Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Kama Samia amekuwa Rais hata Rose Mhando anaweza sembuse Lissu?Rais wa nchi yetu awe na sifa zipi?
Je, ni nani anazo sifa nyingi za kuwa Rais ajae? Je, Tundu Lissu anazo sifa hizo pia?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama Samia amekuwa Rais hata Rose Mhando anaweza sembuse Lissu?Rais wa nchi yetu awe na sifa zipi?
Je, ni nani anazo sifa nyingi za kuwa Rais ajae? Je, Tundu Lissu anazo sifa hizo pia?
Wanahakikisha kuwa huwezi kupata fedha za kigeni (USD/Euro) kwakuwa wao ndio wanapanga ubora na bei ya pamba, korosho, kahawa, chai, dhahabu yako. Hivyo utalazimika kwenda kuwakopa wao kwa riba kubwa. Muda wote utakuwa unahangaika namna ya kuingia kwenye masoko yao kwa bei yao na kulipa madeni yao. Hii ndio sababu Afrika yote iko hoi hata zile nchi zenye Katiba mpya na vyama vipya madarakani.Ni kweli matatizo yetu sio katiba mpya. Umekiri kwamba tunahitaji viongozi imara na waadilifu, najaribu kuwaza kwa sauti huenda pia hii katiba inatoa huo mwanya wa kupata viongozi wa siyo imara na waadilifu, hapo unaonaje?
Je wewe kwa upande wako Unadhani nini kinazuia kupata hiyo dola yenye nguvu ya kubadilisha hali ya mambo ikiwemo kupambana na hiyo mifumo mibaya ya dunia ya manunuzi?
Je hauoni kwamba kuwa na dola yenye uwezo wa kupambana na mifumo mibaya ya manunuzi ya dunia ni sawa na kuwa against na wakubwa wa dunia?
Na kwanini wanasiasa wa afrika wanan'gan'gania kushika dola hali yakuwa wanafahamu fika kuwa hawawezi kubadili hali ya mambo?
Mwisho nini kifanyike kuipata dola ya aina hiyo?
Funguka mkuu tujifunze.
Majibu haya nashauri uyajaze mwenyewe, Mkuu. Mimi nimeisha malizia.Aliepo ni presidential material? Na aliesukumizwa kua Rais alikua presidential material?
Massive escapin'Majibu haya nashauri uyajaze mwenyewe, Mkuu. Mimi nimeisha malizia.
🙄🙄🙄🙄hana sifa stahiki kwa nafasi hiyo maoni yangu na mtazamo wangu.
si muaminifu,
si mzalendo, uzalendo wake wa mashaka.
si mstahimilivu
si muungwana
ana majivuno na dharau kupindukia,
amepungukiwa hekima na Busara,
si mtarabibu wala mstaarabu,
ni mbishi asie na utii,
hana mipango bali lawama,
haaminiki kitaifa bali ng'ambo kwa watwana,
ana uchu na tamaa mno,
ni mbinafsi hatari,
ni mpenda fujo sana,
ana chuki na wanaotofautiana nae kimtazamo,
ni mjeuri mwenye elimu
ana hasira iliyofichika.
nadhani Mbowe anafaa zaidi.
ni mstahimilivu,
Mzalendo asiye na shaka,
si mbishi,
ni mtulivu, mwenye hekima na Busara
hajivuni na wala haringi,
muongea kwa utaratibu na ustaarbu,
Hatukani wala kukejeli mtu,
Hana chuki wala habagui wenye tofauti na mtazamo wake.
si mbinafsi.
Anaaminika kitaifa na kimataifa
Jamaa ni muungwana sana,
nakuja kumalizia ngoja nipande daladala kwanza...........
Wanahakikisha kuwa huwezi kupata fedha za kigeni (USD/Euro) kwakuwa wao ndio wanapanga ubora na bei ya pamba, korosho, kahawa, chai, dhahabu yako. Hivyo utalazimika kwenda kuwakopa wao kwa riba kubwa. Muda wote utakuwa unahangaika namna ya kuingia kwenye masoko yao kwa bei yao na kulipa madeni yao.
kwani bandiko linamzungimzia nani 😳 ebo!🙄🙄🙄🙄
Umebeba kila neno linalo - denominate sifa ukampachika nalo Tundu Lissu..
It's a wisdom to think and analyse things rather than being judgemental..
Wewe ulitaka zipi?Ni zipi ipi (zipi) za ziada anazo TL?
Hakuna binaadam mwenye akili timamu asiyependa kuonekana na sifa anazoona yeye mwenyewe anazo na watu wengine wazitambue hivyo; kwa hiyo kumsifia kwa sifa hizo alizo nazo.Mara nyingi kama sio mara zote hakuna Rais asiyependa kupigiwa makofi na kusifiwa ndani na nje ya nchi yake. kwa maana nyingine hakuna Rais asiyependa kufanya vizuri. Shida zinazowapata viongozi wengi zinatokana na wale watu/taasisi/nchi/kabila/dini waliomzunguuka/wanaomsaidia , wale waliomsaidia kuipata nafasi na aina ya watu wanaomsifia na sababu zao za kumsifia.
Wewe ni 'Kadhi Mkuu 1', hakuna anayehoji hilo.Labda sifa ya kuwa mgombea wa kwanza kuwa mkimbizi, siyo urais.
EeeRais wa nchi yetu awe na sifa zipi?
Je, ni nani anazo sifa nyingi za kuwa Rais ajae? Je, Tundu Lissu anazo sifa hizo pia?
Kiongozi anaweza kuwazuia watu wasimsifu? Muhimu kwake kiongozi anaesifiwa ni kutafakari kwa kina ili kujua ni kwanini nani anamsifu sana kiasi hicho, baaasi. Yaani yule anaetoa sifa hizo ni lazima apekuliwe zaidi kuliko wengine ili kujua kama ni sifa tu au kuna kitu anataka/anaomba/anaiba/anataka kuiba. Vinginevyo kumsifu mtu sio kosa kama amekukuna kwelikweli.Hakuna binaadam mwenye akili timamu asiyependa kuonekana na sifa anazoona yeye mwenyewe anazo na watu wengine wazitambue hivyo; kwa hiyo kumsifia kwa sifa hizo alizo nazo.
Mtu anapokuwa kiongozi, akatafuta kusifiwa kwingi zaidi ya sifa alizo nazo hiyo ni dosari.
Hao watu wanaomzunguka na kumpa sifa hizo, hata asizokuwa nazo, na wengi (wote) wa watu hao wakiwa ni wateule wake, maana yake ni kwamba kiongozi huyo ni mpenda sifa tu, ndiyo maana watu hao kawaweka kwenye nafasi hizo alizowaweka kwa misingi ya kumsifia yeye.
Huyu ni kiongozi mbovu.
"Nyerere alikuwa mzalendo ila aliharibu hii nchi"?Mkuu kuongoza nchi kunahitaji vitu vingi zaidi ya uzalendo,
Nyerere alikuwa mzalendo ila aliharibu hii nchi,
Inahitaji kumchek mtu mwenye kuliunganisha taifa, kuunganisha taifa, kuwa na busara, na kuwa na sera nzuri hususanu wakati huu ambapo tunahitaji zidi kujikomboa kiuchumi tunahitaji kiongozi mwenye sera nzuri za uchumi,
Bahati mbaya kwa Lissu sijawahi sikia akiongelea uchumi, yeye yupo more political based
"Kiongozi anaweza kuwazuia watu wasimsifu"? Sana.Kiongozi anaweza kuwazuia watu wasimsifu? Muhimu kwake kiongozi anaesifiwa ni kutafakari kwa kina ili kujua ni kwanini nani anamsifu sana kiasi hicho, baaasi. Yaani yule anaetoa sifa hizo ni lazima apekuliwe zaidi kuliko wengine ili kujua kama ni sifa tu au kuna kitu anataka/anaomba/anaiba/anataka kuiba. Vinginevyo kumsifu mtu sio kosa kama amekukuna kwelikweli.
Kuna watu walijaribu kuwabwekea wapanga bei lakini hawakufua dafu, miongoni mwao wamo, Mwl. Nyerere, Magufuli, Nkrumah, Gadafi, Mugabe, nk. Hali ni ngumu kweli kweli. Mzee Nyerere ilimlazimu kuachia ngazi (kung'atuka) bila kupenda, nchi ilifisika kwa vikwazo.Its so bad. Anyway ngoja tuendelee kuiota Afrika yenye neema, hata kama itakuwa miaka 500 ijayo.
Maana kutoka kwenye hayo makucha ya hao wapanga bei za mazao na dhahabu zetu kunahitaji sacrifice.
Ila kwa generation hii ya viongozi wa Afrika sidhani kama Afrika itaweza kujinasua kwenye hayo makucha.
Kupitia sera zake mbovu za Ujamaa nyerere aliharibu uchumi wa nchi like forever"Nyerere alikuwa mzalendo ila aliharibu hii nchi"?
Hiki ni kitu gani unachokiongelea hapa hasa. Unaelewa ulichokiandika?
Ukubali kuwa alikuwa 'mzalendo', halafu kwa sababu unaziozifahamu wewe, aamue kuiharibu nchi! Hii inaleta mantiki yoyote?
Haya ndiyo matokeo ya kukariri tu mambo unayosikia yakisemwa na wewe kuyabeba bila ya kuyachambua akilini mwako vizuri.
Sasa kwa kuwa enzi hizi ni za uwekezaji, kama unavyoandika, ungesifu sana kama Nyerere angekuwa kafanya uwekezaji kama unavyohimizwa leo?
Haya, leo tunafanya uwekezaji, kama mtindo wa sasa unavyohimiza, umeiona nafuu yoyote ya ziada?
Mkapa na Kikwete wamefanya sana habari ya uwekezaji; lakini nchi bado ndiyo inakwama zaidi kwenye tope.
Sasa usinielewe kuwa sitaki uwekezaji, lakini unapokuwa kiongozi mzalendo, inakubidi uelewe ni yapi ya kufanya ili uwekezaji huyo unufaishe jamii unayoiongoza.