Hilo likiwezekana, basi litakuwa jambo jema sana kwa Tanzania . Na sioni ugumu maana katika siasa lolote linaweza kutokea na hii ni katika kujenga maridhiano ya kitaifa. Historia inaonesha kuwa hawa wawili yaani Tundu Lissu na Rais Samia Suluhu Hassan ni wazalendo wa kweli kunapokuja kuhusu kujenga taifa moja tofauti na uongozi wa CCM uliopita.
Toka maktaba:
28 November 2017
Nairobi, Kenya
Makamu wa Rais Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu .
17 Feb 2020
Samia Suluhu : "Napenda mawazo ya wapinzani, huwa wanajenga hoja vizuri, walini 'inspire' niingie siasa"
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefunguka kuhusiana na historia ya maisha yake ambapo ameeleza siri ya mafanikio na chanzo kilichomvutia kuingia kwenye siasa. Samia Suluhu anaona hoja za upinzani ni moto, zimejaa mantiki kuliko za mawaziri wa serikali ya CCM , hivyo walinivutia / inspire, mimi ni activist ... kuingia siasani baada ya kuona majibu na hoja za upande wetu (CCM) hazina uhalisia na hazijibu maswali ya wananchi ....