye targets mahsusi, zinazojali uwajibikaji na delivery sio blaablaa. Hao ndio wanafaa kuongoza haya mataasisi makubwa ya serikali.

Ingekuwa wakuu wa idara za serikali wanafanya vyema kwa kiwango cha kustahili kuwa maCEO au Watendaji wakuu basi tungeona tu kwa kupata huduma nzuri za serikali kupitia vitengo na taasisi zao lakini mpaka leo taasisi nyingi zinatoa huduma mbovumbovu. Sasa hapohapo ndio umchukue mmoja wao eti akawe CEO hakuna jipya atafanya zaidi ya kuloga walio chini wasipande na kumfikia.


Katika hili mama anaupiga mwingi sana kuleta new minded person kwenye seekta ya umma.
 
Networking with payback
 
1. Connection
2. CCM
3. Kujipendekeza.
4. Kamlete.
Unakumbuka yule dogo wa degree moja akapewa ukurugenzi TPDC na akatumbuliwa kabla ya kuapishwa? Wakati kuna watu CV zao wanajaza page 20 Ila wako pale mlimani wanakula vumbi.
Vyeo hivi watu wanapeana wakiwa bar sinza Zuhura Yunus anachapisha tu
 
1. Connection
2. CCM
3. Kujipendekeza.
4. Kamlete.
Unakumbuka yule dogo wa degree moja akapewa ukurugenzi TPDC na akatumbuliwa kabla ya kuapishwa? Wakati kuna watu CV zao wanajaza page 20 Ila wako pale mlimani wanakula vumbi.
Vyeo hivi watu wanapeana wakiwa bar sinza Zuhura Yunus anachapisha tu
 
Mavumbi yabakie Vijijini kuhakikisha passability tuu ila isiwe focus ya Taasisi..

Pili barabara ambazo ni zaidi ya 40 km zichukuliwe na Tanroads
 
Akili zetu zimeganda na uwezo wetu hafifu. NI WAOGA MNO WA MABADILIKO HATA MARAIS NI WAOGA WA KATIBA MPYA.
 
Tatizo wanataka mivyeo tu lakini utatuzi wa changamoto za watafuta huduma kwa spidi na uzuri na customer care zero kabisa

Ubunifu na kwenda na wakati sifuri

Kuna wakuu wa idara ukimpa hata komputa achape sentence moja hawezi anadonoa keyboard kama kuku anayetafuta punje ingine ya kudonoa iko wapi.o

Utasikia as kuchapa sio kazi yangu ya secretary tumekuwa tukifanya hivyo toka enzi za Nyerere bosi hachapi chochote!!!! Kijana wewe.Wana vichwa vigumu mno kubadilika wanadhani dunia imesimama iko kule kule walikoanzia Miaka hiyo.kazi
 
Hivi vyeo ni ajili ya shukrani kwa makada watiifu ndiyo maana hakuna ufanisi wowote
 
wanapeana ulaji huwajui ccm ww?
 
Wengi hamko exposed na modern organization world, hamna extra mile mko too authoritative kuliko ile expected sense of delivery, hamna ownership na hamna uwezo wa kutengeneza stratergies ambazo zinazaa matunda ya papo kwa hapo. Hongera sana Mh. Rais na team yako kwa kuliona hili vizuri. Nchi yetu itasonga mbele sasa.
 

Mkuu YEHODAYA Umeongea Vema Sana…
Ila Kuna Mahali naomba Ufafanuzi,
Mfano Umesema Mhasibu amekaa Miaka 10Uhasibu sasa unamuhamishia Wapi ili apate Skills Zingine? Huko si watasema Hajasomea Kazi Ile?Say Umemuhamishia Ugavi au HR?

AU Mhandisi amefanya Uhandisi Kama Mkuu wa Idara for 10yrs,Then Unamuhamishia Say Ugavi au Masoko …

Sasa huko Si watasema Hajasomea mambo hayo na Kuanza Ku mu undermine? Kuwa wameletewa Mkuu wa Idara Mhandisi lakini Sio Mtu wa Masoko?
Pia Kumbuka Kuna Scheme of service…Muundo katika Ukuaji ambao Ndio unaeleza Mkuu wa Idara Flani awe na Sifa Zipi…Hili lipo sana Serikalini.
Nini Mawazo yako?
 
Ni kweli kabisa Mkuu.
Sekta binafsi kuna watu makini na wenye weledi usio na shaka.
Hats hivyo kazi/Ajira/teuzi za Serikalini ni za Wananchi wote.
 
Kifupi kuvunja hiyo vicious circle yenye too much specialization ya Serikali acha kazi join private sector ujenge uwezo utashangaa

Ukienda ukipewa idara yeyote waweza imudu barabara sema private sector areas kubwa zinazofanya watu wawe competent wanajikita kwenye customer care,kuongeza masoko,kuongeza mapato ya taasisi na kujenga image nzuri ya taasisi ndani na nje ,kasi ya utendaji kazi na ubunifu

Wafanyakazi Serikalini wanachoangalia ni mishahara tu inayoingia mwisho wa mwezi hayo mengine yote hawajali.Mfano mkandarasi waweza kuwa kila kitu kiko vizuri unapeleka invoice kwa mhasibu malipo atalipa siku akijisikia hajali kuwa mkataba una penalty malipo yakichelewa no.Sekta binafsi wote mnafanya kazi kama team kuhakikisha vyote hivyo vinatimia

Ndio maana mtu akitoka private Sekta aweza kuendesha taasisi ya umma vizuri kuliko wa ndani mfano ni National Housing ,TBC,CRDB,Tanesco no hata kama hakusomea kinachofanywa na hiyo taasisi ! Hata iwe ya umeme ukapeleka HR

Ukishakuwa private ukaenda serikalini utashangaza watu utendaji wako

Kukaa sana kazi serikalini kunadumaza akili unakuwa mweupe kichwani

Mfano unaenda afisa Madini kazi yake kusaini leseni tu za Madini ana Miaka 20 kitengo cha leseni hapo hakuna mtaalamu wa Madini.Elimu yote inakufa!!
 
Uko sahihi mtu akitoka private sector ni fast learner kwanza itachukua siku maximum tatu tu kujua taasisi kuna shida gani kwa sababu anakuwa na KPI yaani key performance indicators za taasisi kama hiyo bila hata kumpa atakuwa nazo akipitia kimoja baada ya kingine atajua shida iko wapi na kuweka modern strategy za how to turn around the situation.

Serikalini Unapiga simu tu ofisini haipokelewi nusu saa ukiuliza nilikuwa nakunywa chai!! Samahani !!! Aisee bull shitt!! Yaani hapo anajiona ndie kiboko kwenye customer care.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…