Je, Tundu Lissu ashitukia biashara za Freeman Mbowe? Ahoji biashara gani haina TIN Number?

Je, Tundu Lissu ashitukia biashara za Freeman Mbowe? Ahoji biashara gani haina TIN Number?

Wakuu, Tundu Lissu alipofika Uwanja wa ndege, amehoji chanzo cha fedha kwa baadhi ya watu.
View attachment 3194290
Tundu Lissu amesema, "Ni muhimu tukajua, katika Mazingira ya Tanzania halisi hii, haya Mamilioni haya yanatokea wapi na ni salama kiasi gani? Kama mtu ana biashara Nchini au Nje ya Nchi, kuna biashara ambayo huwa haijulikani? Kuna Biashara isiyokuwa na TIN number, isiyokuwa na Leseni, isiyokuwa na jina isiyokuwa na Ofisi Mahali, isiyokuwa na Bank account? Ipo? Niambieni." Mwisho wa kumnukuu.

Je, haya maneno yanalenga Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe?

Sababu ndo huwa anasema ana biashara zake.

Kuna Kipindi Paul Makonda alishindwa kujua Mbowe anafanyabiasha gani hadi akahisi anafanya biashara za madawa ya kulevya.

Pia, soma:

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Polisi; ahojiwa na kuachiwa

Jamani tuache drama nchi yetu iko rehani kwasasa. Tofauti ya Mbowe na Lissu ni jinsi ya kuleta mageuzi lakini Lissu hajasema Mbowe ni mla rushwa . Mbowe na familia yake wana Hotel huko London ya mamilioni ya pound sasa ! Tusimuingize kwenye mambo ambayo si ya msingi mla rushwa ni Wenje sio Mbowe. Mbowe biashara zake na familia inasemekana ni $32M sasa jamaa aje kuhongwa na Abdul gari sio ukweli! .
 
Lissu nimekumbuka allvyokuwa akimwita Rais wa awamu fulani Dr Prof.......Mbowe awe mpole Lissu Ana slogan ya no retreat no surrender
 
kaondokoa nchini kabendera kaachia kitabu kikatawala jf, karudi nchini habari za kitabu zimekufa kana kwamba hazikuwepo na hata huyo waliomjali sana waliosema kapigwa risasi ikulu hawamkumbuki tena, sasa anatawala ( tundu lisu) tena jf, janja janja yote ina mwisho, Januari 20 D.Trump anaapishwa mwisho wa biden na usanii woote, najua mtasema inatusuhu nini lkn wiki 2 zijazo kutatikisika na huu usanii wote utaisha …
Ya mungu mengi tar20 huenda asifike au usifike au nisifike mwenyezimungu ana siri nzito kuhusu ya mbele yetu
 
kaondokoa nchini kabendera kaachia kitabu kikatawala jf, karudi nchini habari za kitabu zimekufa kana kwamba hazikuwepo na hata huyo waliomjali sana waliosema kapigwa risasi ikulu hawamkumbuki tena, sasa anatawala ( tundu lisu) tena jf, janja janja yote ina mwisho, Januari 20 D.Trump anaapishwa mwisho wa biden na usanii woote, najua mtasema inatusuhu nini lkn wiki 2 zijazo kutatikisika na huu usanii wote utaisha …
Usanii gani? Ni hivi akishinda Mbowe ndio chama kimekufa. Nani serious atapigia kura chadema tena?
 
kaondokoa nchini kabendera kaachia kitabu kikatawala jf, karudi nchini habari za kitabu zimekufa kana kwamba hazikuwepo na hata huyo waliomjali sana waliosema kapigwa risasi ikulu hawamkumbuki tena, sasa anatawala ( tundu lisu) tena jf, janja janja yote ina mwisho, Januari 20 D.Trump anaapishwa mwisho wa biden na usanii woote, najua mtasema inatusuhu nini lkn wiki 2 zijazo kutatikisika na huu usanii wote utaisha …
🎯🙏
 
Nimetoa mifano hapo juu nitajie wamiliki.

Labda kama mgeni jijini... Biashara nyingi bongo za wanasiasa wajanja wanatumia wahindi na waarabuil kama owners .

Tanzania nzima wahindi ndio wanaendesha biashara anonymous za wanasiasa wa kibongo na wao ndio wamiliki.

Nimekusanua mkuu...
🤔🤔🤔💭
 
Kwa hili Lissu ni mshamba sana,

Zipo Bislashara kibao wamiliki ni ghosts for a reason.

Mazingira yeyote ya kuweka biashara zako wazi ukiwa kwenye siasa ni kitafuta kujimaliza.

Wapo wengi sana duniani hawaonekani kwenye list yeyote ya legal business lakini ni matycoon.

Yeye hajawahi fanya biashara and he knows nothing about it.....

Atulie aombe michango achangiwe aache bla bla za kishamba.

Hashangai ni yeye tu anazungusha bakuli kuomba mia mia wenzake daily Dubai, Nairobi, Dar, US etc..

Wewe unaish kwa free meal ya special political asylum card bwana wacha kujilinganisha na kila mtu.
Biashara inayokulazimisha uwe ghost lazima uwe na uhalifu nyuma yake.
 
Biashara inayokulazimisha uwe ghost lazima uwe na uhalifu nyuma yake.
Sio lazima.
Inategemea na aspirations, plans and strategy.
Ghosting ni njia rahis ya kukwepa kupewa majina na wanasiasa wajinga wasiofikiri sawa sawa.

Lakini kuna issues za legal implications, sio kila owner anataka kuwa associated na mambo ya Kupambanishwa na serikali for anything whatsoever na hii imefanya wengine waogope kufanya biashara zao wenyewe badala yake wanawekeza kwenye kampuni kubwa zenye low returns .
 
Mbowe ni Dalali mkuu wa Siasa za nchi hii, akifuatiwa na yule dalali wa Zambarau 💖 aliemfukuza uanachama, akaanzisha saccos yake na yeye!
 
Chadema ni chama cha Kibepari.

Huyu jamaa hana chochote lakini anataka kutuaminisha kila mtu asieelewana nae ni fisadi na muwongo...

Tupo makini sana na watu wa namna hii.
Wampinge kwa hoja. Sisi tupo tunawasikiliza wote!
 
Mbowe anajua kuiba pesa za chadema
Mbowe anajua kutafuta pesa zipi? Angekuwa anajua kutafuta pesa asingeng’ang’ania uenyekiti atawale kifalume angeenda kupambana mitaani, Mbowe ni mwizi wa pesa za chadema
Katiba inamruhusu kugombea ,hakuna time limit ,Lissu ni mmoja wa waliotunga hiyo katiba.....Mbowe ameenza kusaidia chadema na lissu tangu akiwa ni mwanachama wa kawaida tu...Mbowe pesa anayo ,hatagemei CDM kusurvice ,Mbowe by nature ni mtu wa kupambania haki ,anaona viongozi aliowaamini wamemuangusha eg slaa ,zitto ,mashinji ,peter etc so kumuachia mtu chama ambaye no OYA OYA anaweza kukipiga BEI.
 
Biashara za siri za mbowe ni kuuza unga ndiyo maana makonda alimtaja kwenye list na biashara ya pili ya mbowe ni kuiba pesa za chadema kisha kuzitakatisha kwa kisingizio cha kujilipa madeni hewa
Unadhalilisha vyombo ya ulinzi na usalama ,yaani mbowe auze unga halafu hakamatwi? Yaani unaconclude kisa makonda kataja? Kwahiyo Makonda alivyotangaza kwamba wenye magari Dar waondoe "TINTED"(Tint) alikuwa sawa?(Ulikuwa unajua motive behind ya lile tamko?)

Unamdhalilisha pia CAG maana hivyo vitu ulivyoviona wewe ina maanisha CAG alivyoenda kugagua CDM havioni? Kama wewe layman wa accountancy umeviona vipi kwa wabobevu/waandamizi washindwe kuona?
 
Wakuu, Tundu Lissu alipofika Uwanja wa ndege, amehoji chanzo cha fedha kwa baadhi ya watu.
View attachment 3194290
Tundu Lissu amesema, "Ni muhimu tukajua, katika Mazingira ya Tanzania halisi hii, haya Mamilioni haya yanatokea wapi na ni salama kiasi gani? Kama mtu ana biashara Nchini au Nje ya Nchi, kuna biashara ambayo huwa haijulikani? Kuna Biashara isiyokuwa na TIN number, isiyokuwa na Leseni, isiyokuwa na jina isiyokuwa na Ofisi Mahali, isiyokuwa na Bank account? Ipo? Niambieni." Mwisho wa kumnukuu.

Je, haya maneno yanalenga Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe?

Sababu ndo huwa anasema ana biashara zake.

Kuna Kipindi Paul Makonda alishindwa kujua Mbowe anafanyabiasha gani hadi akahisi anafanya biashara za madawa ya kulevya.

Pia, soma:

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Dawa za Kulevya: Freeman Mbowe akamatwa na Polisi; ahojiwa na kuachiwa
Na Mbowe alipotajwa na Makonda ni Mropokaji Lissu huyu huyu alikuwa mmoja wa waliomtetea Mbowe. Leo eti nae anashangaa!
 
Back
Top Bottom