Ungetoa mfano wa kitu kipya alichokibuni Samia mbali ya vile anavyoendeleza vya Magufuli, ungekuwa kidogo umetoa mwanga katika nadharia yako hiyo ya "total football".Rais Samia ni muumini wa total football, JPM alikuwa muunini wa kwenda na vipandevipande. JPM alikuwa anasimamisha mambo mengine ili kufanikisha mambo mengine haraaka, lakini Mama Samia anafanikisha mambo yote kwa wakati mmoja polepole. Wakati wa JPM tuliona kuwa kipaumbele chake kilikuwa ni ujenzi, ujenzi, ujenzi, ujenzi, ujenzi na kusimamisha mambo mengine kwanza. Tuliona nchi kama vile imetekwa na jeshi, kila barabara kila mtaa, kila site ya ujenzi, kila lindo kulikuwa na wanajeshi/polisi. Polisi walikuwa anapita njia yoyote na upande wowote wa barabara bila kuzingatia alama za barabarani.
Hata kama nadharia hiyo ingekuwa kweli, kwa hali ya uchumi tuliyo nayo, 'impact' ya matokeo yake ingekuwa hakuna kabisa, kwa sababu bila f'focus' maalum kwa mambo machache kuyafanya kwa ufanisi na kwa haraka, tunabaki tunazungukia mlemle tu na vimiradi/matukio bila kuona lolote lililofanyika.
Binafsi, ningeridhika sana kuona mradi wa Bwawa la umeme, na SGR vikienda kwa haraka, kwa ufanisi na kukamilika katika muda uliopangwa. Sioni sababu ya kusambaza juhudi kila mahala kwa wakati mmoja na kuchukua muda mrefu kukamilisha, na mara nyingi kwa gharama kubwa, na hata kushindwa kabisa baadhi ya miradi kama hiyo.
Angalia Reli ya Mchina (SGR) hapo jirani ilivyokwenda kasi na kuisha kwa wakati; au ile barabara ya Express waliyojenga baada ya reli.
Utendaji wa aina ile ndio huleta mabadiliko ya haraka na unajenga uchumi kwa haraka.
Kuhusu hiyo aya ya kwanza juu ya Samia na uwezo wake wa kuongoza, ngoja niliache hilo kiporo.
Samia siyo kiongozi wa kutolea mfano kwa lolote, labda ujanjaujanja tu, ambao nao watu sasa wameubaini.
Mbaya zaidi ni hilo la Bandari na tabia yake ya kudhani waTanzania hawana uwezo wa kujiletea maendeleo wao wenyewe. Haya yanamfanya aonekane kuwa kiongozi wa hovyo kabisa kuliko wote.