Je, ualimu ni kwa ajili ya watu maskini?

Je, ualimu ni kwa ajili ya watu maskini?

Leo nimejisikia vibaya Sana baada ya kumsikia Mzazi mmoja akimgombeza Mtoto wake aliyekua na ndoto ya kusomea ualimu, maongezi yao yalikua hivi.

Mtoto: baba Mimi nataka kusomea ualimu.

Baba: hivi umechanganyikiwa? yaani uende ukawe Mwalimu? Walimu Wana maisha gani? Eeeh! Wana kipi Cha maana? Sitaki kusikia hizo habari zako Bora ukaombe chuo Cha diploma uombe hata clinical officer nitalipa ada.

Yale maneno yamenifanya nitafakari Sana, kundi la walimu linaonekanaje? Mbona wapo wengi wenye uwezo? Hivi Kuna mtu yoyote anatamani angelikua Mwalimu? Je kutopewa heshima kwa walimu inasababishwa na nini? Je ni ugumu wa kazi? Au salary ni ndogo? ..

Mwisho, unaweza kuruhusu mtoto wako asomee ualimu?
Wangekuwa Masikini wangemchangia Mama kununua Fomu ya Urais? Sio Watu masikini bali ni Wajinga

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Uzuri ni kwamba hata wawaponde walimu kiasi gani, kila mwaka vyuo vya ualimu vinasajiri wanafunzi wengi sana kuanzia certificates hadi degree,.. Penda na heshimu kazi yako mkuu asitokee mtu wa kukukatisha tamaa, kuna walimu wako mtaani wana vyeti wanatamani hata wapate mahali wafundishe part time lakini wamekosa...Jivunie ulichonacho💪💪
Ivo yaan....watajijua...maana wanaponda wakati hawatuongezei hata mia😉
 
Leo nimejisikia vibaya Sana baada ya kumsikia Mzazi mmoja akimgombeza Mtoto wake aliyekua na ndoto ya kusomea ualimu, maongezi yao yalikua hivi.

Mtoto: baba Mimi nataka kusomea ualimu.

Baba: hivi umechanganyikiwa? yaani uende ukawe Mwalimu? Walimu Wana maisha gani? Eeeh! Wana kipi Cha maana? Sitaki kusikia hizo habari zako Bora ukaombe chuo Cha diploma uombe hata clinical officer nitalipa ada.

Yale maneno yamenifanya nitafakari Sana, kundi la walimu linaonekanaje? Mbona wapo wengi wenye uwezo? Hivi Kuna mtu yoyote anatamani angelikua Mwalimu? Je kutopewa heshima kwa walimu inasababishwa na nini? Je ni ugumu wa kazi? Au salary ni ndogo? ..

Mwisho, unaweza kuruhusu mtoto wako asomee ualimu?
Wakitaka kujua umuhimu wa walimu, shule na vyuo vifungwe hata kwa miezi 6
 
Uzuri ni kwamba hata wawaponde walimu kiasi gani, kila mwaka vyuo vya ualimu vinasajiri wanafunzi wengi sana kuanzia certificates hadi degree,.. Penda na heshimu kazi yako mkuu asitokee mtu wa kukukatisha tamaa, kuna walimu wako mtaani wana vyeti wanatamani hata wapate mahali wafundishe part time lakini wamekosa...Jivunie ulichonacho💪💪
hujambo binti yangu
 
Mkuu mbona kama umekasirika ? Pia upo sahihi.
Sipendi mtu anayedharau kitu asichokijua Kwa undani.

Ndio maana Kuna usemi unasema kuweza kwako kiswahili ndio ujinga wako kwenye kiingereza.

Maana yake daktari ukimpa mtu amfundishe nayeye na udaktari wake wote anakua box tu anaweza asifanikiwe kuimpart knowledge Kwa mtoto ipasavyo.

kwahyo mtu asidharau kazi Fulani kana kwamba ni yakawaida wakat akipewa hawez kufanya Kwa ufanisi ambao angeufanya muhusika.

Mm kwenye Maisha yangu hata housegirl wangu siwezi mdharau kwasababu najua siku akiamua kugoma ndani tunaweza tusile chakula Kwa wakati, au akiamua kuweka sumu kwenye msosi tunaweza zikwa kama kuku.

Nachukia sana kazi ya ualimu ikidharauliwa wakati katika mataifa yaliyoendelea ni miongoni mwa kazi special sana.

Ndio wale wanasemaga yule demu malaya sana nenda kamtongoze kama naww atakukubalia.
 
Ualimu ni shida uko akuna posho, akuna pesa ya kinywaji, akuna pesa ya pango, pesa ya likizo mbaka uende ukadeki pagala la mkurugenzi na akuchapie mkeo ndo upate, promotion mbaka ukaroge, seminar mbaka umuonge mkuu wa shule na afisa elimu, kusimamia mitihani 10% Kwa mkuu, kuenda mark mbaka yesu aludi, mikwara kibao shule aina computer lakini mkurugenzi anataka mtoe A za SoMo la computer, ata mjumbe wa nyumba kumi bosi wako anaweza akaja shule akakufokea Kwa Nini ofisi chafu aujadeki na ikiwezekana kama una kimwili kidogo anakulamba na viboko vitatu vya nguvu, pesa ya mwenge utaki unataka utatoa, makato ya Cwt unayataka uyataki itakatwa TU lete fyoko ushughulikiwe
Kma Kuna watu wanapaswa kushukuru jitihada za mwalimu ww jamaa ulipaswa kuwa mmoja wapo maana nikisoma hii handwriting Yako naona Namna Gani mwalimu alipambana sana Kwaajili Yako.

Laiti angeyazingatia hayo yaliyojaa kwenye ubongo wako akaacha kupambania baadae Yako. nakuhakikishia hata space ungeshindwa kuacha kwenye sentence zako.

Nakuibia Siri moja mwalimu ndio mfanyakazi pekee anayepanda cheo bila kwenda coarse.
 
Wewe jamaa kupanda cheo bila coz ndo kitu Cha kukushangaza Tena vyeo venyewe mbaka mwanasiasa acheke ndo mpande?
Wenzio uko wanaposho ya ujuzi na auna kazi na Wala awajawai kuufanyia KAZI kwenye vitengo walivyoajiriwa
 
Nafikiri moja ya sababu inayopelekea ualimu kudharauliwa ni alama anazopata mtu ili kujiunga na ualimu,mfano mnamaliza kidato Cha sita kwa masomo ya sayansi,waliofaulu zaidi ndio huchukuliwa kwenye fani kama za afya,uhandisi n.k,lakini wale wenye ufaulu mdogo ndio watachukuliwa uwalimu,sababu nyingine ni mshahara mdogo na mazingira yao ya kazi kutoboreshwa,hii nchi sijaiona mwalimu kijana mwenye hela zaidi ya TEACHER KONDE [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Walimu wenyewe ndo wanafanya kada yao isiheshimike wanatumia kisiasa baada ya hapo wanatupwa jalalani, mzazi jeuri, Mwenyekiti wa mtaa, mtendaji, wakurugenzi, police, waratibu, makamishna na wengn wakiamua wanampiga biti mwalimu na Hamna kitu atafanywa!

Juzi wakuu wa shule wamemcha.........

Walimu heshimisheni kada yenu
 
Wewe jamaa kupanda cheo bila coz ndo kitu Cha kukushangaza Tena vyeo venyewe mbaka mwanasiasa acheke ndo mpande?
Wenzio uko wanaposho ya ujuzi na auna kazi na Wala awajawai kuufanyia KAZI kwenye vitengo walivyoajiriwa
Mshukuru sana mwalimu wako

Maana maandishi Yako bado yananipa mashaka unapata wapi ujasiri wakudharau ualimu uliokufuta tongotongo hata unaweza kusoma japo msg zangu na bado huelewi kilichoandikwa ila unajibu.

Vyenyewe ✓ Vyenyewe X
Hauna✓. auna X
Hadi✓. Mbaka X

Nenda kwanza katafute tuition usome ukijua kusoma na kuandika njoo nikupe tafsri ya neno cheo.

Wewe ndio wale hata maana ya neno maana hawaijui.
 
Nafikiri moja ya sababu inayopelekea ualimu kudharauliwa ni alama anazopata mtu ili kujiunga na ualimu,mfano mnamaliza kidato Cha sita kwa masomo ya sayansi,waliofaulu zaidi ndio huchukuliwa kwenye fani kama za afya,uhandisi n.k,lakini wale wenye ufaulu mdogo ndio watachukuliwa uwalimu,sababu nyingine ni mshahara mdogo na mazingira yao ya kazi kutoboreshwa,hii nchi sijaiona mwalimu kijana mwenye hela zaidi ya TEACHER KONDE [emoji23][emoji23][emoji23]
Hiyo ya waliofail ndio husomea ualimu nafikri unahitaji kufanya utafiti utakuwa huna taarfa za kutosha nenda Udsm hapo kaangalie wanalofanya Education je wamefail au Wana division 1&2

hiyo miaka ya waliofail kusomea ualimu ilishapita mkuu nowdays ualimu ni coarse inayohitaji pass mark nzuri kma umefail huwezi soma. Utamfundishaje mtoto wakati wew mwenyew umefail Sasa.?
 
Back
Top Bottom