Kwanza hayo mambo ya wanaosomea ualimu hawakufaulu vizuri sio kweli, nenda pale UD mlimani main campus na division two yako ya mwisho kaombe ualimu halafu uone Kama utapata, Kuna Watu Wana one zao nzuri na wanasomea Ualimu.
Issue ya mshahara pia inategemeana na mwalimu wa shule gani/sekta ipi, Kuna shule X mitaa ya Tabata walimu wanalipwa milioni kadhaa na Wana push mikoko ya maana kweli kweli.
Shule Kama Feza, Baobab, Kaizirege n.k mishahara ya hao waalimu sidhani Kama kipato chako kinaingia hapo.
Kuna waalimu wamejiongeza wanafanya issue zao na wanafundisha na wana maisha Safi tu.
Mwalimu pia ni mtumishi ambae kupitia kituo chake Cha kazi anaweza kutengeneza 'mifumo' ambayo itamsaidia asiguse mshahara wake.
Unasema hujaona mwalimu mwenye hela hapa mjini hujui kuwa MC Gara B ni mwalimu, A teacher by Profession...😅
Ndugu being a teacher is not a bad thing, Sana ni blessing ambayo ikitokea 'ukijiongeza vyema' unaweza kutoboa tu, bila kuiba wala kuvunja Sheria.