Je, Tundu Lissu atakutana na Rais Samia Suluhu Ubelgiji?

Je, Tundu Lissu atakutana na Rais Samia Suluhu Ubelgiji?

Protocal huwa kwa kawaida Rais huitisha kikao na watanzania wanaoishi kwenye nchi husika.. Watanzania kupitia Balozi hupewa mwaliko..

Tahadhari: huo sio mkutano wa Siasa au kusutana na kutafuta political mileage au mdahalo wa Urais..... ni Rais anaongea na Watanzania kuwaeleza hali halisi ya nyumbani na kusikiliza maoni yao...
Mwenzako Samia kashatengeneza Political Mileage na kafungulia magazeti na hii itakuwa ndio wimbo wake huko ulaya. Endelea kubwabwaja.
 
Kama Maza atahitaji kukutana na Lissu sawa, lakini awe tayari kutoa majibu ya sintofahamu nyingi
1. Shambulio lake kwa nini upelelezi hadi leo haujafanyika
2. Suala la Ugaidi wa Mbowe
3. Usalama wake - kwani anatamani kurudi nchini
4. Suala la katiba mpya
Haya ndio Maswala magumu yanafanya Wakuu wa Nchi wasikutane na Lissu.
 
Hilo likiwezekana, basi litakuwa jambo jema sana kwa Tanzania . Na sioni ugumu maana katika siasa lolote linaweza kutokea na hii ni katika kujenga maridhiano ya kitaifa. Historia inaonesha kuwa hawa wawili yaani Tundu Lissu na Rais Samia Suluhu Hassan ni wazalendo wa kweli kunapokuja kuhusu kujenga taifa moja tofauti na uongozi wa CCM uliopita.

Toka maktaba:
28 November 2017
Nairobi, Kenya

Makamu wa Rais Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu .

17 Feb 2020
Samia Suluhu : "Napenda mawazo ya wapinzani, huwa wanajenga hoja vizuri, walini 'inspire' niingie siasa"

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefunguka kuhusiana na historia ya maisha yake ambapo ameeleza siri ya mafanikio na chanzo kilichomvutia kuingia kwenye siasa. Samia Suluhu anaona hoja za upinzani ni moto, zimejaa mantiki kuliko za mawaziri wa serikali ya CCM , hivyo walinivutia / inspire, mimi ni activist ... kuingia siasani baada ya kuona majibu na hoja za upande wetu (CCM) hazina uhalisia na hazijibu maswali ya wananchi ....

Ila Mama Samia isingekuwa miccm inayomharibia alikuwa a Roho nzuri sana.
 
Ila Mama Samia isingekuwa miccm inayomharibia alikuwa a Roho nzuri sana.

Sana tu, ndiyo maana tunaona hatua zake Rais Samia Hassan za kujaribu kujinasua kutoka legacy ya utawala wa kimabavu wa awamu ya 5.

Ana mtihani mkubwa Rais Samia Hassan kwani kuna wahafidhina wanaomuabudu hayati mwendazake JPM hawataki kuona mkono wa kheri anaoanza kujaribu kutoa kwa watanzania wenzie wenye mawazo mbadala badala yake wanahamu kuona jinamizi la mabaya ya JPM yamnganganie pia kumuongezea uzito yamburuze na kumchelewesha.

Hii yote ni njama za gang la wahafidhina walioachwa yatima na JPM kumzuia Rais Samia Hassan kujibainisha kuwa yeye Rais Samia Hassan ajisimamie mwenyewe kuwa haafiki mabaya yote yaliyotendeka ktk awamu ya tano kwa kisingizio cha uzalendo feki na kutamani Tanzania mpya inayoshirikisha waTanzania wote bila kujali tofauti zao za kisiasa, mawazo na nia ya kuwa raia huru katika nchi yao.
 
Rais SSH hana chuki na mwenyekiti mwenza wa chama cha demokrasia na maendeleo, rais ameonyesha muelekeo mwema wa uhuru wa kutoa mawazo, uhuru wa vyombo vya habari na ulinzi wa wananchi
 
Mwenzako Samia kashatengeneza Political Mileage na kafungulia magazeti na hii itakuwa ndio wimbo wake huko ulaya. Endelea kubwabwaja.

she is the head of the state, ana hiyo mamlaka..

asingeyafungulia bado ungepiga kabobo tu..
ameyafungulia unapiga kabobo tu..
 
PIGA, UA, GARAGAZA ni lazima wakutane...

Siyo tu na Tundu Lissu bali na wakimbizi wa kisiasa wote i.e Godbless Lema, Roma Mkatoliki, nk walioko uhamishoni tokana na kukimbia utawala katili wa Mwendazake John Pombe Magufuli wanaweza kuwasili Ubelgiji wakati wowote kwa ajili hiyo...

Na mkutano huo utawezeshwa kuwepo na serikali ya Ubelgiji pamoja na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za wakimbizi wa kisiasa...

Kumbukeni pia ombi la Tundu Lissu mwezi April, 2021 la kutaka kuongea na Rais Samia na kukubaliwa lakini tokana na figisu figisu fulani hapo katikati toka kwa wahuni walio ktk circle ya kumshauri Rais wakavuruga ile appointment. Sasa inakwenda kutokea....

Angalieni na kuisoma vyema Press Release ya Ikulu kupitia msemaji wake Zuhura Yunus, inatoa ujumbe fulani kwa wafikiriao vyema...

For instance, PR hiyo imesema kila kitu ambacho Rais atafanya akiwa Ufaransa. Lakini anakwenda kufanya nini Ubelgiji, PR iko kimya. Mpaka hapo, akili kumkichwa..!

Huyu mwanamke (Rais Samia) anaweza kuwa very intelligent. Ameshagundua kuwa kuna watu ndani ya inner circle yake ya ushauri wanamhujumu. Sasa ameamua sometimes ajiongeze mwenyewe...!
 
Huo ubongo wako ni mzigo tu kichwani. Nakushauri utoe
 
  • Kicheko
Reactions: Pep
Anaweza kukutana nae kama diaspora wengine kawaida tu.huyo mtu wenu kule ni Mkimbizi wa kawaida tu hana lolote.
 
Ni kawaida kwa Marais wa Tanzania kukutana na Watanzania wanaoishi kwenye nchi ambazo viongozi hao hufanya ziara za kiserikali, kwa mfano , Mama alipofika nchini Marekani alikutana na Watanzania wanaoishi huko, akiwemo Mwanaccm Mange Kimambi na kisha kubadilishana nao mawazo.

Sasa uzuri wa Bahati ni kwamba Mama amefanya ziara nyingine kwenye nchi za Ufaransa na Belgium, tunaamini kwamba akishafika huko atakutana na Watanzania walioko huko na kubadilishana mikakati.

Swali langu dogo ni hili, Je Mh mama akifika Ubelgiji atakutana na Tundu Lissu ambaye ni miongoni mwa watanzania wanaoishi huko?
Mh Lissu ile mashine, wanaweza kukutana ili Hali liwepo Jambo la msingi vinginevyo mh Lissu hauwezi angaika na kuacha Mambo yake, chezea lissu wewe
 
Sidhani kwa akili za TL anaweza kwenda kukutana na mama. Sababu kubwa ambayo lisu nilivyomprofile ni kwamba kina lisu wameomba kukutana na mama muda mrefu hata kina mnyika wanaomba hayo lakini walikuwa wakipuuzwa sasa Lissu ataona ni kama kujipendekeza wakati yeye anataka haki itendeke.

Na kama wakikutana ni sababu mabeberu watafurahi Lissu akikutana na mama chini ya mediators wa Umoja wa ulaya. Asikwambie mtu ukiwa upande wa mabeberu kuna raha sana.
 
Back
Top Bottom