Haya yote uliyoandika hapa ni ujinga, na situmii neno hilo kama tusi, ninalitumia kwa maana yake halisi.
Kama siyo ujinga, basi utakuwa unayaandika haya kwa kurudia rudia yale yaliyosemwa na wapotoshaji na wewe sasa unayaimba hapa kama kasuku tu, asiyejua anafanya nini.
Kwa mfano:
Huna uwezo wowote wa kuelezea "ubovu wa sera za ujamaa" zilizosababisha "uharibifu wa nchi, 'like forever'".
Kutokana na uandishi wako inaonyesha wewe ni hawa wa siku hizi msiokuwa na nyuma wala mbele katika kuelewa mswala ya kidunia.
Kama ujamaa wa Nyerere" umeweza kuharibu nchi, like forever", wewew hata katika hili tu huwezi kuona ubovu wa akili yako katika kuyang'ang'ania haya ya miaka chungu nzima iliyopita? Umeuona mfano upi wa nchi ya mfumo wa kibeberu (unakotoa jina lako), hapa Afrika na kwingieko ambako 'ujamaa wa Nyerere' haukuwagusa, na sasa ni mfano mzuri wa kuigwa?
Sitapoteza muda mwingi na kukujibu upuuzi mwingine ulioandika huko chini.
Niakupa ushauri tu, achana na tabia za kukaririshwa mambo. Umejaaliwa akili, zitumie kufikiri na kupata majibu sahihi ya maswala unayotakiwa kuyakariri kama kasuku.