Je, tatizo la Stroke linaweza kupona?

Je, tatizo la Stroke linaweza kupona?

Wakuu jana baada ya kurudi home nilivyotoka uwanjani taifa nilimkuta mzee wangu hawezi kutembea yaani upande wa kushoto haufanyi kazi nilipata maumivu mara mbili yaani nilifungwa kwenye timu na narudi home nakuta majanga je Stroke inaweza kupona maana jana nilifika kituo cha afya ili apime kipimo cha CitiScan majibu yakaja kuwa amepata damage upande wa ubongo hapa naongea huku natamani kulia mkono na mguu wake havifanyi kazi naomba kujua dawa au matibabu ya haraka yanayoweza kumfanya harudi katika Hali yake ya kawaida
Pole sana ndugu yangu, naamini baba atapona arudi katika hali yake ya kawaida.
 
Baba yangu mkubwa alipona, ila mzee wangu alifariki 24 hrs baada ya kupata stroke, muwahishe hospital
Ni kweli, inategemea na aina ya stroke. Kwa ile ya hemorraghic, ambapo mishipa ya damu inayosupply kwenye ubongo inapasuka/kuvuja hupata kifo cha haraka bila ya matibabu na kama akipona basi prognosis huwa si nzuri.

Thus why hospitali hufanya kipimo cha CT scan ili kuitofautisha na ile ya ischemic, kwa sababu matibabu yao huwa ni tofauti.
 
Kwa niliowaona directly, wote ni mitishamba na maombi maana kwa maeneo ya uswazi. Wengi hawana pesa za kumudu gharama za hospitali zaidi ya kutegemea hizo njia mkuu

Pole pia brother, Mungu amsaidie mzee arudi katika hali yake
 
Wakuu jana baada ya kurudi home nilivyotoka uwanjani taifa nilimkuta mzee wangu hawezi kutembea yaani upande wa kushoto haufanyi kazi nilipata maumivu mara mbili yaani nilifungwa kwenye timu na narudi home nakuta majanga je Stroke inaweza kupona maana jana nilifika kituo cha afya ili apime kipimo cha CitiScan majibu yakaja kuwa amepata damage upande wa ubongo hapa naongea huku natamani kulia mkono na mguu wake havifanyi kazi naomba kujua dawa au matibabu ya haraka yanayoweza kumfanya harudi katika Hali yake ya kawaida
Pole, mkimuwahi anaweza kupona.
 
Hii nakupa kutokana na uzoefu mkuu
Mwaka 2019 nilimuuguza mama akiwa na umri karibu na mzee wako ye alikuwa 65 kwa ugonjwa huo huo na Sasa amepona yuko sawa akiwa na 70 yake
Nilimpeleka regency wakampa dawa ya dharula Kisha Dr kisanga anakanipa number ya Dr Njenje yuko hapo muhimbili
Jamaa Wana hospital Yao pale nje ya muhimbili kama unaenda mbele kidogo ratiba zao huwa ni asubuhi na mapema sana
Jamaa akanishauri nikaenda kule kinondoni kwa wachina kufanya scan ikaonesha athari
Nikarejea akaniandika dawa mbili ambazo gharama ilifikia kama 2000000
Nikaenda pale Robby one kariakoo nikawa nazinunua kwa mafungu anameza hadi akawa sawa
Angalizo dogo
Jitahidi utumie private hospital kama hao na wale wachina wa kinondoni ili usikawie sana na mgonjwa asichoke na abadani usitumie mitishamba au dawa za asili zinaweza kufanya tatizo liwe kubwa zaidi
Mwisho naamini mzee atakuwa sawa sana
Awe anapata mda wa kupumzika na sio Kila saa kumuuliza unajisikiaje
 
Back
Top Bottom