kibobori mahoro
JF-Expert Member
- Dec 12, 2022
- 7,452
- 10,785
Tatizo ni marupurupu hasa yale ya upigaji! Utauza chaki? Utapewa rushwa ya nini? Kwa ujumla hakuna pesa nje ya mshahara. Angalia TRA mwisho tu wa siku anatoka na kitita.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😂Tatizo ni marupurupu hasa yale ya upigaji! Utauza chaki? Utapewa rushwa ya nini? Kwa ujumla hakuna pesa nje ya mshahara. Angalia TRA mwisho tu wa siku anatoka na kitita.
Mwanasheria anapata posho gani halmashauri?Mwalimu halmashauri anaeanza ni 822,000/= ni sawa na mwanasheria wa halmashauri hawapishani Sana, SEMA kwenye ualimu ni dry hakuna posho n.k
Uko sahihi kabisaKusema ukweli Ualimu kutoboa mfano nyumba Kali 2,gari angalau Harrier na mlo draft =Never. Ukiachana na pesa kiduchu lkn majungu na kuoneana wivu pindi mmja anapopambania maisha yakee.
Fikilia mtu unatoka shule saa11 eti mnapambana watoto wafaulu,Mwisho wa mwezi laki 4. Familia inaitaka pesa ndugu wanaitaka pesa,nguoo kukeep status Ongeza na michepuko.
Pia ukijishugulisha na Biashara ikashine,ukikaa vibayaa unahamishwa wapo unapelekwa chakaa ambako hutofanya chochote ubaki kufunfishaa tu hapoo umasknii milelee.
Hivyobasi Ili Tasnia ya Ualimu iheshimike lazima Kuna mambo yawekwe sawa:
1.Ongezeko la mshahara 2.Kazi Mwisho saa 8 mchana weekend Free watu wapate mdaa wakujitafutia kipatoo.3.walimu certificate wote waondolewe kwenye system,Hawa ndo walevii mpaka chokaa mtu mpaka anajikojolea au mademuu haswaa familia hawajali.4.pia wale maafisa wajitambue sio kusikiliza majungu na wivu hovyoo na kuhamisha hamisha kiipuzi.All in all Ualimu nikazi Yaa Amani sana kama mtu unajielewa na upo Eneo zuri.
Nimesoma kichwa cha habari tu, na ninakijibu kama ifuatavyo,Leo nimejisikia vibaya Sana baada ya kumsikia Mzazi mmoja akimgombeza Mtoto wake aliyekua na ndoto ya kusomea ualimu, maongezi yao yalikua hivi.
Mtoto: baba Mimi nataka kusomea ualimu.
Baba: hivi umechanganyikiwa? yaani uende ukawe Mwalimu? Walimu Wana maisha gani? Eeeh! Wana kipi Cha maana? Sitaki kusikia hizo habari zako Bora ukaombe chuo Cha diploma uombe hata clinical officer nitalipa ada.
Yale maneno yamenifanya nitafakari Sana, kundi la walimu linaonekanaje? Mbona wapo wengi wenye uwezo? Hivi Kuna mtu yoyote anatamani angelikua Mwalimu? Je kutopewa heshima kwa walimu inasababishwa na nini? Je ni ugumu wa kazi? Au salary ni ndogo? ..
Mwisho, unaweza kuruhusu mtoto wako asomee ualimu?
Wapo wanaofurahia kazi ya ualimu ila kwa wanaofuata maslahi lazima uichukie hio kazi maana hamna utakachokipata zaidi ya kuishi umri mrefu tu sababu ya kula vyakula vya asili na kufanya mazoezi ya baiskeli na kusimama muda mrefu kila siku.Sasa Kwa hizo sababu kwa nini watu waendelee kuipenda hyo kazi SI ya laana hiyo akuna kitu kipo sawa
Walimu wenye akili hio ni 0.0005% ya population yote ya walimu.Ualimu ni fani moja nzuri na yenye soko kubwa kama utajua namna ya kujiongeza. Kwasababu kila siku watu kuna jambo wanataka kulifahamu so watahitaji mwalimu wakuwafundisha.
Tatizo ni kuwa vijana wengi wanaohitimu ualimu wanabaki kuwa waalimu wa masomo waliyosomea chuo utasikia mimi mwalimu wa jiografia mara kiswahili au sayansi, wameshindwa kutumia ujuzi na maarifa yao ya kufundisha kufundisha wqtu mambo mbali mbali.
Mfano, kama mtu kasoma ualimu alafu akajielimisha juu ya matumizi ya AI labda ChatGTP au hata sanaa fulani kama muziki au jambo lolote akawa na ufahamu wa hilo jambo anauwezo wa kuhamisha ufahamu au ujuzi wake huo kwa watu wakamuelewa na kumlipa.
Kifupi ukisoma ualimu ukahitimu wafundishe watu vile unavyovifahamu au kuwa na kipaji navyo serious kwa kutumia maarifa ya ufundishaji uliyonayo.
Najua ni ngumu na pengine nikaonekana motiveshno spika ila bila kuwqza nje ya box mwqlimu hauwezi kutoboa japo ndio fani yenye wateja wengi kuliko fani zingine zote.
Umeshindwa yote anzisha basi twisheni au homework aider kwa njia ya digitali uwe unafanya mambo kama mtaaluma sio mbabaishaji, watu wana smartphone wanaweza kutumia na watoto wao. Ujue sio kila mzazi anajua kutafuta kipenyo a kipeuo, why asijiunge na program yako kama inamuondolea aibu ndogo ndogo na mwanae anapata elimu.
Watakulipaje, jisajili Lipa kwa simu kuwa na website na App ya android na Ios fanya kazi kama msomi. Vaa vizuri, eneo la ofisi smart, tumia kamera quality, set up nzuri usikike vizuri, engage na mteja wako. Nusu saa Tsh. 200 hapo una wateja 10+
Ila uandae mtaji wa kama milioni tatu, maana hakuna biashara ya maana isiyo na mtaji wa pesa.
Kwa atakayeokota jambo haya, kila la heri ndugu mwalimu
Mindset za watu tu
Hakika...Mindset za watu tu
Asikudanganye mtu!kazi yeyote inamtoa mtu inategemea nidhamu, Baraka na kutokua na mikosi ya kuuguza hasara n.k!Leo nimejisikia vibaya Sana baada ya kumsikia Mzazi mmoja akimgombeza Mtoto wake aliyekua na ndoto ya kusomea ualimu, maongezi yao yalikua hivi.
Mtoto: baba Mimi nataka kusomea ualimu.
Baba: hivi umechanganyikiwa? yaani uende ukawe Mwalimu? Walimu Wana maisha gani? Eeeh! Wana kipi Cha maana? Sitaki kusikia hizo habari zako Bora ukaombe chuo Cha diploma uombe hata clinical officer nitalipa ada.
Yale maneno yamenifanya nitafakari Sana, kundi la walimu linaonekanaje? Mbona wapo wengi wenye uwezo? Hivi Kuna mtu yoyote anatamani angelikua Mwalimu? Je kutopewa heshima kwa walimu inasababishwa na nini? Je ni ugumu wa kazi? Au salary ni ndogo? ..
Mwisho, unaweza kuruhusu mtoto wako asomee ualimu?
Wiki iliyopita nilikua nafanya ishu moja na waalimu, aisee walimu wanapigana sana majungu waume kwa wake. Sijui wana matatizo gani ni kama vile watoto wadogo. Mpwayungu Village atusaidie tatizo ni nini kwa hawa ndugu zakeWalimu wenye akili hio ni 0.0005% ya population yote ya walimu.
Walimu wanaotoboa wengi ni wale waliojiongeza, wamiliki wa stationeries za shule kama madaftari na kalamu. Anajiongeza anaweka na picha za passport kisha anahamia kwenye u MC kabisa. Hao ndio waalimu waliotoboa na wana maisha mazuri.
Wengi akili zao zinakuwa za kitoto kama wanafunzi wao tu. Wanapigana mashine sana piaWiki iliyopita nilikua nafanya ishu moja na waalimu, aisee walimu wanapigana sana majungu waume kwa wake. Sijui wana matatizo gani ni kama vile watoto wadogo. Mpwayungu Village atusaidie tatizo ni nini kwa hawa ndugu zake