Je, Taasisi za Serikali hazina watumishi wenye Sifa hadi Wakurugenzi Wakuu Wateuliwe toka Nje ya Mfumo?

Inaelekea mleta mada anachukulia waajiriwa walio nje ya mfumo wa ajira ya serikali kama wageni au watu duni. Hili siyo sahihi. Na wao ni watanzania, na ni walipa Kodi. Kama wakiwa na vigezo stahiki wakaajiriwa tatizo nini?

Kufanya 'recycling' ya waajiriwa hao hao ambao kimsingi ni 'deadwoods' hakuwezi kufikisha nchi popote.

Afterall, mifumo ya utendaji kazi ya serikali, haiwapi fursa waajiriwa wake kujifunza, kupata uzoefu na kuwa mahiri ktk maeneo ya ushindani, uendeshaji na uongozi wa biashara wa kisasa. Hii ni kwa sabb ya ukiritimba unaotokana na utitiri wa kanuni, taratibu, urasimu, miongozo, maagizo, makatazo, nk vinavyosababisha waajiriwa kukosa ubunifu!!!

Chukulia mfano wa MD wa TPDC ambaye kimsingi ni zao la private sector.. Ukiangalia background yake kutokana na maelezo yake mwenyewe (hapo chini), siyo rahisi kupata mtu wa viwango vyake kutoka kwenye manispaa, halmashauri, Tamisemi, nk..
 
Ni mwendelezo wa kuwanyanyasa watumishi wa umma, kuwaona hawafai ndo maana kupanda mishahara na madaraja imebaki kuwa ndoto.........kuna watu kibao wana PhD ndani ya serikali, wote hao hawawezi kuongoza MSD?
 
Thr same reasons watu wanataka kuibadili CCM .
 
Miaka ya nyuma mfumo wa uteuzi ulikuwa kwa kupanda ngazi moja baada ya nyingine kutokana na utendaji wa mtumishi. Mfano Mte WEO [emoji3591] Afisa Tarafa [emoji3591] DAS [emoji3591] DC [emoji3591] RC etc... Pia Afisa Misitu Tarafa [emoji3591] afisa Misitu Wilaya [emoji3591] Afisa Maliasili (mkuu wa Idara) [emoji3591] DED etc mfumo huu ulifanya watumishi kukomaa kwenye kuchapa kazi kwani anajua atapanda ngazi. Unfortunately awamu ya tano ikauchimbia kaburi mfumo huu.
 
Tukitaka real changes na mawazo mapya hii ndiyo dawa pekee...
 
Kuingiza mawazo mapya ni lazima kutafuta mabosi kutoka nje ya mfumo uliopo vinginevyo taasisi haiwezi songa itakuwa ya kizamani ya enzi za mawe
Huyo Mkurugenzi mwenye mawazo mapya atawafanya watu wawe wapya? Mungu hawezi wabadirisha watu, kila mtu kampa free will.
 
Huyo Mkurugenzi mwenye mawazo mapya atawafanya watu wawe wapya? Mungu hawezi wabadirisha watu, kila mtu kampa free will.
Angalia kampuni zote za Serikali zilizobinafsishwa kuanzia CRDB ,NBC NMB,Breweries,kilimanjaro hotel,New Africa walikuja wazungu watatu tu mkurugenzi mkuu,Mkuu wa fedha na mkuu wa operations chini wamebaki waswahili wale wale hadi leo!!!

Unaona hadi leo zilivyo vizuri .CEO toka private sector akija ni mawili tu huwezi kuendana kasi ya kazi na utendaji andika barua ondoka shika chako sepa

Hana cha kubembelezana. Mikataba ya ajira iko wazi ukishindwa mawili achia ngazi au achishwa unalipwa chako kisheria katafute maisha huko kwingine watakokuendekeza kudeka kwako na nyodo zako za free will.Sio kesi wanaajiri damu mpya Wewe nenda ka practice hiyo free will. Yako huko uendako

Serikalini na taasisi za umma kuna kuleana mno na kubembelezana ndio maana mambo hayaendi angalau Magufuli alijitahidi kutumia private sector approach kuendesha Serikali nidhamu ya utendaji i na spidi lianza kurudi karibu kabisa kulingana na utendaji wa sekta binafsi.Ilikuwa almost sawa na utendaji wa private sector karibu maeneo yote


Approach ile ya Magufuli kwa msiojua ndivyo private sekta inavyofanya kazi.Hu perform off you go.Angalia CEO wa nchi alivyokuwa Magufuli akachukua approach ya utendaji kazi wa private sector mbona utendaji ulipanda ofisi za umma ukienda unahudumiwa chapchap na kwa heshima kubwa!! Magufuli alichofanya kidogo tu ali.copy approach ya private sector akapeleka serikalini

Sasa wewe na hiyo free will yako kajiajiri ukadeke huko na free will yako

Naapa ningekuwa CEO wa hapo ulipo ndani ya wiki ningekula sahani moja na wewe hadi kieleweke ningehakikisha unafunga virago kadekee huko kwenu ulikozaliwa

Binadamu kawaida wengi hawapendi kazi ukiwemo wewe private sector hu force mtu afanye kazi hakuna kubembelezana inahitajika nguvu ya ziada kukufanya ufanye kazi hataki ondoka ndio dawa yako ukishindikana
 
Uko sahihi
 
MIMI NASHAURI BADALA YA KUTEUA NAFASI HIZO ZITANGAZWE WATU WENYE SIFA WATAOMBA MCHUJO UTAFANYIKA ATAKAE KUWA NA VIGEZO NDIO ATEULIWE
Mawazo mazuri sana..sema shida hii nchi imeendekeza siasa uchwara...hizo nafasi huteuliwa wale chawa pro kama shukrani..hapo hakuna ufanisi zaidi ya utendaji mbovu..wakusifu na kuabudu ili kulinda matumbo yao.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mawazo mazuri sana..sema shida hii nchi imeendekeza siasa uchwara...hizo nafasi huteuliwa wale chawa pro kama shukrani..hapo hakuna ufanisi zaidi ya utendaji mbovu..wakusifu na kuabudu ili kulinda matumbo yao.

#MaendeleoHayanaChama
Mabadiliko muhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…