Je, Tundu Lissu anazo sifa za kuwa Rais wa Tanzania?

Je, Tundu Lissu anazo sifa za kuwa Rais wa Tanzania?

hana sifa stahiki kwa nafasi hiyo maoni yangu na mtazamo wangu.
si muaminifu,
si mzalendo, uzalendo wake wa mashaka.
si mstahimilivu
si muungwana
ana majivuno na dharau kupindukia,
amepungukiwa hekima na Busara,
si mtarabibu wala mstaarabu,
ni mbishi asie na utii,
hana mipango bali lawama,
haaminiki kitaifa bali ng'ambo kwa watwana,
ana uchu na tamaa mno,
ni mbinafsi hatari,
ni mpenda fujo sana,
ana chuki na wanaotofautiana nae kimtazamo,
ni mjeuri mwenye elimu
ana hasira iliyofichika.

nadhani Mbowe anafaa zaidi.
ni mstahimilivu,
Mzalendo asiye na shaka,
si mbishi,
ni mtulivu, mwenye hekima na Busara
hajivuni na wala haringi,
muongea kwa utaratibu na ustaarbu,
Hatukani wala kukejeli mtu,
Hana chuki wala habagui wenye tofauti na mtazamo wake.
si mbinafsi.
Anaaminika kitaifa na kimataifa
Jamaa ni muungwana sana,


nakuja kumalizia ngoja nipande daladala kwanza...........
Hata Mimi nakubali sana kuwa Mbowe anafaa sana kwenye uongozi wa juu na ndiyo sababu chama chake kimeweza ku survive hata katika nyakati ngumu wakati wote. Yupo resilient na anajua ku manage anger. Tatizo kubwa la hao ndugu zetu ni nepotism...Kwenye chama chake ameonyesha hili wazi wazi. Na sijui kwanini hao ndugu wa eneo Hilo wanashindwa kuficha hiyo tabia ya nepotism ya hali ya juu
 
Wanazo zote na za ziada ndio maana uchaguzi wa mwaka tulimshauri Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Ila kwa uchaguzi wa 2025, niliwaomba Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! hivyo iwapo CCM itamsimamisha mgombea Mwanamke, TL asigombee maana itakuwa ni aibu kushindwa na Mwanamke!.

Unless kama sauti hii ni yake YEYE, Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke then TL agombee, wapambane!.

P
Kwenye free & fair election CCM haijawahi shinda uchaguzi.." Mtoto wa Karume(2023)
 
Tatizo kubwa la hao ndugu zetu ni nepotism...Kwenye chama chake ameonyesha hili wazi wazi. Na sijui kwanini hao ndugu wa eneo Hilo wanashindwa kuficha hiyo tabia ya nepotism ya hali ya juu
Unaweza ukatupa mfano wa ukabila CHADEMA? Kila chama kina base yake na strongholds na CHADEMA base yake kubwa ilikua kaskazini.

But chama kimekuwa Sasa kilifika stage kikaongoza majiji yote makubwa Arusha, Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya imebakia Dodoma tu alafu bado unakazana kusema ni cha wachagga?

Toka huko kwenye ukabila, in fact siku hizi CHADEMA inakubalika zaidi nyanda za juu kusini kuliko hata huko Uchaggani.
 
Ukiuchukulia urais kama tasisi inayoongozwa na watu wenye uwezo na sifa tofauti tofauti, na siyo Mali ya mtu mmoja na familia yake,Lissu anazo sifa za kuwa Raisi.

Urais ukichukuliwa kama mali ya mtu ndio yanatokea kama ya yule jamaa yakutokushaurika na ukimshauri ndio umeharibu kabisaa.
 
hana sifa stahiki kwa nafasi hiyo maoni yangu na mtazamo wangu.
si muaminifu,
si mzalendo, uzalendo wake wa mashaka.
si mstahimilivu
si muungwana
ana majivuno na dharau kupindukia,
amepungukiwa hekima na Busara,
si mtarabibu wala mstaarabu,
ni mbishi asie na utii,
hana mipango bali lawama,
haaminiki kitaifa bali ng'ambo kwa watwana,
ana uchu na tamaa mno,
ni mbinafsi hatari,
ni mpenda fujo sana,
ana chuki na wanaotofautiana nae kimtazamo,
ni mjeuri mwenye elimu
ana hasira iliyofichika.

nadhani Mbowe anafaa zaidi.
ni mstahimilivu,
Mzalendo asiye na shaka,
si mbishi,
ni mtulivu, mwenye hekima na Busara
hajivuni na wala haringi,
muongea kwa utaratibu na ustaarbu,
Hatukani wala kukejeli mtu,
Hana chuki wala habagui wenye tofauti na mtazamo wake.
si mbinafsi.
Anaaminika kitaifa na kimataifa
Jamaa ni muungwana sana,


nakuja kumalizia ngoja nipande daladala kwanza...........
Hisia za chuki zimetawala san hii reply yako!! Tunaheshim mawazo yako iwe ya kijinga ama ya msingi
 
Emotional resilience,hii ndio sifa kuu ya Kiongozi mzuri,hutokuja sikia akipatuka Wala kuropoka hovyo Wala ku act Kwa jazba.
Hujatoa jibu la msingi, kupayuka maan yake nn? Yawezekana mtu anaongea mamb ya kwel kbs na yeny mantiki but approaching ikatafsiriwa tofaut. Pia LISSU sio mropokaji tatizo lenu mnataka mtu akosoe huku anapata mafuta na kuwalambisha asali huku anawakosoa!! LISSU hawez mung'unya maneno penye ukwel anapiga mulemule bila kuremba maneno, kitu ambacho wanaccm hawapendi kbs!!
 
Hisia za chuki zimetawala san hii reply yako!! Tunaheshim mawazo yako iwe ya kijinga ama ya msingi
Yes!
na wewe si utulie tu na hisia zako za upendo kwa yeyote kulingana na hoja ya mtoa bandiko, whether ni wa kinafiki ama la, upendo wa kweli ama sio wa kweli na hakika nina uheshimu sana ujinga, upumbavu ama uwerevu wako, na kwakweli huo ni uhuru wako na haki yako kua hivyo ulivyo right?!🤓
 
Tunataka Rais mzalendo; mwenye uwezo wa kukemea mafisadi hadharani, atakayesimamia rasilimali za nchi Kwa wivu mkubwa na mwenye element za udikteta kiasi ili majizi yote yatapike pesa na kuzirejesha kwenye miundo mbinu uchumi urudi Kwa maskini. Huyo si mwingine Kwa sasa ni Mazalendo Tundu Lissu.
 
Kwenye kitabu changu kipya kiitwacho, 'Near Miss' nita explore jinsi ambavyo Mbarawa, Makamba na Mwigulu 'walikaribia kuupata uraisi, ila wakaukosa'...
 
Hakuna sifa kuu kwa kiongozi wa nchi kuwa nayo inayozidi UZALENDO kwa nchi yake.

Kwa hiyo napendekeza uanzie kwenye sifa hiyo.

Kiongozi wa nchi ni muhimu awe na dira inayomwongoza ni wapi nchi anayoiongoza iende na kwa mipango gani na wakati maalum. Siyo maswala ya kubahati sha tu

Kiongozi ni lazima awe na imani na wananchi wake, kwamba hawa watu ndio walio na uwezo wa kujiletea maendeleo na kubadilisha hali duni ya maisha yao. Hayo mengi sana tunayopigiwa kelele kuhusu uwekezaji, hiyo ni kuongezea tu juu ya juhudi zetu wenyewe

Kiongozi ni atakayeheshimu na kujali mali za taifa hili. Asiyekuwa na uvumilivu kabisa katika kutapanya mali za nchi yetu bila ya mpango maalum. Madini yote sasa karibu yamesombwa, lakini ukiuliza ni miradi ipi iliyobadilishwa na madini hayo, hupati jibu hata moja.

Zipo sifa nyingi..., kiongozi anayeweza kujieleza na watu wakaelewa anachozungumzia kwa lugha inayoeleweka; n.k.,
Mara nyingi kama sio mara zote hakuna Rais asiyependa kupigiwa makofi na kusifiwa ndani na nje ya nchi yake. kwa maana nyingine hakuna Rais asiyependa kufanya vizuri. Shida zinazowapata viongozi wengi zinatokana na wale watu/taasisi/nchi/kabila/dini waliomzunguuka/wanaomsaidia , wale waliomsaidia kuipata nafasi na aina ya watu wanaomsifia na sababu zao za kumsifia.
 
Kama form four failure anaweza kuwa rais basi Lissu ni above next level

Sent using Jamii Forums mobile app
Mara nyingi natamani potential candidate akipata nafasi hata ya dk 2 za kuzungumza na wananchi awaambie nini angefanya/atafanya kama angekuwa/atakuwa Rais wa nchi hii. Shida yetu kubwa kuliko zote sio uhaba wa demokrasia bali uchumi mdogo, huduma mbovu na ukosefu wa huduma kabisa. Kule nchi za Uarabuni na Uchina hakuna demokrasia pana lakini hali za maisha na uchumi ni kimbilio kwa watu wa nchi nyingine kutafuta huduma, ajira, mikopo, elimu, afya na starehe. Sitamani kumsikia mgombea anayehubiri demokrasia saaaana kama ya Magharibi na kuacha kutuambia atafanya nini juu ya wezi wa mali ya umma, maji, uchukuzi, elimu, ajira, umeme, gharama za maisha, chakula, hali ya hewa, masoko, mitaji, technolojia, nk. Nataka mtu aeleze polepole kwa kituo nimwelewe bila kunifokea au kulaumu na kubeza wengine.
 
Tundu Lissu anaweza akafanya kwa ufanisi kazi za kutumwa lakini siyo kuwa mwamuzi wa mwisho.

Ana element za Ki-Magufuli kujisikia kuwa yeye ndiyo ana akili kuliko wengine na ni bora kuliko wengine. Hizo ndiyo typical characteristics za ma DIKTETA. Nadhani hata risasi alizopigwa na Magufuli zilitokana na kwamba fuse zinazofanana zili react zilipokutana.

Urais inahitaji mtu humble, mwenye akili iliyotulia, anayefikiria jambo mara 2, anayetafuta ushauri kwa wengine, asiye mropokaji, anaye muogopa Mungu kwa vitendo na asiyependa dhuluma.

Samia hadi 2030
Mkuu Lissu ana uwezo ambao Undisputable.
Tofauti yake na Magufuli Lissu ni mwenye uelewa mkubwa sana na anajali haki na utawala bora.
 
Back
Top Bottom