Mara nyingi natamani potential candidate akipata nafasi hata ya dk 2 za kuzungumza na wananchi awaambie nini angefanya/atafanya kama angekuwa/atakuwa Rais wa nchi hii. Shida yetu kubwa kuliko zote sio uhaba wa demokrasia bali uchumi mdogo, huduma mbovu na ukosefu wa huduma kabisa. Kule nchi za Uarabuni na Uchina hakuna demokrasia pana lakini hali za maisha na uchumi ni kimbilio kwa watu wa nchi nyingine kutafuta huduma, ajira, mikopo, elimu, afya na starehe. Sitamani kumsikia mgombea anayehubiri demokrasia saaaana kama ya Magharibi na kuacha kutuambia atafanya nini juu ya wezi wa mali ya umma, maji, uchukuzi, elimu, ajira, umeme, gharama za maisha, chakula, hali ya hewa, masoko, mitaji, technolojia, nk. Nataka mtu aeleze polepole kwa kituo nimwelewe bila kunifokea au kulaumu na kubeza wengine.