Je, tupo kwenye dakika za lala salama unabii wote wa biblia umeshatimia ?

Maelezo yanajitosheleza kabisa,
 
Mkuu mbona hakuna historia ya kaisali kushusha moto wala chapa yake kutumika katika kuuza na kununua bidhaa?
 
Mkuu mbona hakuna historia ya kaisali kushusha moto wala chapa yake kutumika katika kuuza na kununua bidhaa?
Chapa ilikuwa ni muuli wa mamlaka ya kaisari mkuu ulikuwa ni lazima uoneshe muhuri wa kasiari ndio uweze kuuza au kununua na lazima ukifanya ibada lazima uwekewe alama kwamba ulifanya ibada ya kaisari tafuta historia ipo.


Huyu kaisali alakuwa kama mungu, bila shaka analingana na ile pembe ndogo, alikuwa anafanya miujiza huku kufanya miujiza maana yake ni ishara flani ili kuwaaminisha watu kuwa yeye anafanana na mungu kama manabii wa hivi leo wanavyofanya miujiza au waganga na wachawi.


Masuala ya miujiza yalikuwepo tangu kipindi cha musa kule misri waganga walikuwa wanaweza kubadirisha fimbo kuwa nyoka, hivyo nafikiri unanielewa.


Katika kipindi cha dola la roma kulikuwa na miujiza na wachawi, kulikuwa na teknolojia kidogo ya kutengeneza majengo marefu na sanamu mengine yapo hadi hivi leo kuna mambo mengi sana yalifanyika kwenye dola hilo katili.
 
Swali lako ni zuri sana kwa sababu linagusa siasa, dini na uchumi wa Dola la Roma, hasa katika enzi za Kaisari (Imperial Rome). Hebu nikuelezee kwa hatua:


1. Biashara na “muhuri wa Kaisari”​


  • Ni kweli kwamba dola ya Rumi ilikuwa na mfumo mkali wa udhibiti wa kodi na biashara.
  • Siyo kwamba kila mfanyabiashara alihitaji muhuri wa Kaisari binafsi, ila biashara nyingi zilihitaji kibali rasmi kilichokuwa na alama au muhuri wa kiserikali.
  • Muhuri wa Kaisari au wa serikali uliashiria mamlaka – mfano kwenye sarafu zote lazima iwe na picha au jina la Kaisari. Hii ilimaanisha kwamba biashara yoyote kubwa (hasa ile ya kimataifa au ya kiserikali) ilikuwa chini ya nembo yake.
  • Wale waliokuwa wakisafirisha bidhaa walihitaji hati zilizoidhinishwa, na mara nyingine mihuri ili kuhakikisha usalama wa bidhaa na ulipaji kodi.
    👉 Kwa lugha ya mfano, hakuna biashara kubwa iliyoweza kusimama bila “kibali cha Kaisari.”

2. Ibada kwa amri ya Kaisari​


  • Kuanzia karne ya 1 KK (baada ya Julius Caesar na hasa Augustus), ibada ya Kaisari ilianza rasmi – ilijulikana kama Imperial Cult.
  • Hii haikuwahi kabisa kuchukua nafasi ya dini zote, bali ilikuwa ishara ya utii wa kisiasa.
  • Katika majimbo mengi ya Dola, kulikuwa na mahekalu, sanamu na sikukuu kwa heshima ya Kaisari.
  • Ilikuwa jambo la lazima kwa raia kushiriki ibada hizi au kutoa sadaka ndogo kama ishara ya uaminifu.
  • Wale waliokataa (hasa Wakristo wa kwanza) walionekana kama wasaliti au waasi wa dola. Hii ndiyo sababu ya mateso ya Wakristo, kwa kuwa walikataa kusema “Caesar ni Bwana,” wakashikilia “Yesu ni Bwana.”

Kwa ufupi​


  • Biashara kubwa ilihitaji kibali au nembo ya Kaisari (mfumo wa kisheria na kifedha ulikuwa chini yake).
  • Ibada kwa Kaisari ilikuwa ya lazima kama ishara ya utii wa kisiasa, siyo tu ya dini ya hiari.

🔑 Hivyo Kaisari alikuwa siyo tu kiongozi wa kisiasa, bali pia nembo ya uhalali wa biashara na mshindi wa ibada ya heshima.


Unataka nikutafutie maandiko ya kihistoria (labda kutoka Tacitus, Suetonius, au maandiko ya Wakristo wa kwanza) yanayothibitisha haya kwa undani zaidi?


Haya ni majibu kutoka kwa Chatgpt.

Ubarikiwe Genius Man
 
LGBTQ+ NA VATICAN: MLANGO MTAKATIFU, LAVENDER MAFIA, PADRE JAMES MARTIN NA SIRI ZILIZOJIFICHA

Biblia inasema

“Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.” (Ufunuo 17:5)

Biblia mara nyingi inafanya mfano wa mwanamke kwa Kanisa. Mwanamke safi anawakilisha Kanisa safi, lakini mwanamke kahaba ni mfano wa Kanisa lililopotoka.

Wengi wamefasiri kwamba “Babeli Mkuu” ni ishara ya Kanisa lililopotoka hasa Roma, mji wa milima saba, kitovu cha mamlaka ya Kipapa kwa karne nyingi.Na ukweli ni huo

Leo nitagusia tukio la Juzi 6 September na la Jana 7 September huko Roma ,Vatican. Hili tukio halitakiwi kupita hivi hivi kwasisi wachambuzi wa dini ,madhehebu na mambo ya Kiroho .

Katika Mwaka wa Jubilei wa 2025, kundi la mahujaji kutoka jamii ya LGBTQ+ liliruhusiwa rasmi kupita katika Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro, likiongozwa na vikundi vya Kikatoliki vya LGBTQ. Tukio hili lilionekana kama ishara ya kukubalika wazi kwa watu wa jinsia moja ndani ya ibada rasmi za Vatican.

Kwa upande mmoja, tukio hili lilichukuliwa kama ishara ya upendo.

Kwa Sisi wachambuzi huru mambo ya dini na vituko vyao, linaashiria hatua za Ufunuo zinazoonyesha kahaba mkuu anayeendelea kupamba uso wake kwa miale ya kidini huku akibeba ajenda za dunia.



PADRE JAMES MARTIN NI NANI?

Huyu ni mlezi wa mashoga ndani ya Kanisa Katoliki na ana baraka za Papa Francisco marehemu na Sasa amekutana na Papa Leo,

Padre James Martin, S.J., ni MJesuit, amejulikana kwa kazi yake na jamii ya LGBTQ+ kupitia maandishi, mihadhara na huduma zake .

Kwa wafuasi wake, yeye ni sauti ya huruma na upendo; kwa sisi wachambuzi huru,wahafidhina ni ishara ya mlango unaofunguliwa kwa ajenda inayopingana na mafundisho ya Biblia.
Mlezi wa mashoga katika kanisa Katoliki katika picha na Papa

Hii ni picha ya Papa Leo XIV akiwa na Padre James Martin, mlezi maarufu wa jamii ya LGBTQ+ ndani ya Kanisa Katoliki



Picha hiyo ilipigwa katika Maktaba ya Kitume ya Ukumbi wa Kipapa (Apostolic Palace) alikokutana rasmi Papa na Padre Martin tarehe 1 Septemba 2025.

Papa na Padre Martin tayari wanajulikana kwa ushirikiano wao wa karibu wa kisiasa na kiroho. Martin ni kuhani mlezi wa makundi ya LGBTQ+ ndani ya Kanisa Katoliki.

Kulingana na Padre Martin, aliona ujumbe uliotolewa kutoka kwa Papa Leo kuwa ni wa “uzima wa uwazi na kukaribisha,” sawa na ule wa Papa Francis, na alisema: “Todos, todos, todos.” (Wote, wote, wote).

Padre martin aliwahi pia kukutana na Marehemu Papa Francisco ambaye alikuwa anapenyeza sana ajenda ya Mashoga ndani ya katoliki


Kanisa Katoliki limeanza kutumia lugha ya “huruma”, “ukaribisho”, na “kujumuisha” badala ya kuzungumzia adhabu au kuwakanya MASHOGA waache hizo Tabia .

Sisi wachambuzi huru,wahafidhina wa dini tunasema hii ni mbinu ya gradualism , hatua ndogo ndogo za kupunguza upinzani hadi kufanikisha mabadiliko makubwa.


LAVENDER MAFIA — SIRI ZA NDANI YA VATICAN
“Lavender Mafia” ni mtandao wa siri wa makasisi na maofisa wa Vatican wanaodaiwa kuwa mashoga au kuunga mkono ajenda ya LGBTQ.

Wanaoshirikiana na kuhusika katika kulinda watu fulani, kushinikiza sera, na kudhibiti maamuzi ya Kanisa.,

Siri zinazojificha ni pamoja na

• Kesi na kashfa za ngono miongoni mwa makasisi zilizofichwa kwa muda mrefu.
• Mtandao wa kulindana kwa siri, ukijulikana kama Lavender Mafia.
• Uhusiano wa Kanisa na ajenda pana ya kisiasa ya ulimwengu (“New World Order”).
• Matumizi ya alama na ibada zinazohusiana na nguvu za kishetani kama ilivyoelezwa katika unabii.

Wachambuzi wa kiunabii wa kihistoria (historicist) wanasema “Babeli Mkuu” wa Ufunuo 17 ni Kanisa Katoliki la Roma.

Sababu

• Ni mji wa milima saba (Roma).
• Ni mwanamke kahaba , ishara ya Kanisa lililopotoka.
• Amelewa damu ya watakatifu, kumbukumbu ya mateso ya waumini wakati wa karne za giza na Inquisition.(ZAMA ZA GIZA)

Mashuhuda wa kihistoria tuwasikilize wanasemaje

Martin Luther (1483–1546)-mwanzilishi wa kanisa la LUTHERAN na aliyewahi kuwa kasisi ndani ya Roman Catholic anasema👇👇

“Niliwahi kuogopa kuwa Papa ndiye mpinga Kristo; lakini sasa kwa kuona kazi zake, najua hakika ndiye ameketi pale Babeli, Babeli halisi na kahaba mkuu wa Ufunuo.”


John Knox (1514–1572):mwanamatengenezo na mwanzilishi wa kanisa la PRESBYTERIAN alisema👇👇


“Kanisa la Rumi ndilo kahaba mkuu wa Ufunuo. Ni kiti cha mpinga Kristo, na utawala wa Papa ndio Babeli ulioangamiza ulimwengu kwa unajisi wake.”


Sir Isaac Newton (1643–1727):
Mwanasayansi mashuhuri kuwahi kutokea duniani pia alijikita katika tafsiri za unabii, aliandika katika kitabu chake Observations upon the Prophecies of Daniel and the Apocalypse of St. John

Alisema 👇

Kwa mtazamo wa kihistoria, Kanisa Katoliki ndilo kahaba mkuu, mama wa makahaba, lililojivika dini lakini likipinga ukweli wa Neno la Mungu na kuwatesa watakatifu wake.

Sehemu nyingine anasema

“Kanisa la Rumi ni ule mpinga Kristo wa unabii, Babeli Mkuu wa Ufunuo, kahaba aliyelewa damu ya watakatifu. Hii haipaswi kutiliwa shaka na yeyote anayesoma unabii kwa makini.

John Wesley (1703–1791) –Mwanamatengenezo pia Mwanzilishi wa Kanisa la Methodisti alisema:👇👇

“Kanisa la Roma ndilo kwa hakika Babeli Mkuu, mama wa makahaba. Ndiyo mfumo ambao unabii unamwonyesha kama chanzo cha ufisadi na mateso kwa watu wa Mungu.”


Tukio la mahujaji wa LGBTQ+ kupita Mlango Mtakatifu linaashiria namna alama za unabii zinavyotimia hatua kwa hatua.

Biblia inasema na inatuonya

“Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” (Ufunuo 18:4)

Wito wa Mungu ni kujitenga na Babeli Mkuu na kushikamana na Neno la Mungu lisilobadilika
 
GUYS GUYS GUYS! !

WHAT A TIME TO BE ALIVE! LOOK UP!


View: https://youtu.be/NYYwMQYqI7g?si=E4FYZ2ai1EjcRYBg
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…