Je, tutarajie Rais Samia Suluhu kumrudisha Paul Makonda tena kwenye mfumo wa siasa?

Hamna hata mtu mmoja anasema kwamba Makonda anafaa kuwa kiongozi....Huyo mtaani kwao tu anapoishi hajapewa hata ukatibu wa nyumba 10....Atulie kwa sasa na afanye kazi zingine na sio siasa...
 
Kijana aliye na maisha ya raha kuliko vijana wote nchini....
Alijisahau saana akajiona na yeye ni mtawala!! Alichomfanyia kada mwenzake Nape si cha kiuungwana kabisa!!
Hivi mpaka leo hawapatani hawa??
 
Mtu ambaye anasemwa kawabambikia watu kesi za madawa ili kujipatia fedha na mali,mtu anayetajwa kuhusika na kupotea watu na ukatili wa kila aina hayo ndio mapungufu kidogo?
Hafai kabisaa na kulikuwa na mauaji ya ajabu ajabu mengi sana kipindi kile....
 
Kijana aliye na maisha ya raha kuliko vijana wote nchini....
Alijisahau saana akajiona na yeye ni mtawala!! Alichomfanyia kada mwenzake Nape si cha kiuungwana kabisa!!
Tumekubaliana hayo yashapita, tunaanza upyaa
 
Hamna hata mtu mmoja anasema kwamba Makonda anafaa kuwa kiongozi....Huyo mtaani kwao tu anapoishi hajapewa hata ukatibu wa nyumba 10....Atulie kwa sasa na afanye kazi zingine na sio siasa...
Watu wa humu huwajui? Humu hata diamond hawezi kupata kura 10, watu wa humu ni......
 
Mtu ambaye anasemwa kawabambikia watu kesi za madawa ili kujipatia fedha na mali,mtu anayetajwa kuhusika na kupotea watu na ukatili wa kila aina hayo ndio mapungufu kidogo?
Maneno tu hayo hakuna ushahidi
 
Yaani Makonda kabisa???
Mnapo andika hivi vitu mna kuwa mmetumwa au mna kuwa mmevuta bangi?
Mnamjua Makonda na makando kando yake au mnamjua kwa sura yake?
Hebu tafuteni mada za kuweka hapa na muachane na wafu wazikwe waliko fia.
Wapambe nuksi wapo mzigoni kumchanganya maza
 
Unawaza Nini?tumrudishe dar? Funguka kijana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…